Ambokile Amanzi
JF-Expert Member
- Dec 12, 2018
- 965
- 1,333
Haya sawa.Kwa kuwa humu hatujuani tulicho somea ngoja nitulie, ila ukiamini uchawi lazima uwe duni kimaendeleo hata ukiumwa malaria yale yanayo leta ukichaa utasema umelogwa, hapo ndo umuhimu wa elimu unajulikana. Wenzetu wanajikita kwenye programming (OOPS ) sizani kama utakuwa unajua maana hii tunaijua tulio somea civics tu , wewe jikite kutafuta uchawi tuone kama unaendelea.
Ngoja nikuambie kisa kimoja labda utaelewa, miaka ya tisini kuna kaka yangu alifaulu kwenda special school, nikiwa mdogo niliwasikia watu walisema haiwezekani mtu afaulu kama vile bila kuwa mchawi, ingawa nilikuwa mtoto ilinikatisha tamaa sana maana nilikulia katika mazingira ya dini hadi nikawa najisemea kuwa mimi Sitaweza kuwa msomi ikiwa uchawi unahusika, ila mpaka hapa nimefika na utu uzima wangu sijawahi feli katika mitihani yangu yote na sina hata chale mwilini. Na wale ambao nawakumbuka walikuwa wanamsema ndugu yangu hawana chochote, tukienda likizo ni kutuomba pesa utafikiri walitukopesha. Amini katika uchawi ufe masikini au uwe mtumwa wa tunguli.