Kijana miaka 25-30 kwanini uendelee kukaa kwa shemeji yako? Ati kisigizio ‘unasikilizia ajira’?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
12,463
Reaction score
27,556
Kwanza sipo hapa kukubeza au kukutukana bali kukumbushana kama wanaume Tegemewa wa leo na kesho pia nataka kujua hasa uwezo wako wa akili upo kiasi gani kichwani mwako!

Ni kweli una elimu Ni kweli mfumo wetu wa Elimu una mjenga msomi kuwa tegemezi wa ajira tu hilo sipingi lakini bado haiindoi akili yako ya kuzaliwa ( common sense) ambayo tunasema kuwa ikitolewa elimu yako ya darasani yote kabisa yaani akili za a e i o u na mengine yote huo uwezo unao baki nao hiyo ndo akili yako ya kuzaliwa sasa na ndo akili ya maisha yenyewe.(Hii ni kwa uelewa wangu)

Kwahiyo ukiniambia unasikilizia ajira pasipo kujishughulisha na shughuli zingine bado nitaamini uwezo wako wa akili upo chini sana pamoja na kwamba mitihani na vyeti umefaulu kwa ufaulu mkubwa.

Kuna kisingizio cha mtaji vijana wengi husema sana sina mtaji nk. Hii point huwa napinga sana kwa sababu kijana anayesema hana mtaji lakini kwa wakati huo ana miliki simu ya 700k-1m!

Kiasi kwamba simu hiyo akiuza hawezi koswa laki4! Na njia ya kuuza simu ni rahisi sana kwa ulimwengu huu.

Nitajiwekea mfano mimi mwenyewe maana kuna nyuzi zangu nyingi sana nimejaribu kushare nanyo vitu kadhaa.

Kipindi nasoma Olevel na badae sana nikaenda veta ni kweli nilikuwa nafikia kwa dada yangu na dada yangu kwa kiasi fln alinisaidia sana kumaliza masomo ya veta au tuseme kozi kwa miaka3.

Mimi nikiwa kwa dada japo ilikuwa mjini nilikuwa nahakikisha likizo yangu iwe fupi au ndefu nafanya shuguli za kupunguza makali ya maisha pale kwa dada japo shemeji hakuwa vibaya wala dada pia alikuwa na kazi yake nzuri tu.

Moja ya vitu nilihakikisha nalima bustani ya mbogamboga hapohapo nyumbani kwa njia ya Makopo na mifuko ya cement na dada idea yangu akaipenda sana akanunua Makopo special yenye maua ya kuvutia ....

Bustani ile waliipenda sana hadi nikaanza kupata oda kutoka kwa marafiki zake wakiwemo wazungu

Majirani tuliwauzia hadi zile mbogamboga nk

Imagine mti wa miezi2 wa pilipili mwendo kasi nikawa nauza hadi 20- 35k!

Ilifika hatua likizo ikifika dada anachelewa kunitumia nauli kimakusudi ili magari ya ya kwenda kwetu yaniache ili tu nikomee kwakwe ni paboreshe kwakwe.

Baada ya kumaliza hayo masomo ya Veta moja kwa moja nikaenda nyumbani japo dada hakupenda ila niliwaza mengi sana nikikaa hapa kwa shemeji nini mataokeo yake hapo mbele?

Niliwaza mambo mengi sana ijapokuwa dada alikuwa ameniahidi kunipa mtaji baada ya muda fulani nilikubali ila nikamuomba niende kwanza nyumbani mara moja then nirudi kuishi kwakwe.

Kumbuka alikuwa ananikubali mno hata mme wake pia kwakwe nilikuwa kama mdogo wake tu mpaka leo hii.

Nilikuwa nikifika nyumbani baada ya siku 3 tu naenda kwa dada mwingine kisha namuomba anisaidie kuninunulia mbegu za chainizi na matango.

Mfano matango gram 25
Na Chinese gram 10 tu

Hizi ndo naanza nazo ambapo matango ndani ya siku50 nimeshachuma tiyari hali kadharika na Chinese cabbage.

