Kijana: Maisha ya mtaani hayatambui cheti

Kijana: Maisha ya mtaani hayatambui cheti

Kwa sasa Elimu imekuwa hitaji la lazima kwa binadamu yeyote duniani

Na ikiwa huajapata Elimu inakubidi ukae na waliosoma wakuelekeze baadhi ya mambo Fulani .

Mtaa hautambui Cheti Ila mtaa unatambua maarifa ambayo mtu anayapata kupitia elimu.
Umemaliza kitu Dr.
 
Ni kweli elimu yetu haimuwezeshi muhitimu kukabiliana na changamoto za kimaisha lakini nafikiri tumei-underestimate sana elimu yetu na wasomi wetu kuliko uhalisia.

Mtaani population kubwa zaidi ya ambao hawajasoma ndio wana maisha magumu ukilinganisha na waliosoma. Vilevile waliosoma wanataabika kwa kipindi kifupi tu kabla ya kuliotea goli tofauti na hawa ambao hawajasoma population kubwa zaidi wanaishia kwenye ufukara maisha yao yote.

Nafikiri hii trend ya kuwadharau wasomi kwa kiasi kikubwa inatokana na ukimya wa wasomi waliotoboa. Kuna wasomi wengi wana maisha mazuri lakini hawana kelele tofauti na ambao hawajasoma wakiliotea tu goli wanakua na kelele nyingi sana.

Tuache kudanganya vijana, bado elimu ina mchango mkubwa sana na kuna wasomi wengi wanafanya vizuri kimaish
Sahihi kabisa
 
Bado upo gizani, na umepumbazwa kuhusu vyeti ambavyo huko duniani wameanza kuvikataa! Umejiuliza kwa nini Elon Musk alitoa hii kauli???

Njoo duniani (mtaani) uone vichwa halisi!
Punguza hasira mkuu. Kuwa na chuki au wivu dhidi ya aliekuzidi kielimu haitakusaidia chochote. Mimi ni msomi na elimu yangu imenisaidia mambo mengi sana, so far nipo kwenye uelekeo mzuri kwa kipato na maisha kwa ujumla.

Kwenye jamii ninayoishi nachangamana na ndugu, majirani, jamaa na marafiki katika circle yangu naona population kubwa zaidi ya ambao hawajasoma ndio wenye maisha magumu kuliko waliosoma.

Mfano mdogo tu hapa nimetulia kwenye grocery moja hivi mtaani kwangu. Kuna kijana kahitimu degree ya usimamizi wa biashara ana factory yake ya viatu bado ni ofisi ndogo lakini unaona kuna potential ya kukua wakati upande wa pili wa barabara kuna shoeshine mtu mzima kielemu ni std 7. yupo hapa mtaani takribani mwaka wa 5 anaishi kwa kubangaiza tu
 
Ni kweli elimu yetu haimuwezeshi muhitimu kukabiliana na changamoto za kimaisha lakini nafikiri tumei-underestimate sana elimu yetu na wasomi wetu kuliko uhalisia.

Mtaani population kubwa zaidi ya ambao hawajasoma ndio wana maisha magumu ukilinganisha na waliosoma. Vilevile waliosoma wanataabika kwa kipindi kifupi tu kabla ya kuliotea goli tofauti na hawa ambao hawajasoma population kubwa zaidi wanaishia kwenye ufukara maisha yao yote.

Nafikiri hii trend ya kuwadharau wasomi kwa kiasi kikubwa inatokana na ukimya wa wasomi waliotoboa. Kuna wasomi wengi wana maisha mazuri lakini hawana kelele tofauti na ambao hawajasoma wakiliotea tu goli wanakua na kelele nyingi sana.

Tuache kudanganya vijana, bado elimu ina mchango mkubwa sana na kuna wasomi wengi wanafanya vizuri kimaisha
hii ndiyo point elimu bado ni muhimu
 
Ile kuwa uone nilidhani magorofa
Kumbe mwana ukomed hakuna Cha kuokota.
 
Kuwa na chuki au wivu dhidi ya aliekuzidi kielimu haitakusaidia chochote
Kupishana mtazamo ndiyo wivu na chuki?? Elon Musk ana wivu??Umejuaje kama umenizidi kielimu??
Mimi ni msomi na elimu yangu imenisaidia mambo mengi sana
Unavyohisi elimu yako imekusaidia kujitambua??
katika circle yangu naona population kubwa zaidi ya ambao hawajasoma ndio wenye maisha magumu kuliko waliosoma.
Mimi ninao wasomi walionizunguka wa shahada moja mpaka tatu halafu wana maisha magumu.

Nimekuambia tembea duniani coz bado upo gizani! Halafu unaonekana limbukeni coz kitendo cha kujiita 'mimi msomi' kimeonyesha ushamba na ulimbukeni.
 
Kupishana mtazamo ndiyo wivu na chuki?? Elon Musk ana wivu??Umejuaje kama umenizidi kielimu??

Unavyohisi elimu yako imekusaidia kujitambua??

Mimi ninao wasomi walionizunguka wa shahada moja mpaka tatu halafu wana maisha magumu.

