Kijana baada ya kumaliza masomo yako mjini ni wakati wa kurudi nyumbani kijijini, wazazi wako wanakungoja

Na wazazi wakamgeuza house girl badala wamtafutie kitu cha kujishugulisha.

Ajira ni changamoto
 
Na wazazi wakamgeuza house girl badala wamtafutie kitu cha kujishugulisha.

Ajira ni changamoto
sure,
yupo kaka yangu mkali sana,
kijana wake hakufaulu kidato cha nne, kijana amechunga sana ng'ombe na nguruwe za nyumbani kwao,

mimi na yeye hatukonana kitambo kidogo,
majuzi nimekutana nae mjini, kwanza kabadilika sana na ametakata vizuri sana,

nikamuuliza kulikoni mjini, unafanya nini? akanijibu hua kila baada ya wiki moja anakuja mjini naleta nguruwe wazima na kuwauza...

nikamuhoji biashara ikoje lakini,
akasema sio mbaya na ndio maana kila wiki niko mjini ingawa wanyama hao si wengi sana huko vijijini tunapoenda kuwanunua kwasasa,

akanieleza kua safari hii amekuja na nguruwe wenye jumla ya kilo294,
na kila kilo ya nguruwe nauza elfu10...

sikutaka kuuliza zaidi,
ila kwa nilivyopima maelezo yake ni kwamba anatengeneza pesa mingi sana kwa mwezi mara 3 au 4 ya mwenye mshahara wa laki6 au 7 kwa mwezi,

gentleman,
hii si fursa ya kuchangamkia kabisa kuondokana na unyonge wa kiuchumi πŸ’
 
Mwenyewe ulishindwa kurudi kijijini kwenu ukajisali kuwa chawa wa CCM mjini.
 
Halafu
 
Aiseeee mkuu ulivyoandika hapa kuna watu haya ndo maisha yao halisi yaani umepiga panapouma...🀣

Nimekumbuka miaka hiyo ya nyuma nilikuwa nimemaliza tu chuo nikakaza nibaki mjini aisee nilipigika ile mbaya, siku moja mshua kanipigia simu ananiambia unafanya nini huko si urudi tu nyumbani....

Nilikuwa mpole balaa huku moyoni nikijisemea daah mshua kajuaje hali ninayopitia ile sijakaa vizuri nikaona muamala wa 200k ya nauli na matumizi madogo! MAISHA HAYA YAACHE TUπŸ˜€πŸ˜€
 
unaona sasa,
sasa hivi unakula maisha kijijini saaaafi, na ukitaka kuja kula bata mjini unakuja tu bila mbambamba yoyote lakini una uhakika wa kila kitu..

ni kujipanga, kuamua na kuthubutu tu maisha unatoboa maisha πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ’ͺ
 
unaona sasa,
sasa hivi unakula maisha kijijini saaaafi, na ukitaka kuja kula bata mjini unakuja tu bila mbambamba yoyote lakini una uhakika wa kila kitu..

ni kujipanga, kuamua na kuthubutu tu maisha unatoboa maisha πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ’ͺ
HahaπŸ˜‚ nilishatoka huko kwa sasa nipo ndani jiji moja hivi kubwa, hicho ni kipindi cha miaka kama 6 nyuma hahaha.....
 
unaona sasa,
sasa hivi unakula maisha kijijini saaaafi, na ukitaka kuja kula bata mjini unakuja tu bila mbambamba yoyote lakini una uhakika wa kila kitu..

ni kujipanga, kuamua na kuthubutu tu maisha unatoboa maisha πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ’ͺ
Haya mambo yapo na wala sio utani, vijana waache kung'ang'ania mjini kama pamewashinda.

Unakuta kijana hana kazi ya kueleweka anashinda anazurula tu, kodi anadaiwa kila siku ni kumpiga chenga mwenye nyumba inafika hatua anaondoka saa 11 asubuhi kurudi saa 8 usiku ili wasigongane na mother house.

Kingine ambacho ni aibu mtu upo mjini lakini ukipigiwa simu na ndugu, jamaa na marafiki kuwa tumefika mjini tuje walau tukusalimie unabaki kutoa sababu za uongo tu kumbe hutak wajue maisha unayoishi kwa vile yanatia huzuni...

Mwisho:VIJANA BADILIKENI ACHENI KUNG'ANG'ANIA MJINI TZ MAPORI NI MENGI NA KUNA FURSA KIBAO.
 
huo ni ukweli kabisa gentleman,

kuna kijana wa darasa la saba7 tu wa hapo kijijini kwetu, kila wiki analeta mjini wanyama aina ya nguruwe kati ya 10-15 kutoka mkoani, anaondoka na kati ya milioni3-4. Just imagine hata 25 hajafika...

kijana anazurura kuwanunua hao mifugo huko kijijini anawakusanya pamoja wenzake wanawakusanya wanajaza Lori la kukodi wanaleta mzigo town within 2 to 3days anarudi kijijini..

lakin kuna jamaa anaisubiri laki6 yenye makato kibao for 30days na mwingine hana kabisa hata hiyo πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…