Kijana aliyeuawa na watu wanaojiita Sungu sungu Mburahati, Rais Samia ingilia kati

Suchak ongea kwa hoja...sheria ipi inaruhusu sungu sungu waue?

Baada ya kuuawa Jongo utafuata wewe......
Sheria ipi inaruhusu kuchukua Mali ya mwenzio kwa nguvu.

Ifike mahali na nyie mnaofeli KWENYE malezi mchomwe, inaonekana unafaidika kwa namna Moja ama nyingine na ukibaka wa mwanao jumanne.
 
Kajifunze kulea Kwanza ndo ulete vifungu vyako
 
Kibaka akikamatwa kwenye tukio malizaneni nae hapo hapo nasema mpelekeni kwa mola wake akatubu hakuna kulea kibaka sijui mwizi ukimkamata hakikisha hatokaa apate nafasi ya kumwibia mwingine tena
 
Kuua sio poa, ila wananchi nao wamechoshwa na usumbufu wa hawa vibaka na kila wakienda kwenye vyombo vya sheria hawapati ushirikiano wa maana.

Kuna clip moja inatembea mitandaoni ya kibaka mmoja alijificha kwenye dari ya nyumba moja ya biashara, wenye hasira zao wakamsokoa huko akaanguka chini.
Dah...! walimpokea kwa fimbo, mawe na rungu, jamaa akaanguka chini wakamalizia kwa tofali za kichwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…