Kiingereza cha Rais Samia

Nina wasiwasi kuwa sababu ya Dr. Magufuli kutokwenda nje ya Africa ni kuongea kiingereza. Kwani si kuna option ya kuzungumza kiswahili akatafsiriwa?

Lakini kuna zile gadgets wanatumia kwenye mikutano ya kimataifa zinazotafsiri lugha mbalimbali.

Angeweza kutumia kimojawapo. Tena kwa uhalali wa kukitangaza kiswahili duniani na angeeleweka tu. Mbona Xi Jingpin anaongea Kichina anatafsiriwa na mkalimani na haina shida?

Kuna zaidi ya hapo.
 
Sukuma gang tupumzisheni walau kidogo jamani!!!
Hili jitu linafananisha kiingereza Cha Magu na Samia, hahaha, Magu hovyo kabisa, sukuma gang wakagawane nguo za marehemu
 
Sukuma gang bado wanaweweseka , tuwaache wakamalizie msiba na kupalilia kaburi
 
Kile kidude kwenye moyo
 
Halafu hivi ni mimi tu [maana nisije kuwa na nitpick] au mbele/ pembeni ya Kamala, Hangaya kaonekana kama hana gravitas?
Wewe ulikuwa husikilizi message ulikuwa unavizia wapi atakosea kiingereza, mie nimemsikiliza na nimemwelewa, halafu ujue siyo native speaker wa hiyo lugha.

kweli kuna makosa ya knowledge kayafanya hasa la the first woman participation.
 
Toa upuuzi wako hapa,kwani yeye ni Muingereza au Mmarekani? Mbona anaongea vizuri tu? Hii ndio shida kuu ya wabongo kama wewe. Unataka aongee kama wenye lugha halafu iweje? Au kwa kuwa umeishi Marekani hivyo unataka kila mtu aongee kama wao?
 
Kama angekuwa wa awamu tofauti tungesema pengine ana haki ya kurekebisha yaliyokosewa...Sasa huyu na kampeni alifanya na mwenzake kama ishara ya maono ya pamoja anapokuja kuyageuka mwenzake anapokosa power hiyo si sawa, ni indicator ya kukosa integrity na uaminifu ambayo sidhani kama yeye yupo hivyo
 
Hivi lugha ya Kiingereza ina uzito gani katika vigezo vya kuwa Rais wa Tanzania? Jee, hiki ni kitu kweli cha kutupotezea usingizi : eti Magufuli na Samia wanapishana kwenye lafudhi tu lakini wote hawakimudu Kimombo! Afadhali lugha inayozungumziwa ingekuwa Kiswahili, kwani Rais inabidi awe mfano kwenye lugha ya Taifa. Mtanzania una mengi ya kuwazia kuhusu kujikwamua kwenye changamoto za kiuchumi na kijamii, zaidi ya kujadili Kiingereza cha Rais wako. Hoja hii haina tija kwenye maslahi ya Mtanzania. Kama mmoja wao anakimanya kimombo zaidi ya mwenzie, so what?
 
Sifa zile za Dr Jiwe yaani hicho kitu hakutaka kabisa, hakutaka hata kidogo kudhalilisha nafsi yake. na kwa kufanya hivyo pia watu ambao walikuwa wanahoji elimu yake wangeendelea mkunyanyasa kupitia udhaifu wa kuto jua kuongea kiingereza.

Nb. Pamoja na yote yatupasa tujue kwamba kuongea kiingereza sio ishara kuwa upo juu kielimu.
 
Inakwenda kusikojulikana..
Hapana. The state is finally back from ruthless hijackers and mercenaries.
Ilipo sasa hivi kama wananchi tunaweza kupaza sauti na tukasikilizwa si kuuliwa.

Tusiruhusu ipitilize kusikojulikana!!
 
Sasa utamfananisha na jiwe?si afadhali yeye kuliko jiwe aliyekua anajifungia chumbani anaogopa kusafiri
 
Nb. Pamoja na yote yatupasa tujue kwamba kuongea kiingereza sio ishara kuwa upo juu kielimu.
Nadhani iangalie kwenye taswira hizi:
1. Elimu inayoeleweka bila ufaulu wa kukariri.
2. Uwezo binafsi wa mtu kujenga hoja na kujieleza!
3. Maandalizi (mazoezi) binafsi

NB: Huko tuliko tujiandae kikamilifu ku encounter international situations. Dunia ni kijiji. Wengi wanaomsema SSH wanapata shida hizo hizo hata wakikutana na Wachina, Indians, Russians ambao si native English speakers.
 
Akisoma anakuwa fluent kidogo, kuwa mtu wa pwani kunamfanya aweze kusoma vizuri.

Yale ya kutoa kichwani ni mweupe pe! Kama mimi tu😋
Tatizo ni maandalizi... Na kukosa mtiririko wa hoja!
Na mtu akiwa hivyo haijalishi anatumia lugha gani!
 
Acha visingizio vya kijinga, kiingereza ni lugha rasmi ya taifa kama kilivyo kiswahili, kiingereza hakitumiki serikalini kwa hiari bali kinatumika kisheria, maneno ya wanasiasa weka pembeni.
 
naona anasoma wala hatowi kichwani.Kwa maelezo yako yanamhusu pia muandaaji.
 
Meko hata kiswahili tu aliondoka kinampiga chenga:

MBWA anaita UMBWA
 
Ni kweli kabisa mkuu, lakini hapa nilikuwa najaribu kuongea ili watu wafahamu kwamba unaweza kuongea sana kiingereza, kiarab au hata kichina na kifaransa sio kwababu umesoma sana, isipokuwa isipokuwa umekaa sana nchi ambazo wanaongea sana hizo lugha.

Nina mfano, Kuna rafiki yangu mmoja sikuwa juwa kuwa yupo vizuri kiasi kile katika uongeaji wa kiingereza, na ni kwa vile hakuwa muongeaji wa kiingereza bila sababu kama kaka na dada zangu wa kihaya..

Sasa Kuna siku tukuwa na orally interview jamaa alitelemsha ngeli ya hatari bahati nzuri interview hiyo ilikuwa adharani, wote tuliokuwa tunashiriki tulikuwepo yaani mwenzako anahojiwa unaona na unasikia.

Baada ya hapo tukamuuliza ndugu yetu hii kitu umeingia nayo kutoka wapi!!? (Jamaa ni muislam) watania wakasema dua hizo huyo ni shehe. Ila uhalisia jamaa alikaa Zambia Lusaka, baba yake akiwa anafanya kazi TAZARA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…