The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Wakuu, hivi mtu anatoa wapi ujasiri wa kumpiga kikatili mzazi wake wa kumzaa hadi kumuua kisa imani za kishirikina?
====
Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamshikilia Hamis Mohamed Bakari mwenye umri wa 25 ambaye ni mkulima mkazi wa kijiji cha Masiku kata ya Malingula wilaya ya Masasi mkoani hapa kwa tuhuma za mauaji ya Aidina Rashidi Milanzi mwenye umri wa miaka 56 ambaye ni mama yake mzazi.
Akizungumza na waandishi wa Habari hii leo ofisini kwake kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amesema kuwa mtuhumiwa alitekeleza kitendo hicho tarehe 18,2,2025 kwa kumpiga mama yake kichwani kwa kutumia Mwichi jambo lililo msababishia majeraha na kupelekea kifo chache, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya kamanda ni kuwa tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina.