Jussep
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 330
- 368
Nina wasiwasi kuwa sababu ya Dr. Magufuli kutokwenda nje ya Africa ni kuongea kiingereza. Kwani si kuna option ya kuzungumza kiswahili akatafsiriwa?Nimemsikiliza Hangaya, ana uwafadhali sana tena sana ukimlinga na Dr Jiwe, Dr Jiwe anaachwa mbali sana na Hangaya kwenye hii lugha.
Kama kuna mtu yeyote anabisha haya nisemayo aje kuthibitisha kwa ushaidi wa klip yake yoyote akiongea kiingereza Dr Jiwe.
Kuhusu kukosea juu ya kusema kuwa Kamala ndio mwanamke wa kwanza kugombea nafasi ya umakamu urahisi Marekani, kama mnakunbuka jiwe alisema kuwa Saddam Hussein Kuwait kipindi cha kampeni za 2015. mbele ya watanzania wenzake akiwa anaongea kiswahili kabisa.
Dr. Jiwe hakika aliufahamu udhaifu wake ndio maana hakutaka kutoka nje ya nchi hasa nchi za Ulaya na America, alifahamu atashikwa kigugumizi tu, badala yake akawa anawapekeka mama Samia na Majaliwa.
Nb. Anaepinga kuwa Dr. Jiwe hakujua kuongea lugha ya kiingereza aweke klip yake hapa.
Lakini kuna zile gadgets wanatumia kwenye mikutano ya kimataifa zinazotafsiri lugha mbalimbali.
Angeweza kutumia kimojawapo. Tena kwa uhalali wa kukitangaza kiswahili duniani na angeeleweka tu. Mbona Xi Jingpin anaongea Kichina anatafsiriwa na mkalimani na haina shida?
Kuna zaidi ya hapo.