Kijana jitahidi ujifunze angalau lugha mbili za kimataifa

Kijana jitahidi ujifunze angalau lugha mbili za kimataifa

Nje ya mada kdg.

Kijana pambana unapo ona pana mwanya wa mafanikio.

Kuna watu vijijini wanavuja majasho kwenye mashamba na jua limewaka hatari.

Mtu analima na hajui kama atavuna.
 
Tafuta pesa bana acha
Mbambamba
nmekua nikifuatilia mahojiano meng sana ya watu mashuhuri duniani na weng wao hanajua lugha moja tu walozaliwa nayo au waliko tokea

Ukiwa mtu muhimu au mtu mwenye mafanikio lugha huwa haina maana wala haisaidii kitu

CR7
Messy
Neymar
Raisi ya india
Raisi wa china
CR mtoe kwenye hiyo list, anaongea lugha nne, kireno, kiingereza, kihispania na kiitaliano
 
kuwa najua kingereza then najifunza kifaransa. Natumia Youtube na Duolingo. Nimekosa mtu wa kupractise naye. Lakini bado najipa muda niweze kushika misamiati mingi na miundo kadhaa/ grammar.
Tuko pamoja kwenye hii safari. Mimi najifunza kifaransa kwa wivu mkubwa.
 
Wengi sana matajiri wafanyabiashara karibia wote hawajasoma kina Kishimba, madon wa migodi, ata wachina wakija huku si unaona wanatumia wakalimani which means ukiwa na hela utaeleweka tu unachotaka kusema
Maskini mnajipaga moyo kwa mifano ya kijinga.
 
Wengi sana matajiri wafanyabiashara karibia wote hawajasoma kina Kishimba, madon wa migodi, ata wachina wakija huku si unaona wanatumia wakalimani which means ukiwa na hela utaeleweka tu unachotaka kusema
Wewe pia ni tajiri? Kama sio wao wamekuzidi wapi?
 
kingereza tu wanafundishwa for more than 10 years na hawaelewi sembuse izo lugha nyingine?

talking from little experience, wabongo tumejifungia sana nchini mwetu, unaeza kwenda vacation/business trip nchi za watu usikutane na mbongo hata mmoja hotelini au mtaani zaidi utakutana na wakenya, wanaija, wazulu, washona, wakongomani, wasomalia, waganda, wanyarwanda.

najua uchumi ni tatizo but wake up guys, come on. try
Wewe unatosha ukiweza kwenda, acha masimango.
 
Mkuu umeongea jambo la msingi sana.

Ukienda United Arab Emirates na Qatar utakutana na wakenya wengi sana wanafanya kazi hasa za ulinzi, usafi n.k

Pia kwenye restaurants kumejaa wahudumu wa kikenya na wengi hata hawajasoma sana. Lakini kikubwa kilichowasaidia ni lugha ya kiingereza.

Watanzania wanapitwa na fursa nyingi kwa kuogopa lugha.

Watanzania wengi hata lugha ya kiingereza tu ni shida.

Ndio maana Kenya ina waandishi wa habari wakubwa wanaofanya kazi kwenye vyombo vikubwa vya habari kama CNN.

Pia kenya ina waandishi wa habari wakubwa wanaoweza kufanya interview na watu wakubwa kama maraisi, matajiri wakubwa, wafanyabishara wakubwa kwa sababu ya lugha yao imenyooka. Mfano mwandishi Larry Madowo wa CNN.

Vijana wakitanzania wanaishia kuitegemea serikali badala ya kwenda kuchangamkia fursa mambele...

Tatizo kuu lugha.
 
kingereza tu wanafundishwa for more than 10 years na hawaelewi sembuse izo lugha nyingine?

talking from little experience, wabongo tumejifungia sana nchini mwetu, unaeza kwenda vacation/business trip nchi za watu usikutane na mbongo hata mmoja hotelini au mtaani zaidi utakutana na wakenya, wanaija, wazulu, washona, wakongomani, wasomalia, waganda, wanyarwanda.

najua uchumi ni tatizo but wake up guys, come on. try
Dubai na Qatar kumefurika wakenya na waganda.

Na wanapiga kazi kwenye maeneo mengi sana.

Vijana wa kitanzania kazi kushinda vijiweni wakinywa kahawa na kashata wakibishana Simba na Yanga.

Ndio maana yule kijana mmiliki wa kampuni ya NALA mtanzania Benjamin Fernandez aliamua kuweka makao makuu ya kampuni yake Nairobi Kenya kwa Vijana smart upstairs wanaojielewa.

Sio hawa vijana wa kitanzania machawa wanaoshinda mitaani kusaka teuzi.
 
Back
Top Bottom