Huu ni ukweli mtupu, miaka ya nyuma mimi binafsi niliamua kujichanganya Zanzibar kwa jamaa yangu alie kuwa ana sukuma kazi za ujenzi. Akaniunganisha tukawa tunapiga pamoja, ila ile kazi nilifanya kwa muda mchache nikatafuta connection ya hotelini. Nikapata hoteli moja iko Nungwi pale nikaingia kama mwanafunzi (trainee) na nilikuwa kitengo cha Muhudumu awali nilienda kwa lengo la kuwa Bar Man ila nilikuta nafasi zimejaa, hivyo nikaona kuliko kukosa ngoja nikomae hapo hapo.
Nikapiga trainee miezi 4, faida niliyo pata hapa nilivyo maliza na msimu wa high season ndio ulikuwa unaingia. Hoteli hiyo hiyo ikanipa ajira na mshahara ulikuwa 350k kwa mwezi, usafiri kwenda na kurudi pamoja na chakula ukiwa kazini hoteli inatoa vyote bure kabisa. Na uzuri zaidi kwa kitengo nilicho kuwepo nilikuwa napata sana tip kutoka kwa wageni, kwa mwezi tu nilikuwa sikosi angalau 200k hiyo nje ya mshahara. Hiyo hela ilikuwa inapiga tafu kwenye masuala ya kulipia chumba maana staff wengi walikuwa wanakaa mjini ndio maana hoteli ilikuwa inatoa usafiri.
Kwa namna hiyo nilikuwa na uwezo wa kuto gusa mshahara wangu, maana kula ilikuwa tunakula pale pale hotelini mara moja moja sana nilikuwa napika geto. Kwa hiyo huyu jamaa anacho sema ni sahihi kabisa, huenda tu jamaa hajafunguka zaidi ili watu waelewe vizuri. Nimetoa huo mfano wangu ili kila mmoja aelewe mambo yanavyo enda. Chukulia huo mfano kwa kijana unae jitafuta uamue ku focus na maisha kweli na uwe na malengo, ukiamua kutunza hiyo 350k ndani ya miaka mitatu utakuwa umetengeneza pesa nzuri sana. Pesa ambayo unaweza toka na kuamua kujiajiri wewe mwenyewe.
Mwezi wa sita kazi za hoteli huwa nyingi sana kwa hiyo mnaweza jichanganya. Kingine nacho weza kusema Zanzibar ukiwa mzuri kwenye kuongea na kuandika kwa ufasaha angalau lugha ya Kiingereza ni bingo sana. Kupata kazi ni rahisi sana hasa receptionist, utapiga trainee yako baada ya hapo unapata ajira unaanza kula mshahara wa 600k. Sasa kuliko kukaa tu unaweza tafuta mwalimu mzuri akufunze hiyo lugha, jipe muda wa kujifunza kisha zama Zanzibar.