Kijana mwenye wazo la Biashara la mtaji wa Mil 5-10

Kijana mwenye wazo la Biashara la mtaji wa Mil 5-10

Tembea uone

Nanunua carton 450,000 within a few hours nimemaliza mzigo kwa 700,000 na hapo nauza Bei ya chini Ili mzigo utoke chapchap

Ni mwendo wa kucheza na fast moving products na wholesalers only
Una kitu kama utaniruhusu naomba nikutafute PM.
 
Habari, kuna aina nyingi sana za biashara kwa mtaji wako, japo ingefika milion 15 ingependeza zaid, unaweza fungua duka la kuuza malighafi za kutengenezea chakula cha kuku, kama mashudu ya alizeti, mashudu ya pamba, damu, chokaaa, pumba nk, hii biashara inalipa na hizi bidhaa kuna baadhi unafuata mkoani nyingine zipo hapa Dar.

Biashara ya pili ni kununua nafaka mikoani na kuja kuuza Dar, hasa mahindi hii pia iko vizuri japo kwa kipindi hiki mahindi yapo juu sana lakini unaweza kuvuta subira ikifika mwezi wa 5 unaanza na mahindi ya Mtukula kwa milioni kumi inatosha kuna kipindi mahindi yanauzwa sh 600 kwa hiyo ukiwa na milioni 10 unakwenda kuchukua tani 15 - 18 na ukija kuuza unapata faida nzuri tu.

Kuna biashara ya kufungua mashine, kiukweli hii ndio biashara ya ndoto yangu, biashara hii imegawanyika makundi 3.

Unafungua mashine kwa ajili ya kusaga vipeto vya watu tu, hii kwa siku hukosi kuanzia 20-50 kutokana na eneo ulilopo lakini unawez kuwa na mashine ndogo kama SB 30 kwa ajili ya kukoboa mpunga kwa watumiaji wa chini biashara hii ni nzuri sana kwa nje ya Dar.

Biashara nyingine ni kufungua mashine ya kusaga sembe hii unaweza kufanya hapa Dar tena ukiwa na mtaji mzuuuli unachofanya unafungua mashine yako unaleta mahindi kutoka shamba unakoboa kwa mashine yako, kuna wale wasiokuwa na mashine watakuja kukoboa kwako lakini pia kama una mtaji wa kutosha unawakopesha mahindi wajasiliamali wadogo pale pale mashineni wanasaga wanauza sembe wanakulipa pesa yako.

Biashara ya tatu ni kufungua mashine ya kukoboa mpunga, hii inakuwa ya kukoboa mpunga tu, unanuna SB 50 unafunga mahali pazuuri kisha unakuwa na stoo kuuubwa ya kuhifadhia mpunga, wakulima wanaleta mpunga kwako wahifadhi kisha ukifika msimu wanakoboa, lkn pia wafanya biashara wanakuja hako kukoboa na kununua mchele hii ni nzuri sana, karibu mp boss.
Mkuu kufunga machine ya kisasa ya kikoboa mpunga na ku-grade Michele pomoja na kujenga ghara ni estimation ya mtaji kiasi gani
 
Back
Top Bottom