Kihoro kikubwa cha kuogofya cha mwanaume(Men's worst nightmare)

Wewe unaishi kwenye nadharia za social media za akina Andrew Tate na redpill, siyo uhalisia wa maisha ya Kitanzania ya sasa.
 
Na mimi hoja yangu haijajikita katika kufukuzana tu ndani ya nyumba kama kuku.

Soma uelewe.

Kufukuzwa kwa aina yoyote.

Mtu umuoe mwenyewe. Akuzingue?

Kuna sehemu lazima utakuwa umefeli.

Na ndio mada inalenga hayo maeneo ambayo mwanaume amefeli au kama hajafeli basi anayahofia au yanampa shinikizo na kujiona duni au mnyonge.

Ndio maana mwanume anapaswa achunge
a) Afya yake.
b) Kipato chake
c) Himaya yake.
Lazima afuatilie na ajue mipaka ya himaya yake na waliomo ndani yake wote awatawale.

Ukikosa hayo au mojawapo lazima mwanamke anaweza kukufanya chochote
 
tatizo la upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction - ED) lipo na linazidi kuongezeka siku hadi siku.
Hili si tatizo la kipekee kwa eneo hili tu, bali ni changamoto ya kiafya inayowakabili wanaume wengi duniani kote kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha, magonjwa, na sababu za kisaikolojia.
 
Wewe unaishi kwenye nadharia za social media za akina Andrew Tate na redpill, siyo uhalisia wa maisha ya Kitanzania ya sasa.

Ningekuwa sijaoa ungekuwa sahihi.
Maana wengi mnakimbiliaga huku.
Ooh ukiwa mkubwa utajua.
Oooh! Ukioa utajua!

Nilichosema nimesema.
Ukiona mtawala yeyote au nyumba yoyote imeanguka ujue tatizo lipo kwa mtawala. Na kwa level ya familia tatizo lipo kwa mwanaume mwenyewe.
 
Safi sana sasa hapa umerudi kwenye mstari! Kumbe unajua kuwa mwanaume anaweza kufeli na mwanamke akamfanyia chochote?

Hiyo ndo pointi yangu tangu mwanzo.
 
Basi endelea kuishi na mkeo kama mateka wako.
 
Safi sana sasa hapa umerudi kwenye mstari! Kumbe unajua kuwa mwanaume anaweza kufeli na mwanamke akamfanyia chochote?

Hiyo ndo pointi yangu tangu mwanzo.

Na ndio pointi ya Kiranga ilipo.

Ni kwamba ni mpaka mwanaume afeli ndipo afukuzwe ndani ya nyumba.

Ndio maana Kiranga anakuambia labda huyo mwanaume awe hana Akili(zoba) au Kapuku FC
 
Nimekuelewa sana, hoja yako ni kwamba mwanaume akiwa na pesa na akili ana control yote.

Si ndio ulicho kimaanisha toka mwanzo wa reply yako kwenye comment yangu?
Sasa kama nakubali mwanamme anaweza kuachwa anakuwaje na control yote?

Wapi imesema mwanamme ana control yote?

Control yote maana yake ni nini?

Mwanamme akiachwa na mwanamke na kuamua kuendelea kivyake na kujiongeza kwingine, kwa sababu ana akili ya kujua hapa tumeshindwana na ana pesa ya kuweza kulianzisha kwingine, hapo ana control yote kivipi wakati kaachwa?
 
Unapoambiwa uishi na mwanamke kwa akili. Wanamaanisha Akili za mwanaume halisi✍🏿
 
Sasa kama nakubali mwanamme anaweza kuachwa anakuwaje na control yote?

Wapi imesema mwanamme ana control yote?

Control yote maana yake ni nini?
Kurahisha, hemu sema hasa pointi yako iko wapi?
 
Na ndio pointi ya Kiranga ilipo.

Ni kwamba ni mpaka mwanaume afeli ndipo afukuzwe ndani ya nyumba.

Ndio maana Kiranga anakuambia labda huyo mwanaume awe hana Akili(zoba) au Kapuku FC
Unajua wewe unafeli wapi? Pointi haikuwa kama mwanaume amefeli au hajafeli. Mada ya Mshana Jr inazungumzia nightmares tunazopitia wanaume.

Hata uwe na akili na mabilioni, hofu ya kusalitiwa au kufanyiwa paternity fraud ipo palepale. Kwani matajiri hawafanyiwi huo udanganyifu?
 
Kurahisha, hemu sema hasa pointi yako iko wapi?
Point yangu ni kwamba.

Mwanamme mwenye akili na pesa.

1. Anakuwa makini sana kwenye uchaguzi, haangukii kwa mwanamke anayeweza kumkataa kirahisi.

2. Lakini umesema watu si roboti, na hawatabiriki kirahisi hivyo. Sawa, inawezekana mwanamke akabadilika. Lakini hata mwanamke akibadilika, mwanamme mwenye akili na pesa anatakiwa ama kuweza kumbadili tena mwanamke ama kujua kuwa hapa mwanamke kashabadilika hatuwezi kuendana, na kukubali kuachwa/kuacha, na kuanzisha maisha kwingine bila tatizo.

Hujaelewa wapi hapo?
 
Nimekuelewa lakini pointi yako ya kwanza inafanya kazi kwenye nadharia tu. Hakuna mwanaume anayeoa akijua huyu mwanamke atakuja kumkataa au kumletea nyodo baada ya miaka 10.

Wote huwa tunakuwa makini wakati wa kuchagua, lakini maisha yana tabia ya kumbadilisha mtu.
 
