Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Kijana jitunze, kuteremkia miaka 40+ kuna zimwi linaitwa Kisukari na Presha. Mkeo atakuvumilia?

Kwaiyo ukifanya yote hayo ndo utatoboa miaka 70+?
Miaka 40+ uo umri sio kufanya ngono ni kula Bata kwa Sana.

Mimi nikipata Yale Maisha ya kulala vizuri msosi uhakika yaani hito 40 yrs hata bila ngono naishi fresh
Msiba huo..
 
Pole Mkuu
Mbaya zaidi ukute yapo kwenye familia.
Kwa upande wa baba yangu sukari ipo inatembea kizazi hadi kizazi.
Basi nasi tunajua huko mbeleni kuna tutakaokuwa nao.
Imagine familia ya watu saba watatu tu ndio hawana sukari hawa waliobaki wanapambana nao.
Inabidi ujitunze sana,inaweza kusaidia kuukwepa,ingawa wa kurithi ni tatizo
 
Huu uzi umepata nguvu kwa sababu ndani yake kuna mambo na ngono na maudhui kama hayo, ambao kwa sasa sisi wabongo ndio mwelekeo wetu.

Yote ya yote ni uzi mzuri sana ambao kila mtu anapaswa auprint kwenye hard paper na pengine kubandika ukutani sebuleni na chumbani ili kila siku ukukumbushe kikupasacho kutenda kama kijana.
Naomba mbinu ya kuuprinti Mkuu
 
Kwema Wakuu!

Hatufuatiliani wala hatupangiani maisha. Ila tunakumbushana huku nami nikijikumbusha pia Kwa Nia nzuri tuu. Ili baadaye tusijekujikuta katika Huzuni kuu.

Vijana tunapoambiwa tule na tunywe Kwa nidhamu sio Kwa sababu tunaonewa wivu au kuna mtu anataka kuwa juu yetu Kwa kutupa amri. HASHA! Bali ni Kwa faida yetu.

Kisukari na Presha sio magonjwa mazuri Kwa ustawi wa Ndoa zetu. Ukisikia pigo Baya basi ni kukosa nguvu za kiume. Tena Kwa miaka 40 Kwa mwanaume bado ni kijana. Na Kwa bahati nzuri miaka hiyo wengi neema ndio zinazidi kufunguka na wamesha-settle. Sasa ume-settle halafu unajikuta huna nguvu za kiume. Asikuambie mtu inahuzunisha Sana..

Presha na kisukari yatakufanya ukose Raha ya maisha sio tuu kwenye ndoa Bali hata katika ulaji wako. Utapangiwa nini ule na kipi usile. Vyakula vizuri utabaki kuvitazama tuu, utakula chukuchuku na michemsho mpaka Ulie.
Ni akheri ujipangie sasa hivi Kula Milo mizuri Kwa kufuata kanuni za Afya ya Mwili.
Na ni akheri magonjwa hayo yakupate too late yaani huko miaka ya 80+ lakini sio 40+. Ni hatari na utateseka Sana. Miaka 80+ huna ulichobakiza, hata wewe mwenyewe utakiri kuwa umekula chumvi nyingi vyakutosha. Lakini sio miaka 40-60. Hiyo ni miaka michache Sana.

Ukiona Taikon anaelezea Jambo Fulani basi kaa nalo macho, lizingatie Sana. Kwa sababu Taikon nipo kwaajili ya kujenga na wala sio kubomoa.

1. Kula na kunywa vizuri,
i. Kula Mbomboga Kwa wingi, kula Protein Kama nyama nyeupe, maziwa, mayai, Kwa wingi,
Kula wanga kidogo Sana. Mfano unapika maharage mengi halafu unakula na wali kidunchu, au ugali kidogo na Samaki au nyama au maharage mengi.

ii. Matunda, pendelea Kula matunda,
Kama umeoa, pendelea Ndizi zilizoiva angalau kila siku moja hasa usiku, hii itafanya uume wako kuwa na nguvu kutokana na madini ya Potassium.

Mkeo aweke Kachumburi yenye Nyanya, vitunguu, limao na pilipili hizi zinaongeza Libido.
Safisha figo Kwa Matikiti, matango, usisahau mapapai na maembe, pia machungwa huku utapata vitamini

Weka chumvi kiasi yenye ladha ya Kwa mbali. Usiweke chumvi nyingi. Kuweka chumvi nyingi kuna sababisha hatari ya kupata Presha "Hypertension" ambayo sio nzuri Kwa Afya yako.

Kula Milo miwili ukiwa age ya 25-50 iwe balanced.

iii. Kunywa maji mengi, angalau Lita mbili na nusu mpaka tatu na nusu Kwa siku.
Pombe kunywa kiasi Kwa STAREHE sio kujiumiza. Angalau kwa wiki mara moja na hakikisha usinywe mpaka ukazima.

