Kijana huwezi tajirika kwa kuuza popcorn Makumbusho

Kijana huwezi tajirika kwa kuuza popcorn Makumbusho

Kuna mda huwa nawaza naishia kucheka tu [emoji3][emoji3][emoji3], ivi mtu una miaka zaidi ya saba wewe unauzaga popcorn tu, wengine wanatembeza Maji barabarani nusra wagongwe na magari Kwa faida ya elfu tano kwa siku.

Mtaji ni changamoto lakini ebu sisi kama vijana tujitahidi kusave kidogo kidogo ili tutoke huko kwenye uchuuzi wa hand to mouth, upo Dar miaka zaidi ya kumi hutaki kurudi kwenu afu biashara yenyewe unauza mahindi ya kuchoma vyombo Dovya. Huna akili.
Tuwekee picha za hao vijana wenzako tuwasute
 
Kila unapo kuja mjini bila konekisheni kutoboa sio rahisi wengi walio kuja miaka ya 2000 bila wenyeji wanao eleweka bado wako ubungo wengine mbezi magufuli wana sukuma turoli wengine wana uza maji wagine wapiga debe, maisha yanahitaji msaada ya mtu alio toboa, ni wachache wanao fanikiwa bila msaada wa ndgu jamaa au rafiki.
Hii nina ushaidi nayo
 
Bro! Maisha ni magumu Sana kijijini,
Hapa mjini, unaweza, kupata chakula cha Mia tano!Kijijini, inabidi ulime,uchome mkaa, utengeneze gongo,mpaka uchakae! Nani anataka mateso bro! Kama umeishapita njia ya iringa, mlima kitonga, kuna vijana wanalima nyanya, hawa hata upite usiku wa manane!utawakuta mle polini,wanasubili wateja!watu wanachuuza vitu kutafuta ahueni ya maisha, kijijini, bodaboda unambeba Nani? Hata ukilima mazao, utamuuzia Nani, watu ni maskini mno!kijijini kwetu,kaya nyingi chai ya asubuhi hakuna, watu hawawezi hata kununua majani yq chai, wanasaga kahawa, au kuchoma sukari!
Sukari na majani ya chai ipi bei mkuu..?
 
Kuna mda huwa nawaza naishia kucheka tu [emoji3][emoji3][emoji3], ivi mtu una miaka zaidi ya saba wewe unauzaga popcorn tu, wengine wanatembeza Maji barabarani nusra wagongwe na magari Kwa faida ya elfu tano kwa siku.

Mtaji ni changamoto lakini ebu sisi kama vijana tujitahidi kusave kidogo kidogo ili tutoke huko kwenye uchuuzi wa hand to mouth, upo Dar miaka zaidi ya kumi hutaki kurudi kwenu afu biashara yenyewe unauza mahindi ya kuchoma vyombo Dovya. Huna akili.
Aisee ,walimu umewapa likizo au sio ? [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Duh ina maana Dar ishakuwa saturated since 2000's!

Japo hii mentality ya kuhitaji connection naona tunayo sana sisi wabongo. Mbona wenzetu wasomali, wakenya, wa nigeria na wale wa west africa hua wanaenda nchi za watu, hakuna wanaemjua, wanapambana mpaka wanatoboa

Lakn sisi wabongo mtu kutoka tu hapo mwanza kuja dar anahtaji connection!!
Jambo lolote unalolifanya ili utoboe UNAHITAJI MENTOR.
Mentor ni mwalimu wako na mshauri wako.

#YNWA
 
Kuna mda huwa nawaza naishia kucheka tu [emoji3][emoji3][emoji3], ivi mtu una miaka zaidi ya saba wewe unauzaga popcorn tu, wengine wanatembeza Maji barabarani nusra wagongwe na magari Kwa faida ya elfu tano kwa siku.

Mtaji ni changamoto lakini ebu sisi kama vijana tujitahidi kusave kidogo kidogo ili tutoke huko kwenye uchuuzi wa hand to mouth, upo Dar miaka zaidi ya kumi hutaki kurudi kwenu afu biashara yenyewe unauza mahindi ya kuchoma vyombo Dovya. Huna akili.
Kheri ya kuuza popcorn na kuchoma mahindi kuliko kuwa kula kulala, kukaa kijiweni, kuwa na visingizio huna wa kukuwezesha, kuponda kazi za wenzako, kujifanya mjuaji kwamba kushinda maisha lazima ufanye kazi maofisini au kutapeliwa na watu wa forex, forever living and such...
Yoyote apataye hela halali kudos kwake, na wengine tunanunuwa bidhaa kwao mpaka kieleweke
 
Biashara ya PDF.

#YNWA
Nimefanya kazi kwenye sekta ya mahindi mabichi kwa miaka mitatu.

Mfano mdogo, wale wamama wanao tembeza mahindi mabichi pale Mbezi Beach huwa wanayanunua kwa bei kati ya 300-450, na hali ikiwa ya mvua kama sasa hivi anauza mahindi si chini ya 50 kwa bei ya 1,000/= ambapo faida ni elfu 25; ni kwamba anaenda sokoni saa 12 asubuhi ananunua na kuuza by saa 3 au nne amemaliza, na kwenda kununua mengine.

Kwa hiyo kwa siku anapata kati ya elfu 20-30 faida.

Sasa kama ni PDF endelea kuamini hivyo
 
Unaweza ukafikiri uwezavyo kulingana na IQ yako.
Wakati mwingine unaweza kukuta mtu anashona na kukarabati,kung'arisha viatu (shoes shiner) kwa miaka na miaka na kama huijui ama huna uelewa wa hii kazi ukasema uwezavyo.

Kuna siri moja ama zaidi ikiwa ni pamoja na;
1: Eneo alofanyia kazi au biashara halina ushindani wala bughudha za kulogana wala kutozwa kodi na akitoa matumizi nyumbani bado anabaki labda 15K.

2: Kutokana na hiyo biashara alishawekeza maeneo mengine na hivyo anaendelea kuheshimu hiyo kazi lkn pia inafanya watu wasimshitukie kwakuwa tu wanaidharau hiyo kazi na yeye anakimbiza kimyakimya.

3: Mara nyingi kwa watu wengi akifanya kazi flani kwa muda mrefu inafikia wakati anahofia kuacha ili akajaribu kwingine kwa kuhisi kuwa akianguka atakosa namna ya kuinuka tena.

Hii husababishwa na kukosa kujiamini na wengi imewaharibia sana na hasa kwa wale walio ajiriwa,hata km anapewa ujira kidoogo utamuona kila siku yupo.

Kwa mfano,hawa waitwao house girl,akiaminiwa sehemu na akapewa uhakika wa ajira hata akifikisha umri wa miaka 40 unaweza kukuta anadhani hajafikia umri wa kuolewa ama kujitegemea pengine hata yeye akatoa hiyo ajira kwa wengine.

Angalia wanaoganya kazi madukani kwa Wahindi,kwanza ni lazima anyimwe muda wa kupata wazo jipya,muda wote akili imetekwa na kazi za Mhindi (binadamu siyo mmea) na hii mbinu inapandikiza uoga wa kujitegemea ama kuhisi kuwa akitoka hapo hatakuwa na maisha tena.
 
Back
Top Bottom