Twilumba
JF-Expert Member
- Dec 5, 2010
- 12,576
- 14,522
Kama ni vibaya halali yao!!!.Hata kama ni vibaka kwanini wasiwakamate na kuwapeleka Polisi?
Siku ukikutana na hao vibaka utaomba wapotezwe wote!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ni vibaya halali yao!!!.Hata kama ni vibaka kwanini wasiwakamate na kuwapeleka Polisi?
Mamaye hakumfunza sasa anafunzwa na ulimwengu!!Pole kwa kuondokewa na huyo kijana ambaye naona kabisa ni mtu wako wakaribu
Sheria ipi inaruhusu kuchukua Mali ya mwenzio kwa nguvu.Suchak ongea kwa hoja...sheria ipi inaruhusu sungu sungu waue?
Baada ya kuuawa Jongo utafuata wewe......
Kajifunze kulea Kwanza ndo ulete vifungu vyakoKwa akili zenu duni mnaowatetea hawa wapuuzi sungu sungu vyombo vya sheria tuvifute?
Tuwaache sungu sungu wakichukua sheria mkononi?
Kwa hiyo hata mafisadi,wauza madawa ya kulevya, majambazi,wahujumu uchumi tuwaachie sungu sungu wawaue?
Acheni ujinga na upumbavu...kwa sababu yoyote sungu sungu hawapaswi kuwa juu ya sheria.
Wizi na ukabaji unaendana na mauaji au kutishia mauaji.ILA KUUA SIO JAMBO JEMA.kosa la wizi na adhabu ya kifo wala haviendani.
Kibaka akikamatwa kwenye tukio malizaneni nae hapo hapo nasema mpelekeni kwa mola wake akatubu hakuna kulea kibaka sijui mwizi ukimkamata hakikisha hatokaa apate nafasi ya kumwibia mwingine tenaMheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, sisi wanawake tuna imani sana na wewe, tutakupa kura zetu zote za urais mwaka 2025 ila kuna mambo machafu sana yanayofanyika katika serikali yako.
Sisi wanawake wa Tanzania tumesikitishwa sana na mauaji ya kijana mdogo mkazi wa kata ya Mabibo kitongoji cha Soweto yaliyofanywa na watu wanaojiita Sungu sungu.
Kijana huyo anaitwa Jumanne Jongo. Ameuawa kikatili sana kwa kukatwa miguu na mikono.
Cha ajabu wauaji wa kijana huyu wanajulikana na hawajakamatwa hata mmoja.Taarifa nilizokuwa nazo bado wameahidi kuua vijana wengine wanaowahisi vibaka.
Genge hili la mauaji ya vijana linaongozwa na watu wanaojiita Sungu sungu kutoka kata ya Jitegemee ,Mabibo wilaya ya Ubungo.
Haya sio mauaji ya mara ya kwanza, huko nyuma sungu sungu hao wa Jitegemee wameshawahi kuua vijana wengi kwa kisingizio kuwa vijana hao ni vibaka.Hata kama ni vibaka kwanini wasiwakamate na kuwapeleka Polisi?
Kwanini sungu sungu wanajichukulia sheria mkononi?
Mh.Rais nchi yako ni nchi inayofata utawala wa sheria, iweje wapumbavu wachache watie doa uongozi wako?
Taarifa nilizokuwa nazo mauaji hayo yanapata baraka kutoka katika uongozi wa serikali ya mtaa wa Jitegemee chini ya mwenyekiti Kilema.
Hivi OCD wa Kinondoni hana taarifa ya tukio hili? Mpaka sasa hivi amechukua hatua gani? Anapata kigugumizi kipi cha kuwakamata wauaji hao wakiongozwa na mpumbavu mmoja anayeitwa Samwel?
Kwa taarifa yako mh.Rais sisi wanawake wa Mburahati na Jitegemee tumeguswa sana na kifo cha huyu kijana, tunatafakari mara mbili mbili kuwa wanachama wa CCM.
Embu ukiwa kama Rais tumia mamlaka yako kushughulikia suala hili.Maana sisi wanawake wenzako tuna wasiwasi sana kuhusu maisha ya watoto wetu wanaouawa kila kukicha na hawa watu walio juu ya sheria wanaojiita Sungu sungu.
Kuna hoja kwamba huyu kijana alikuwa kibaka,lakini sheria inasemaje? Kwani hukumu ya kibaka mauaji?
Chonde chonde mh.Rais fanyia kazi suala hili ikibidi mwajibishe kamanda wa Polisi wa Kinondoni kwa kushindwa kuwakamata hao wauaji wa huyu kijana.
Kuua sio poa, ila wananchi nao wamechoshwa na usumbufu wa hawa vibaka na kila wakienda kwenye vyombo vya sheria hawapati ushirikiano wa maana.Jamani, tukubali tukatae, halali ya kila mwenye kosa ni kupelekwa kwwnye vyombo vya sheria, ila kwakua vibaka wanakera na polisi huwa wanawaachia, basi wapewe kichapo tu kama bakora za kutosha kisa wapelekwe polisi, ila kukatana mikono na miguu kisha kumuua nashani si ubinadamu