Kiinua mgongo cha Wabunge chashushwa toka Milioni 238 kuwa Milioni 130!

Kiinua mgongo cha Wabunge chashushwa toka Milioni 238 kuwa Milioni 130!

Jamani, ilishasemwa huwezi kula tu bila kuliwa kidogo, nipe nikupe ndio mwendo siku hizi. Kulalamika kwao kwa hicho kiinua mgongo cha 238M ni sawa sababu kuna makubaliano ambayo yapo and walikubaliana kuwa kitabaki hivyohivyo, so kugomea bunge kwao ni poa tuuuu..... wameliwa hao hawajala...
 
Nani anajua kanuni ya kukokotoa mafao ya wabunge? Kwa nini kuwe na kutofautiana mara 238 mara 130 CAG kapendekeza. Yaani mtu mmoja tua anamua wapewe kiasi gani bila mwongozo wowote?
Wewe unawajua watawala wetu?

Hizo kanuni na taratibu zilizomo kwenye makaratasi huwa siyo kazi ngumu sana kutenguliwa, iwapo tu watawala wetu wa CCM wataona zinawatilia kiwingu.

Unakumbuka wakati wa Bunge Maalum la Katiba chini ya uongozi wa Spika Samuel Sitta, walipoweza kutengua kanuni ya 2/3 ya kuipitisha Katiba pendekezwa, ambapo walitengua kanuni inayotaka 2/3 ya wabunge waliomo ndani ya Jengo la Bunge na wakaruhusu zipigwe kura hata kwa 'SMS' kutoka kwa mahujaji waliokwenda kuhiji Macca na wagonjwa waliolazwa hospitali ya Apollo kule India?

Kwa hiyo chini ya utawala wa CCM, kinachozingatiwa siyo kanuni, taratibu na sheria za nchi, bali kinachoangaliwa zaidi ni kanuni hiyo inamhusu nani, ndiyo maana haiwezi kuwa jambo la kushangaza sana kuona Mwalimu aliyelitumikia Taifa hili kwa uaminifu mkubwa baada ya utumishi wake wa miaka 40 kazini akiambulia mafao ya kustaafu yasiyozidi shilingi milioni 30 wakati waheshimiwa wabunge wetu kwa kipindi cha miaka 5 pekee wakitaka kujilipa shilingi milioni 230!
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Wanawake wa Tanzania wanaweza kuongoza Taasisi lenye changamoto nyingi kama Bunge ... No wonder watu wa Ulaya wanatulazimisha kuwa na viongozi wanawake ... Grrrrrrrrrrrrrr
 
Back
Top Bottom