mwakani naolewa
Senior Member
- Jul 25, 2024
- 148
- 426
Dar es salaam, leo 26 July kuna kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 16 hadi 17 (jina linahifadhiwa) maeneo ya Ubungo Msewe amepatikana nje ya nyumba akiwa amejilaza huku akivuja damu nyingi sana maeneo yake ya siri yaani sehemu ya haja kubwa chanzo kikidaiwa ni kulawitiwa na wanaume wenzake kisha kuchomwa kisu na kutelekezwa barabarani.
Bibi Asha ambae ni mkazi wa eneo hilo ameeleza kuwa alishtushwa na kelele usiku wa saa 8 za kijana huyo akiomba msaada kuwa wamsaidie maana anakufa, ameeleza kuwa hiyo ni tabia ya kijana huyo akishalewa hupiga kelele ila jana ilikuwa tofauti.
Waziri Dkt. Gwajima D tafadhali fuatilia suala hili, tunaweza kumpoteza kijana huyu.
Hizi ni baadhi ya picha za kijana huyo akiwa mahututi lakini hakuna polisi aliyejitokeza hata baada ya kupigiwa simu.