Kijana jitahidi ujifunze angalau lugha mbili za kimataifa

Kijana jitahidi ujifunze angalau lugha mbili za kimataifa

Mkuu umeongea jambo la msingi sana.

Ukienda United Arab Emirates na Qatar utakutana na wakenya wengi sana wanafanya kazi hasa za ulinzi, usafi n.k

Pia kwenye restaurants kumejaa wahudumu wa kikenya na wengi hata hawajasoma sana. Lakini kikubwa kilichowasaidia ni lugha ya kiingereza.

Watanzania wanapitwa na fursa nyingi kwa kuogopa lugha.

Watanzania wengi hata lugha ya kiingereza tu ni shida.

Ndio maana Kenya ina waandishi wa habari wakubwa wanaofanya kazi kwenye vyombo vikubwa vya habari kama CNN.

Pia kenya ina waandishi wa habari wakubwa wanaoweza kufanya interview na watu wakubwa kama maraisi, matajiri wakubwa, wafanyabishara wakubwa kwa sababu ya lugha yao imenyooka. Mfano mwandishi Larry Madowo wa CNN.

Vijana wakitanzania wanaishia kuitegemea serikali badala ya kwenda kuchangamkia fursa mambele...

Tatizo kuu lugha.
Kwenye comments wanakwambia mbona Kishimba na Msukuma hawajui kiingereza lakini wana hela 😄😄
 
Back
Top Bottom