Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Neno kiinua mgongo sijui lina maana gani kwa wanasiasa? maana mtumishi anastaafu utumishi wake na kupewa pesa za mafao halafu anarudia kazi hiyo hiyo mwaka huo huo na kuanza kupata mishahara na posho kama mwanzo huku akisubili mafao yake tena baada ya kustaafu kwa mara ya pili kabla ya kurudi kwa mara ya tatu kwenye utumishi wake!!! sijui nchi za wenzetu ziko kama ilivyo Tanzania?
Yaani pamoja na wabunge wa Sisiemu kufanya kazi ya 'kutukuka' kwa kupitisha kwa asilimia 100 muswada ulioletwa kwa hati ya dharura wa gesi na mafuta, bado serikali imeamua kuwapiga 'teke' katika kutekeleza kwa vitendo kile kitu kinachoitwa shukurani ya punda ni mateke katika yale mafao yao, ambapo kila Mheshimiwa Mbunge alitarajia 'kulamba' shilingi milioni 230?
Ndipo hapo wabunge wa CCM wajifunze na koona faida ya kuusaliti Umma wa watanzania na kuwakumbatia wawekezaji wa nchi za nje pamoja na 'wapambe' wao hapa nchini, ambao ni watawala.
Hili sijui tuliite bao la mkono pia?kama ni kweli kwa hili moja nitamsifia baba riz one milele
Bado haijala kwao, kazi ya miaka 5, mshahara mnono, posho nono, viti maalum vinono, halafu unalipwa mil 130 unaona wameliwa? Hizo bado ni nyingi sana.ndiyo hivyo. Imekula kwao hiyo...
Jamani wabunge wa sisiemu, kichwani mwao nadhani kuna upepo!
Halafu kuna dogo alikuwa anazunguka na chopa hadi wakaparamia miti. Sijui atalipaje?Kwa wananchi kicheko....kwa wanaomalizia ungwe ya kuitwa waheshimiwa kilio...hapo prezida kacheza kama pere....
CAG kasema 130m ndo ipo kisheria, zile nyingine zilikuwa za rushwa ili wapitishe muswada wa gesi na mafuta. Nasikia kafulila alizinyaka nyepesi nyepesi akaahidi kuipeleka serikali mahakamani ili apate kick toka mashirika ya kimataifa. Jamaa kashtuka.Hawana ubavu Wa kuwanyima posho iko kisheria wataitolea mahakamani
Duuh hii habari ni pigo kwa wabunge wa CCM.
Huyu hana shida na hako kakiinua mkia, shida ilikuwa mafuta na gesi baasi!Ivi mbunge wa chalinze nae atapewa hicho kiinua mgongo.
Mkuu si kuna kulipia?Ahahaha,isingekuwa mfungo ningepiga bia tatu chap chao
Usiombe hata kupumzishwa tuu kule segerea. Kuna nyakati ngumu hebu fikiria wakati unakunya kwenye debe halafu yona anamwangalia. hakuna toilet paper, halafu ukamwage! Usafishe ndoo> Ni balaa.Mramba huko segerea inawezekana kapumzishwa tu