CCM bhana.
Zanzibar hakuna tatizo ulilolieleza kweye mada yako.
Hii ni propaganda ya CCM ili iendelee na mchezo mchafu; kubaka demokrasia na kung'ang'ania madaraka.
Kama utakuwa mkweli na si mnafiki, tatizo la Zanzibar ni CCM kutoheshimu maamuzi ya wapiga kura na propaganda chafu ya sultani atarudi ikiwa CUF itachukua madaraka.
Tatizo jengine ambalo Nyani Ngabu ameliona hapa Tanzania ni upoyoyo wa wananchi. CCM na serikali zake wanatumia upoyoyo huo wa wananchi na vyombo vya dola kung'angania madaraka.
Kwa kweli hakukua na sababu ya kuwepo mkwamo Zanzibar kwa sababu umeshataja hapo kuwa Zanzibar ni lazima waunde serikali ya umoja wa kitaifa. Ni takwa la kikatiba.
CCM waache kung'ang'ania madaraka, ZEC inajua ni nani ameshinda, watangaze matokeo yaliyobakia na mshindi aapishwe aunde serikali na shughuli za maisha ziendelee.
Tume ZEC ikimalizia kutangaza matokeo ya majimbo yaliyobakia au isitangaze. Matokeo yanajulikana tayari kwa sababu yalishatangazwa majimboni na kubandikwa ukutani na wasimamizi wa majimbo.
CCM ndio watavuruga amani ya nchi hii.
Magufuli angekuwa mnufaika mkubwa wa siasa kwa kipindi hiki kama Zanzibar ikiongozwa na Chama cha upinzani. Tawala zote zitataka kujikita katika mikakati kuleta maendeleo na kukuza uchumi. Mashindano ya kiuchumi na kuinua hali za maisha ya walalahoi.
Acha propanganda chafu na za kijinga, ambia Chama chako kiachane na ulafi na ung'ang'anizi wa madaraka au kifute mfumo wa vyama vingi kama haina nia ya kuachia madaraka inaposhindwa kupitia kisanduku cha kura.
Wewe huna tofauti na Lukuvi.