Kijana huwezi tajirika kwa kuuza popcorn Makumbusho

Tuwekee picha za hao vijana wenzako tuwasute
 
Hii nina ushaidi nayo
 
Sukari na majani ya chai ipi bei mkuu..?
 
Aisee ,walimu umewapa likizo au sio ? [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Jambo lolote unalolifanya ili utoboe UNAHITAJI MENTOR.
Mentor ni mwalimu wako na mshauri wako.

#YNWA
 
Hapo kwenye mahindi ya kuchoma ninakupinga.

Wachoma mahindi wanaigiza faida kati elfu 20 hadi 60 kwa siku. Na biashara yao huwa nzuri zaidi kipindi cha mvua haswa Disemba-May
Biashara ya PDF.

#YNWA
 
Kheri ya kuuza popcorn na kuchoma mahindi kuliko kuwa kula kulala, kukaa kijiweni, kuwa na visingizio huna wa kukuwezesha, kuponda kazi za wenzako, kujifanya mjuaji kwamba kushinda maisha lazima ufanye kazi maofisini au kutapeliwa na watu wa forex, forever living and such...
Yoyote apataye hela halali kudos kwake, na wengine tunanunuwa bidhaa kwao mpaka kieleweke
 
Biashara ya PDF.

#YNWA
Nimefanya kazi kwenye sekta ya mahindi mabichi kwa miaka mitatu.

Mfano mdogo, wale wamama wanao tembeza mahindi mabichi pale Mbezi Beach huwa wanayanunua kwa bei kati ya 300-450, na hali ikiwa ya mvua kama sasa hivi anauza mahindi si chini ya 50 kwa bei ya 1,000/= ambapo faida ni elfu 25; ni kwamba anaenda sokoni saa 12 asubuhi ananunua na kuuza by saa 3 au nne amemaliza, na kwenda kununua mengine.

Kwa hiyo kwa siku anapata kati ya elfu 20-30 faida.

Sasa kama ni PDF endelea kuamini hivyo
 
Unaweza ukafikiri uwezavyo kulingana na IQ yako.
Wakati mwingine unaweza kukuta mtu anashona na kukarabati,kung'arisha viatu (shoes shiner) kwa miaka na miaka na kama huijui ama huna uelewa wa hii kazi ukasema uwezavyo.

Kuna siri moja ama zaidi ikiwa ni pamoja na;
1: Eneo alofanyia kazi au biashara halina ushindani wala bughudha za kulogana wala kutozwa kodi na akitoa matumizi nyumbani bado anabaki labda 15K.

2: Kutokana na hiyo biashara alishawekeza maeneo mengine na hivyo anaendelea kuheshimu hiyo kazi lkn pia inafanya watu wasimshitukie kwakuwa tu wanaidharau hiyo kazi na yeye anakimbiza kimyakimya.

3: Mara nyingi kwa watu wengi akifanya kazi flani kwa muda mrefu inafikia wakati anahofia kuacha ili akajaribu kwingine kwa kuhisi kuwa akianguka atakosa namna ya kuinuka tena.

Hii husababishwa na kukosa kujiamini na wengi imewaharibia sana na hasa kwa wale walio ajiriwa,hata km anapewa ujira kidoogo utamuona kila siku yupo.

Kwa mfano,hawa waitwao house girl,akiaminiwa sehemu na akapewa uhakika wa ajira hata akifikisha umri wa miaka 40 unaweza kukuta anadhani hajafikia umri wa kuolewa ama kujitegemea pengine hata yeye akatoa hiyo ajira kwa wengine.

Angalia wanaoganya kazi madukani kwa Wahindi,kwanza ni lazima anyimwe muda wa kupata wazo jipya,muda wote akili imetekwa na kazi za Mhindi (binadamu siyo mmea) na hii mbinu inapandikiza uoga wa kujitegemea ama kuhisi kuwa akitoka hapo hatakuwa na maisha tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…