Maji mengi ni dawa kwani yanafanya seli za mwili wako kufanya kazi Kwa ufanisi zaidi. Maji hupunguza pia sumu mwilini na kuufanya mwili wako kuwa na Nuru.

Yaani mtu anayezingatia kunywa maji ngozi yake hung'aa

Pia maji mengi husababisha mtu kutokuzeeka Kwa haraka. Na hii ni kutokana na Uzalishwaji wa seli za mwili kufanyika Kwa ufanisi

2. Fanya mazoezi,
Mazoezi hujenga mwili na kuufanya kuwa na Afya, kwani hufanya mzunguko WA damu kufanya kazi vizuri. Kumbuka Damu ndio hubeba virutubisho na kuvisafitisha mwilini. Kumbuka pia ndani ya damu ndio kuna Seli nyeupe zinazolinda mwili dhidi ya magonjwa, Seli nyekundu ambazo husafirisha hewa ya Oksijeni kuzipa Seli, tishu na ogani Uhai. Hasahasa Ubongo.

Hii ni kusema mazoezi yanaimarisha ufanyaji kazi WA viungo vya Mwili Kama vile Ubongo. Hii inafanya akili kuwa active.

Aina ya mazoezi
i. . Mazoezi ya Mwili
Haya yanalenga zaidi viungo na organ za mwili. Kukimbia, Push-up n.k.

ii. Mazoezi ya Akili/Ufahamu.
Haya yanalenga zaidi tafakuri, uchanganuzi, uchambuzi, n.k. haya ni Kwa kusoma Nyaraka na vitabu, michezo na Bangua bongo, Game zinazoshughulisha akili n.k.
Pia mazoezi ya ubongo hufanyika Kwa kujaribu kufanya vitu vipya ili kutafuta changamoto mpya. Kama ni biashara, au kazi au miradi unaanzisha ili akili ipate changamoto mpya.

iii. Mazoezi ya Kiroho na Nafsi.
Haya hulenga zaidi roho na Nafsi yako.
Kudhibiti Nafsi yako na matamanio yake, mfano Kufunga Kula na kunywa,
Kama unapenda kunywa pombe kujizuia kutokunywa Kwa muda wa siku kadhaa.
Kama unapenda Kulala na wanawake, kujizuia hata Kwa miezi sita bila kuchepuka, hayo ni mazoezi ya kiroho na nafsi.
Pia kutoa Zaka au Sadaka Ile inayouma. Ni zoezi la Nafsi au kiroho.

Hii itakusaidia kujidhibiti, pia kuzuia Nyege mshindo au ukosefu wa maamuzi.

3. Mapumziko na Burudani/STAREHE.
Angalau Kwa siku ulale masaa yasiyopungua Nane.
Starehe au burudani angalau Kwa wiki au Kwa mwezi mara moja. Hii itakufanya usiyachoke maisha na kuyaona hayana maana.

Usingizi utakusaidia kutunza Ubongo wako na hii itakusaidia nyakati za uzeeni kwani utakuwa haupotezi kumbukumbu kijinga jinga.

Kabla watu hawajaona uzee wako wewe mwenyewe utaanza kuuona Kwanza Kwa kujikuta unasahau sahau mambo, na hiyo huanza kutokea miaka 30+ kama hutokuwa mtu wa kuzingatia mapumziko.

Kijana wa sasa unapaswa ujidhibiti mwenyewe ili isijekula kwako ufikishapo miaka 40.
Hakuna kitu kibaya Kama kufikisha umri huo yaani 40+ halafu ujikute hauna pesa, halafu magonjwa Kama kisukari na Presha vikupige. Ni hatari Sana.

Kupigiwa nje nje! Yaani mwanamke wako wala hatakuwa na Woga, nawe utakuwa unajua na chakumfanya hauna.

Wale mnaolalamika andiko refu nimewasikia. Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
mwagia moyo maji jamaa yangu usiogope magonjwa,hakuna aliyeishi milele
 
Umeongea ukweli,kama wapo watakao kuelewa watafaidika na ushauri wako,
Nina 48 na nimepata kisukari kipndi cha mafanikio yangu,ninachotaka napata ila ninamisi maisha halisi niliyojioangia iwapo ntafanikiwa,nilitamani niowe wake watatu ila sasa siweiz
Kuna vyakula natamani sana kula hivi sasa ni sumu kwangu nawanunulia watu tu na watoto wangu
Kuwa makini na kisukari ndugu
Kuna watu wengi watakufata kuwa wana dawa na watakula pesa zako na unabaki na kisukari chako hivho hivyo
Nayoandika hapa spambi habari ninapambana na hii hali wakati wote nikilazimisha furaha
KUWENI MAKINI KUJIRINDA DHIDI YA KISUKALI
Pole sana Mkuu.
 
