Kiinua mgongo cha Wabunge chashushwa toka Milioni 238 kuwa Milioni 130!

Kiinua mgongo cha Wabunge chashushwa toka Milioni 238 kuwa Milioni 130!

Ss Zzk atapeleka nn kule kwny vituo vya watoto yatima?!
 
Hatari kashafulia tayari na alichokua anakitarajia ni hayo mafao alipopata hzo tarifa alipanic mpaka akaomba mwongozo.

haa haa haa angejua kabla asingechezea hela kwenda kuchukua fomu ya milioni na kugawa pesa kwa wadhamin haa haa haa kesho wakimsusia rais nitawapa 5
 
ni mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali hivyo hapo yupo kazin kuzuia matumiz mabaya ya serikali
Anahusika kweli kwenye mchakato wa malipo? Au Rais aliomba ushauri kwake baada ya kelele za wanaharakati na wananchi? Kikawaida nafikiri mchakato unahusisha uongozi wa bunge na rais...Hata hivyo ni faraja, maana wafanyakazi wa umma wanasotea pensheni hiyo kwa miaka zaidi ya 35 kukaribia pendekezo hilo la milioni 235.
 
Kama mnavyoelewa, Serikali kupitia kwa CAG imekataa wabunge wasilipwe milioni 238 na badala yake kwa mujibu wa sheria amesema walipwe takribani milioni 130.

Wabunge wa CCM waliobaki bungeni baada ya kupata taarifa hiyo wamekubaliana kutopitisha muswada wa kuanzisha tume ya walimu jioni hii. Mbaya zaidi wamepanga kugomea hotuba ya rais kesho iwapo hawatalipwa milioni 238.

Nawapa pole waemingizwa mkenge wakapitisha miswada ya gesi yenye kumnufaisha baba riz na watu wake wakiahidiwa kulipwa milioni 238 na badala yake fedha imepunguzwa.

Nilitaka kushangaa, katika nchi ambayo wastaafu wameongezewa pensieni kutoka 50,000/- hadi 100,000/- kwa mwezi, walimu wanamadai lukuki ambayo hayalipiki, wazee wanakosaa madawa hospitalini, leo wabunge ambao wanapata mishahara minono ya zaidi ya 3,000,000/- kwa mwezi na posho ya karibu 300,000/- kwa siku. Wakati mzee aliyestaafu baaada ya kulitumikia taifa hili kwa zaidi ya miaka 30 kiinua mgongo chake ni kati ya 10,000,000/- na milioni 50,000,000/- lakini mbunge aliyetumikia bunge kwa miaka 5 tu kiinua mgongo chake ati ni 230,000,000/-. This is not fair, this country belongs to each and everyone of us. Namshukuru CAG kwa kuliona hilo. Ati wapate kiinua mgongo kikubwa kwa ajili ya kulipa madeni kana kwamba walitukopea sisi, no, watumishi wakikopa na kushindwa kulipa wanafilisiwa nyumba zao wao ni nani wasifilisiwe kulingna na mikataba ya mikopo yao?
 
Wanajifanyaga akili zao ndogo hawawezi kufikir wakati mijitu ni miprofesa na midaktar
 
CCM wamezoea wakumbuke kuwa watanzania wanahali ngumu laiti kama watanzania wote wangekuwa na uwezo wa kujuwa wabunge wa ccm wanachogombania kuwa ni 238milions wangeandamana , wangejuta kuchagua mafisadi kama hao.
UKAWA KAZENI BUTI maisha yabadilike watanzania tuache kuzeeka na miaka 40 maana kwetu mwenye baiskeli ni tajiri wengine ni full yeboyebo jamani ccm tugawane sawa rasilmal za nchi tanzania ni yetu sote
uroho ccm muache hivi watanzania mnatuchukuliaje? kama .......











l
 
Ni kubwa mno na hawaistahili kabisa.

Hao sana sana wanayostahili labda ni milioni 10 ingawa hata hizi bado ni nyingi vilevile.

Neno kiinua mgongo sijui lina maana gani kwa wanasiasa? maana mtumishi anastaafu utumishi wake na kupewa pesa za mafao halafu anarudia kazi hiyo hiyo mwaka huo huo na kuanza kupata mishahara na posho kama mwanzo huku akisubili mafao yake tena baada ya kustaafu kwa mara ya pili kabla ya kurudi kwa mara ya tatu kwenye utumishi wake!!! sijui nchi za wenzetu ziko kama ilivyo Tanzania?
 