Point yako ni non sequitur logical fallacy.

Hakuna mtu anayejua kwa uhakika kuwa kesho atakuwapo, lakini hilo halituzuii kupanga maisha ya kesho.

Sijasema kwamba mwanamme anatakiwa kupanga kuwa na mwanamke ambaye ana uhakika 100% kuwa hawezi kumuacha.

Ila hilo halimaanishi kuwa mwanamme (au hata mwanamke for that matter) hawezi kuwa na chujio la kuchuja vicheche wa wazi kabisa ambao ukiwaangalia hapa unajua hamna kitu.

Objective si kutafuta mwanamke ambaye kamwe hatakuletea matatizo. That is against the laws of physics.

Objective ni risk minimization.

Wanaume wengi wanaangalia mwanamke mwenye makalio makubwa, mwenye sura nzuri, wengine mwenye pesa, kuliko kuangalia risk minimization katika mahusiano.

Yani kuna risk minimization fulani mwanamme ukishafanya, mfano ukishafikisha 98% ya vigezo, hiyo iliyobaki inakuwa sawa tu kuwapo, kwa sababu hakuna kitu kilicho 100%.

Ndiyo maana kwenye uchumi kukiwa na 5% unemployment wanahesabu hiyo ni full employment. Kwa sababu hiyo 5% inakuwa katika margin of error kui control ni kazi sana. Hawatafuti 100% employment ili waseme hapa kuna full employment.

Na mwanamke aliyefikisha vigezo 98%, hata mkishindwana mkaamua kuachana, hamtaachana kishamba kama kicheche ambaye hajafikisha hata 10% ya vigezo.

Point yangu si total control, that is against the laws of physics.

Point yangu ni risk minimization, kwenye levels mbili. Kwanza kupunguza saana saana uwezekano wa kuwa na mwanamke mnayeweza kuachana kirahisi, na pili, hata ikitokea hiyo 2% uliyobakisha ikawa mtu kabadilika, mkaachana, mnaachana vizuri kila mtu anaendelea na maisha yake.

Moja ya tatizo kubwa linalofanya hoja yangu kuwa ngumu ni utamaduni wa "all or nothing at all".

Yani ni kama tunaona mwanamme au hata mwanamke, kuwa kamili, kuwa ana sifa, ni kutoachana na mwanamke/mwanamme wake.

Suala la talaka, suala la kuachana, linaonekana kama kushindwa, kama upungufu. Na kuna masuala ya utamaduni na dini, yasiyo mazuri, yanachangia sana kwenye attitude hii.

Unaambiwa kwamba Mungu anachukia talaka. Unalazimishwa kwa pressure ya dini kukaa na mtu ambaye unaona kabisa hamuendani.

Wakati kuna sehemu kuachana ndiyo akili yenyewe. Mkikaa pamoja mnaweza kuongezeana matatizo mpaka mkauana.
 
Hapa umeeleweka vizuri Mkuu.
 

Tunarudi palepale.

Yaani mwanaume na akili yake aache mambo ya msingi ahofie usaliti?
Usaliti ni jambo linalotarajiwa katika mamlaka na tawala yoyote duniani. Hilo ni jambo tarajiwa.

Huwezi kukaa kuwaza kusalitiwa.

Hofu za wanaume wala hazipo kwenye usaliti.
Mada inazungumzia hofu ya mwanaume katika vipengele ya afya, maumbile yake, na mambo ya kiuchumi. Ambayo kimsingi tunazungumzia heshima ya mwanaume.

Usaliti hauangalii kama unayote hayo.

Kama Mungu muweza wa yote alisalitiwa, aliasiwa sembuse mwanadamu?

Tofautisha changamoto zinazoathiri heshima ya uanaume ambazo ndio hofu ya wanaume na masuala ya usaliti
 
Hivi kuna kitu kinachomvua mwanaume heshima na utu wake kijamii kama kugundua analea watoto wa mtu mwingine?

Wewe unaishi dunia ya kufikirika naona.
 
Hivi kuna kitu kinachomvua mwanaume heshima na utu wake kijamii kama kugundua analea watoto wa mtu mwingine?

Wewe unaishi dunia ya kufikirika naona.

Kati ya msaliti na msalitiwa yupi anavunja heshima?

Kulea mtoto asiyewako nako tunarudi palepale ni ukosefu wa akili.
Mwanaume mwenye akili timamu hawezi kubambikiwa watoto.

Hivi wewe unaitafsiri vipi Akili?
Unapoambia Akili timamu unafikiria kwa mtazamo upi?

Mwanamke akichepuka anachepuka kwa utashi na hiyari yake. Wewe unavunjiwaje heshima kwa mwanamke wako kuchepuka? Embu nipe hoja zako.

Mkeo kumuoa haimaanishi hana hiyari ya kutumia mwili wake atakavyo. Anaweza kutumia vibaya au vizuri.

Akitumia vizuri ni heshima kwake. Akitumia vibaya halikadhalika
 
Unaishi sayari gani wewe? Kwenye jamii yetu ya Kiafrika, mkeo akichepuka na kila mtu mtaani akajua, hakuna atakayesema yule mwanamke hana akili, jamii itamnyooshea kidole mume kwamba yule mwanaume ameshindwa kulea na kuisimamia nyumba yake.

Usaliti wa mwanamke huwa unavunja heshima ya mwanaume kwa 100% kijamii, you cannot separate a man’s respect from his wife’s behavior katika uhalisia wa maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…