Hongera kwa bango zuri mkuu,

Sisi wenye 40+ tunakuelewa sana ila niongezee hapo kwenye kula healthy, mazoezi, mapumziko ya kutosha n.k tunatakiwa kuwa na uchumi imara.

Trust me, kama uchumi unayumba hasa ukiwa late 30s na early 40s kuna vitu vingi sana mwili utapata shida. Tengeneza investments zenye uhakika au ajira ambayo walau ni ya uhakika ili wakati huu uko 40s uweze kusomesha madogo bila tatizo, uwe na nyumba walau kodi isiwe tatizo, uwe na stable family nk.

Wazungu wanasema life begins at 40, wakimaanisha at 40 uneshamalizana na kashkashi za maisha, vijana wameenda shule wanamalizia huko but kibongobongo 40 ndio tunasomesha primary na secondary, wengine bahati mbaya hata nyumba hatuna..its hectic asee.
 
Huu uzi umepata nguvu kwa sababu ndani yake kuna mambo na ngono na maudhui kama hayo, ambao kwa sasa sisi wabongo ndio mwelekeo wetu.

Yote ya yote ni uzi mzuri sana ambao kila mtu anapaswa auprint kwenye hard paper na pengine kubandika ukutani sebuleni na chumbani ili kila siku ukukumbushe kikupasacho kutenda kama kijana.

Na Mimi nimechomekea suala la ngono makusudical ili kufikisha kile nilichotaka watu wakipate.
 
Hongera kwa bango zuri mkuu,

Sisi wenye 40+ tunakuelewa sana ila niongezee hapo kwenye kula healthy, mazoezi, mapumziko ya kutosha n.k tunatakiwa kuwa na uchumi imara.

Trust me, kama uchumi unayumba hasa ukiwa late 30s na early 40s kuna vitu vingi sana mwili utapata shida. Tengeneza investments zenye uhakika au ajira ambayo walau ni ya uhakika ili wakati huu uko 40s uweze kusomesha madogo bila tatizo, uwe na nyumba walau kodi isiwe tatizo, uwe na stable family nk.

Wazungu wanasema life begins at 40, wakimaanisha at 40 uneshamalizana na kashkashi za maisha, vijana wameenda shule wanamalizia huko but kibongobongo 40 ndio tunasomesha primary na secondary, wengine bahati mbaya hata nyumba hatuna..its hectic asee.

Inatisha Sana. Unaweza ukapagawa Asee!
 
Inatisha Sana. Unaweza ukapagawa Asee!
Ndio maana wapo wanaojiua kabisa, uwezo wa kufanya maamuzi sahihi wanakosa, msongo wa mawazo, kipato duni, vijana wapo watano hujui pa kuwapeleka, madeni kila kona...asee ni shida ambiere!!
 
😀😀
Ukikaa na Watu wazima au Wazee ukazitambua changamoto zao huwezi ongea hivyo
nyerere yuko wapi?mugabe je?,samora mashel,mobutu,mkapa,magufuli,gadafi,sadam hussein na wengi tu,walikuwa wakipangiwa misosi lakini walidanji,,,,,kula pombe weyee
 
Hongera kwa bango zuri mkuu,

Sisi wenye 40+ tunakuelewa sana ila niongezee hapo kwenye kula healthy, mazoezi, mapumziko ya kutosha n.k tunatakiwa kuwa na uchumi imara.

Trust me, kama uchumi unayumba hasa ukiwa late 30s na early 40s kuna vitu vingi sana mwili utapata shida. Tengeneza investments zenye uhakika au ajira ambayo walau ni ya uhakika ili wakati huu uko 40s uweze kusomesha madogo bila tatizo, uwe na nyumba walau kodi isiwe tatizo, uwe na stable family nk.

Wazungu wanasema life begins at 40, wakimaanisha at 40 uneshamalizana na kashkashi za maisha, vijana wameenda shule wanamalizia huko but kibongobongo 40 ndio tunasomesha primary na secondary, wengine bahati mbaya hata nyumba hatuna..its hectic asee.
Wenye 40+ tunasoma huku tunasema inhiiiiiiii! Tunashukuru Mungu hata tukifika sehemu tukitaja umri watu wanabisha, kwamba we still look young and healthy. Vimichepuko ndio havitaki kusikia kuwa tunakaribia umri wa baba zao!
 
nyerere yuko wapi?mugabe je?,samora mashel,mobutu,mkapa,magufuli,gadafi,sadam hussein na wengi tu,walikuwa wakipangiwa misosi lakini walidanji,,,,,kula pombe weyee
Mkuu ulitaka waishi milele? Katika uliowataja wapo waliofika 90+. Saddam, Machel na Gaddaf waliuawa. Hakuna binadamu atakaeishi milele ila inauma wazazi kuzika watoto wao.
 
Back
Top Bottom