Anahusika kweli kwenye mchakato wa malipo? Au Rais aliomba ushauri kwake baada ya kelele za wanaharakati na wananchi? Kikawaida nafikiri mchakato unahusisha uongozi wa bunge na rais...Hata hivyo ni faraja, maana wafanyakazi wa umma wanasotea pensheni hiyo kwa miaka zaidi ya 35 kukaribia pendekezo hilo la milioni 235.

kwa upande wa Cag ni swala la ushauri tu ila sidhan kama una nguvu ya moja kwa moja ktk malipo hayo labda tu kama serikali imeupokea ushauri huo na kuufanyia kazi
 
Wabunge wa UKAWA wawe makini sana katika kipindi hiki...unaweza kukuta hili ni changa la macho tu ili ionekane wabunge wote wamekosa hiyo hela kumbe sivyo!
 
Leo nimekumbana na kali ya mwaka, eti wabunge wa CCM wameramba shilingi za kitanzania milioni 800 ili waipitishe miswada mitatu tata, ikiwemo ya gesi na mafuta na uwazi.

Habari hizo za kijiweni zimezidi kudokeza kwamba kwa hali yoyote ile miswada mitatu ilikuwa LAZIMA ijadiliwe na IPITISHWE hata kwa bao la mkono.

Mzushi huyo akasonga mbele kwa kusema hata spika wa bunge angetukanwa ama angelazwa juu ya vitabu vya kanuni za bunge za uwasilishaji miswada; na huku akisomewa kanuni hizo na UKAWA mbele ya hornspeaker nne kumwelekea spika huyo wa bunge; bado asingezielewa kanuni zilizoandikwa na kusomwa mbele yake.

Hata kama kanuni hizo zingemfufua Nyerere bado asingezielewa tu. Hii ndiyo habari ieneayo chini kwa chini.

LISEMWALO eti lipo. Muh! Ni ngumu kumeza lakini!
 
Kama wamelamba pesa zote za umma unashangaa na hilo mkuu.


swissme
 
Napendekeza wabunge wanaomaliza muda wao walipwe mafao yao mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

Hii ni kutokana na kuepuka matumizi ya pesa katika kuwalaghai wananchi na kuweka usawa wa kiushindani kati ya wagombea na wagombea.

Pia kuwasaidia wabunge wasioweza kurudi, badala ya kuziteketeza kwenye kuhonnga wapiga kura, baada ya uchaguzi waziwekeze na kutoa ajira kwa watanzania na kukuza uzalishaji.

Ni wazo langu tu.

zuri sana na lina mantiki sana
 
Hata Kafulila alitukanwa ndani ya Bunge na kutishiwa kupigwa na yule Tumbili mwizi mara baada ya kutujuza Watanzania kashfa nzito ya Escrow na kuitwa mzushi mkubwa, lakini penye ukweli uongo hujitenga. Sasa ukweli kuhusu escrow tunaujua.
 
Leo nimekumbana na kali ya mwaka, eti wabunge wa CCM wameramba shilingi za kitanzania milioni 800 ili waipitishe miswada mitatu tata, ikiwemo ya gesi na mafuta na uwazi. Habari hizo za kijiweni zimezidi kudokeza kwamba kwa hali yoyote ile miswada mitatu ilikuwa LAZIMA ijadiliwe na IPITISHWE hata kwa bao la mkono. Mzushi huyo akasonga mbele kwa kusema hata spika wa bunge angetukanwa ama angelazwa juu ya vitabu vya kanuni za bunge za uwasilishaji miswada; na huku akisomewa kanuni hizo na UKAWA mbele ya hornspeaker nne kumwelekea spika huyo wa bunge; bado asingezielewa kanuni zilizoandikwa na kusomwa mbele yake. Hata kama kanuni hizo zingemfufua Nyerere bado asingezielewa tu. Hii ndiyo habari ieneayo chini kwa chini. LISEMWALO eti lipo. Muh! Ni ngumu kumeza lakini!

Mkuuu husicheze na mwenye nguvu
 
Hata Kafulila alitukanwa ndani ya Bunge na kutishiwa kupigwa na yule Tumbili mwizi mara baada ya kutujuza Watanzania kashfa nzito ya Escrow na kuitwa mzushi mkubwa, lakini penye ukweli uongo hujitenga. Sasa ukweli kuhusu escrow tunaujua.

Na mtukanaji yuko nje anasikiliza bungehilo kupitia tbccm wakati tumbiri yupo mjengoni
 
Back
Top Bottom