Kijana huwezi tajirika kwa kuuza popcorn Makumbusho

Bado hm aujatuma.
 
Sio kila asiyetoboa hana akili,

Maisha ni FUMBO kubwa sana
Sasa kama ma tabula rasa akina nanii ndio wakuu wa mikoa, waenezi wanangoa madokta kwenye nafasi zao, akina giggy money wana fanya biashara za uchi na wanakaa apprtments mikocheni wanalipa kwa dola, wakati kuna watu na digree zao mwaka wa 5 huu wapo wanazunguka na bahasha mikononi,
 
Bakhresa ametajirika kwa kuuza chapati na maandazi.
Utajiri ni spritual.
Usikariri kila mtu akafanye biashara ya mbao.
 
Bakhresa ametajirika kwa kuuza chapati na maandazi.
Utajiri ni spritual.
Usikariri kila mtu akafanye biashara ya mbao.
Kuna waliofilisika kwa kuuza chapati na maandazi, tusikariri.

Wachaga zamani walikuwa na story zao sijui Mengi alianza kwa kuuza karanga, basi kila mkibosho akishuka mjini anauza karanga, karibu wote walikuja kufa maskini.

Ruge Mutahaba mwenyewe kwa kutumia jina la Diamond alileta diamond Karanga na ikafilisika.
 
Ukitaka kujua kuwa we si mtanzania Omba Passport.
 
Mithali 30:8


8 Uniondolee ubatili na uongo; Usinipe umaskini wala utajiri; Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.

9 Nisije nikashiba nikakukana, Nikasema, Bwana ni nani? Wala nisiwe maskini sana nikaiba, Na kulitaja bure jina la Mungu wangu.
 
Acheni watu wahangaike na maisha kwa namna ambavyo ni halali bila kuvunja sheria hata kama anapata 5000 kwa siku, nani amekuambia kwamba watauza maji/popcorn maisha yao yote, kama wewe unafikiri umefanikiwa, waonyeshe njia ya mafanikio hatua kwa hatua sio kukandia

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
wewe mwandishi una utajiri kiasi gani? Siri ya biashara yoyote ni mauzo makubwa Kuna mtu namfahamu anauza mahindi ya kuchoma 200 kwa siku, hao wanaotembeza popcorn makumbusho ni wafanyakazi ina maana biashara inalipa wapo location nzuri sawa na mwenge ya zamani jamaa wanakunja 50k faida kwa siku maana kiroba cha mahindi 20kg kinaisha ndani ya siku 2 usilolijua ni sawa na usiku wa giza labda kama unachangamsha genge!
 
Kazi nyingi wanazo fanya vijana wa dar faida huwa zinaanzia 20k hadi 50k huwezi ishi kwa kipato cha elfu tano maisha ya dar

Nauli
Kula na kunywa
Kodi
Bili ya Maj na umeme

Braza utatoaje kwa hiyo elfu tano
 
Kuna watu dar wanapaona kama USA vile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…