Baada ya mavuno hayo sasa nalima nyanya huku nina kuku kadhaa nao wanataga hii ilikuwa inanipa hela muda wote.

Najua mtauliza kuhusu matunzo

Mimi nilikuwa napiga sumu tu tena ya buku4 tu hadi naivisha na matango nilikuwa sipigi zaidi ya mara2 hadi mavuno!
Mbolea samadi ya kujichotea nyumbani.

Vijana wengi wasomi nilikuwa nawapiga gape kubwa sana hadi wanaanza kuniomba hela licha ya kwamba kijijini niliwakuta wana muda mrefu tu ila akili kama hii hawakuwa nayo wao Kila mara walikuja bondeni kutafuna matango nakuepeana story fulani kaajiriwa bana fulani nae anajitolea nk

Lakini hakuna kijana aliyejaribu hata kuiga kutoka kwangu hakuna.

Kuna kipindi nililima matango nusu heka na kila Tango shambani nikawa nauza kwa 200 pc1 wao hao hao ndo tulikuwa tunsaidiana kupiga hesabu na kuchuma matango yale halafu mwisho nawapa 5000 wanafurahi sana.

Ukweli ni kwamba shemeji yako umniyima uhuru wake hawezi kaa na Boxer yake kwenye sofa ili apungwe upepo na wewe ukiwepo hawezi!

Vilevile dada yako hawezi van kanga moko kama mtengo kumtega shemeji yako mbele yako hawezi.

Una binya uhuru wao sana mkuu wapishe na ukapambane.

Nchi hii ina ardhi kubwa sana sidhani kama mzee wako kakusomesha hadi chuo kikuu au popote pale umalize then ukae nae umwambie mzee naomba 1m nikafanye kilimo nikiwa nasubiri ajira lazima kama anayo atakupa kama hana atakuambia tuitafute na atakuwezesha.

Mwaka jana nilienda morogoro kuangalia fursa za kilimo(ardhi) ukweli nilistaajabu kuona ardhi njema namna ile!

Na hapo nilihitimisha kwa kusema umasikini wa watanzania upo kwenye akili zetu na si sehemu yoyote Ile.

Mwisho nikuombe sana ujitambue na ujue tiyari wazazi wako wanahitaji msaada kutoka kwako.

Elewa kuwa miaka 30 wewe sio mtoto kuna muda dada yako anashindwa kukutimua au shemeji yako anaona akikutimua ndoa itaingia mchanga!

Umechakaza masofa ya shemeji yako maskini na huna aibu unaangalia cartoon ili wa assume wewe bado mtoto serious mkuu?

Angalia hiyo remote ulivyoichakaza hadi maandishi hayaonekani tena na unaona kawaida tu. Hapana mkuu jitambue nawewe unapaswa uwe na kwako mkuu miaka 25-30 wadogo zako wanahitaji wajifunze kutoka kwako bro.

Wanahitaji siku moja wafunge safari waje kwako kukutembelea na kucheza na watoto wako.

Wakuu sio kwamba mimi Nina maisha bora sana hapana nina uhakika wa kula tu na sivingine sina hata gari msije mkafula na mapovu hapa kunisema baada ya kujipata sasa nawaona ninyi si kitu hapana sijajipata kabisa bado na nina hasira kubwa mno ya kupambana.

Hapa tunakumbushana tu kama vijana wa leo na kesho ...

ACHA NYAYO ZAKO WADOGO ZAKO WAZIFUATE.

AHSANTE SANA KWA MUDA WAKO.
FB_IMG_1745980188220.jpg
 
Tupunguze ushauri ,duniani hapa kila mtu ndio mara ya kwanza kuja , hivyo hakuna mwenye kanuni yote ya maisha.
 
Nimeweka zangu odds 3 Kwa 100k nasikilizia apa Kwa Shem lake nikiwa na juisi ya barid😂
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Mimi nina biashara tena biashara nzuri tu ila nakaa kwa mke wa mdogo wangu. Una lipi la kuniambia kabla sijaamua kuhamishia familia yangu yote hapa ?

AHSANTE SANA KWA MUDA WAKO.View attachment 3451387
 
Back
Top Bottom