Nimekuambia tembea duniani coz bado upo gizani! Halafu unaonekana limbukeni coz kitendo cha kujiita 'mimi msomi' kimeonyesha ushamba na ulimbukeni.
Population ya wasiosoma na waliosoma bado ambao hawajasoma wana maisha duni zaidi ukitaka kujua ilo angalia makazi ya watu wengi wliosoma na ambao hawajasoma. Mfano masaki na tandare utaona kuna utofauti mkubwa sana
 
Umesema kwa sauti ya kawaida lakin huo ujumbe nimgumu na mzito pia si rahisi hata kidogo.
 
wliosoma na ambao hawajasoma. Mfano masaki na tandare utaona kuna utofauti mkubwa sana
Ndiyo maana nimekuambia tembea coz hakuna elimu nzuri kama kutembea! Unaona mpaka sasa unaamini Tandale hakuna wasomi na ndiyo maana ni masikini!

Halafu Masaki ni wasomi na ndiyo maana ni matajiri!
Yaani kwako sehemu yenye wasomi ndiyo kuna matajiri!Yaani ukipata shahada ya kwanza na kuendelea basi una asilimia kubwa ya kuwa tajiri!
 
Elimu ni muhimu Kuna vitu vingi itakufungua macho na akili...

Huwezi sema kwakua ajira hamna watu wasisome ama wasitafute hizo ajira jibu ni hapana...

Hata walioenda veta wapo ambao vilevile hawana kazi au maisha magumu.....

Nadhani kikubwa ni mwanafunzi aji assess mwenyewe na aone umuhimu wa maarifa pamoja na ujuzi mwingine wakati ambao soko la ajira ni gumu.....
 
Ndiyo maana nimekuambia tembea coz hakuna elimu nzuri kama kutembea! Unaona mpaka sasa unaamini Tandale hakuna wasomi na ndiyo maana ni masikini!

Halafu Masaki ni wasomi na ndiyo maana ni matajiri!
Yaani kwako sehemu yenye wasomi ndiyo kuna matajiri!Yaani ukipata shahada ya kwanza na kuendelea basi una asilimia kubwa ya kuwa tajiri!
Nini ambacho hauelewi kijana? Tatizo mnawakandia wasomi kwa kufanya rejea ya majobless na matendo ya wanasiasa(mfano Lipumba, Kabudi n.k) lakini wapo wasomi wanaofanya makubwa sema tu hawasikiki kwa sababu hawana makelele. Embu niambie Max Mello angekua std 7 angeweza kuwa founder wa jf ambayo inatukutanisha mimi na wewe?

Tafuta jamii mbili tofauti. Jamii A ina population kubwa ya wasomi, jamii B ina population kubwa ya wasiosoma halafu fanya ulinganisho ni jamii ipi imestaarabika na imeendelea zaidi kiuchumi. Sio lazima iwe Masaki na Tandare, unaweza kuzitaja yoyote hapa halafu tufanye ulinganisho.
 
Embu niambie Max Mello angekua std 7 angeweza kuwa founder wa jf ambayo inatukutanisha mimi na wewe?
Hivi yule founder na mmiliki wa WCB ana elimu gani?? Ametokea wapi?? Halafu acha kujivunia elimu ya bongo utafikiri kama hatuifahamu!
Huyo founder wa jamii forum unaifahamu elimu yake vizuri??
 
Hivi yule founder na mmiliki wa WCB ana elimu gani?? Ametokea wapi?? Halafu acha kujivunia elimu ya bongo utafikiri kama hatuifahamu!
Huyo founder wa jamii forum unaifahamu elimu yake vizuri??
Dah.! Mzee baba tunaelewana kweli? Unajua maana ya population? Population maana yake idadi ya watu wote(sijui kwa neno moja la kiswahili inaitwaje) Mimi najenga hoja kwa kuangalia population ya jamii nzima, wewe unaongelea mtu mmoja mmoja. Haiwezekani kufika hitimisho la kitakwimu kuwa na sample ya mtu mmoja.

Elimu ya diamond nafikiri kaashia olevel, sasa tuchukue population ya walioishia olevel na walisoma mpaka degree, ni upande upi una watu wengi walio-settle kimaisha na upande upi una watu wengi wanaotaabika kimaisha. Hapo ndipo unapata takwimu ya jumla
 
Na waliotoka familia masikini wakatoboa je
Ukitoka katika familia ambayo tayari ishatengeneza njia kutoboa kwako ni rahisi zaidi. Waliotoka kwenye familia masikini population yao kubwa inaishia kuwa fukara maisha yao yote sema tu story za wachache sana wanaofanikiwa kutoboa ndio huwa zinavuma
 
Embu niambie Max Mello angekua std 7
Mimi najenga hoja kwa kuangalia population ya jamii nzima
sasa tuchukue population ya walioishia olevel na walisoma mpaka degree, ni upande upi una watu wengi walio-settle kimaisha na upande upi una watu wengi wanaotaabika kimaisha
Nimekuambia wewe bado coz una fikra za kizamani.Hivi mpaka sasa unaamini kuwa ili uwe na maisha mazuri lazima uwe umesoma chuo kikuu??

Hoja yako ni dhaifu coz sasa hivi kuna population kubwa ya wasomi wa ngazi zote za elimu na hawana maisha mazuri.Umejiuliza kwa nini??

Back
Top Bottom