Kiingereza cha Rais Samia

Kiingereza cha Rais Samia

Ni vigumu sana kuwa fluent kwenye lugha ambayo huitumii kwenye mawasiliano yako ya kila siku, inakuwa ngumu sana kujenga misamiati ya kutosha ikiwa hiyo lugha huitumii...........na bila misamiati au maneno ya kutosha utaanza kutafutatafuta maneno sahihi na mwishowe unaishia kupata kigugumizi na kupoteza confidence......
 
Ni vigumu sana kuwa fluent kwenye lugha ambayo huitumii kwenye mawasiliano yako ya kila siku, inakuwa ngumu sana kujenga misamiati ya kutosha ikiwa hiyo lugha huitumii...........na bila misamiati au maneno ya kutosha utaanza kutafutatafuta maneno sahihi na mwishowe unaishia kupata kigugumizi na kupoteza confidence......
Mleta uzi yeye yuko fluently kwenye kutema yai mkuu

Ova
 
Mh samia kwanza amejitahidi sana licha ya kukosea hizo fact za kwambaHarris ni mgombea wa kwanza kugombea umakamu wa rais wakati walikuwepo akina Hilary Clinton walipambana na akina Trump kuutaka urais wa marekani .Hiyo lugha siyo tu ni our second language wengine ni third au fourth kwani kuna lugha mama kiswahili then hicho kiingereza ambacho kilikuwa kimemshinda mazima bwana yule mpaka akaanzisha operation ya kukidisvalue kionekane ni nonsense language
 
Nchi ambayo viongozi wanakimbia midahalo kipindi cha chaguzi haya ndio matokeo yake.

Mtangulizi wake kwenye midahalo ndio alikua hataki hata kusikia japo ni ya kiswahili.
 
Nchi ambayo viongozi wanakimbia midahalo kipindi cha chaguzi haya ndio matokeo yake.

Mtangulizi wake kwenye midahalo ndio alikua hataki hata kusikia japo ni ya kiswahili.
Pata picha Hangaya yuko kwenye mdahalo wa Kiingereza na Lissu 🤣.

It won’t be fair at all.
 
Hii sasa ni point. Midahalo inahitajika sana ili wananchi tuweze kuwapima wagombea. Na CCM wanaigopa sana. Tena tunaongelea ya Kiswahili, siyo ya Kiingereza.
Nchi ambayo viongozi wanakimbia midahalo kipindi cha chaguzi haya ndio matokeo yake.

Mtangulizi wake kwenye midahalo ndio alikua hataki hata kusikia japo ni ya kiswahili.
 
Ukae kitako kwa kutulia, zama zenu Sukuma gang zimekwisha.

Mama atakaa madarakani mpaka 2030 mtake msitake.
Mada ni lugha kwa viongozi wetu, wewe na sukuma gang, zama zao...
 
Rais ana shida sana yakutikuwa mfatiliaji wa mambo muhimu !
Rais pia ana shida ya wasaidizi maana wanamuandikia vitu vya kumuabisha kabisa!

Yani kila akiongea au kusoma vitu lazima atakwenda chaka....sijui shida ni nini?
 
Akiwa anasoma, kuna afadhali kidogo.

Lakini akiwa anaongea kutoka kichwani ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa], anapata shida sana.

Yaani Magu na Hangaya walichaguana wote wakiwa weupe kwenye hiyo lugha pendwa.

Muangalie na msikilize kwenye video hapo chini. Yale ambayo hayajaandikwa [hajaandikiwa] kwenye karatasi, anapata shida kuyaongea.

Anajiuma uma tu. Hajiamini. Mpaka hata taarifa za ukweli [facts] anazikosea.

Uchaguzi mkuu wa Marekani wa 2020 haukuwa uchaguzi wa kwanza wa nchi hiyo kuwa na mwanamke kama mgombea umakamu wa Rais.

Wakati Geraldine Ferraro anagombea kwenye tiketi moja na Walter Mondale, Hangaya alikuwa wapi?

Wakati Sarah Palin anagombea na John McCain, Hangaya alikuwa wapi?

Au alitaka kusema kuwa 2020 ndo mara ya kwanza kwa mwanamke kuwa katika tiketi iliyoshinda uchaguzi lakini akajiuma uma na akakosea hizo basic facts?

Halafu, ni ‘the United States and Tanzania have enjoyed excellent relations [siyo relation], for the last [past sounds much better] 60 years’.

Halafu kuna watu wanadai eti Hangaya yuko vizuri kwenye Kiingereza 🤣. Ama kweli hii lugha ni janga la kitaifa.

Maana mtu yeyote aijuaye vizuri hiyo lugha hawezi kusema eti Hangaya yuko vizuri.

Hangaya na Magu labda wanapishana kwenye lafudhi tu. Magu alikuwa na lafudhi nzito/ nene zaidi. Hangaya ya kwake si nzito kivile, hivyo kuonekana kama vile anaimudu, kumbe wapi!

Kwenye sintaksia, semantiki, sarufi, kunyambua vitenzi, n.k., hawapishani sana. Wote mulemule tu.


Jamani pongezeni kuwa Tanzania kidogo kidogo inarudi duniani kutoka kusikojulikana...
Hayo mengine ni madhaifu ya mtu! Hayarekebishiki kirahisi rahisi... Bora yeye kajikubali anakanyagamo humo humo!

Not everybody is a public speaker!

Shida inayoina kwa SSH ni kukosa muda wa kujiandaa... Kushindwa kujiamini... Uchaguzi mbaya wa maneno (diction)... Kukosa utulivu wa akili!


#Mungu Ibariki Tanzania...
 
Hapana.

Fluency haihusiani na kusoma vilivyoandikwa.

Ni kwamba hana lafudhi nzito/ nene. Hicho ndicho kinachomfanya aonekane ana afadhali.

Lakini maneno mengi sana yanampa shida kuyatamka.

Hata yale maneno ya kawaida ya hiyo lugha hawezi kuyatamka vizuri.

Ukimwandikia neno kama ‘xylophone’ au ‘discombobulation’, anaweza kupoteza fahamu akijaribu kuyatamka.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Nacheka sio kama najua sema basi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom