Kijana unayejitafuta kimaisha, katika utafutaji wako Zanzibar iweke namba moja

Ili upate fursa ya kuingia Hotel kufanya field (Training) au kazi kwa Zanzibar,

tasnia ya hotel industry Zanzibar imevamiwa na madalali (Agents) wa hizo kazi, wengi wa hao madalali wamekuwa matapeli, usipokuwa makini unapigwa kitu kizito.
Maana soko kubwa la ajira kwenye hotel wamelishika wakishirikiana na baadhi ya Ma HR na Supervior wa idara wenye tamaa.
 
Nahisi ni kweli,rafiki yangu amekaa Zanzibar miaka minne na wiki ijayo anataka kurudi akachane mbao iringa. Lakini nilimuuliza na Mimi nizamie huko hata mwaka ananipiga chenga sasa sijui anakwepa Nini? Au hataki nifanikiwe? 🤔
 
Washkaji walishanitonya kitambo Zanzibar ujenzi raia wanakamata 15 per day, Ukijikunja miezi mitatu Milioni unakuwa umeisogelea. Sema nauli ya kunitoa huku karagwe hadi Zanzibar ndio mtiti bado naitafuta.
Elfu 15 unayosema kwa mwezi ni 450,000 tu. Hiyo milioni ya kwenye karatasi hewa au cash.
 
Pole
 
Elfu 15 unayosema kwa mwezi ni 450,000 tu. Hiyo milioni ya kwenye karatasi hewa au cash.
You disappoint me. You must know how to read with comprehension, Dude. Nimeandika raia Wanakamata 15 per day Ukijikunja three months unakuwa close to million[15,000 x 90 =1,350,000] . But why is it close to 1M? It's because of the high cost of living in Zanzibar, or should I say expenses are high. And you must remember that I won’t always be working.
 
Mkuu kwa unyenyekevu mkubwa naomba uniambie ni sehemu gani Zanzibar wanalipa hichi kiasi naweza weka bondi baadhi ya vitu vya mjomba nikadandia gari hata kesho kutwa. I have to support my people at home, and where I work, I earn only 4,000 per day.
Pole sana mkuu. Zanzibar kweli kazi za vibarua mshahara unaanza 12-15k chai na chakula cha mchana unapewa. Na watu wanaotoka bara wana soko kwq sababu wanapiga kazi. Ukipata hela ukapata sehemu ukajishikiza kulala tu ambapo naona huku huwa wanashare room karibu na site. Hata hizo na kufundishwa na kupewa vyeti ni kweli kabisa.

Karibuni tujenge uchumi wa buluu. Zanzibar ni njema atakae na aje
 
upo znz sehemu gani mkuu, nina mpango wa kurudi huko ivi karibuni kusip & kuwhine kandokando ya bahari
 
Saidia fundi, mafundi 30 au 35
Okay ni hela nzuri lakini sasa kama ni mtu mgeni ndio ameenda kwa mara ya kwanza atumie mbinu gani kuzipata hizo kazi au aende mazingira ya wapi ili azipate hizo kazi au kuna kampuni maalum ndio wanachukua wafanyakazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…