Upo sahihi Kama mumeokotana na hampendani.
Na hamjui nini maana ya Familia.
Siku zote familia yenye mfumo uliousema kamwe haiwezi kuendelea.
Hiyo ni Familia yenye ubinafsi, na kwenye ubinafsi kuna unyanyasaji.
Unakuta mume anamnyanyasa mke kisa Mke Hana kipato, au kisa mume ndiye analisha familia. Halikadhalika na Mke naye anamnyanyasa mume kisa Hana kipato na yeye ndiye analisha familia.
Msingi Mkuu wa ndoa ni Upendo na wala sio pesa.
Ushauri wako ni mzuri Kutokana na Dunia ya sasa ilivyo, wanawake ni selfish Kwa watu wasiowapenda. Hilo ulizingatie Sana.
Pesa zako hazimfanyi mwanamke akupende, hilo pia uliweke akilini.
Na Mwanamke lazima Ajue uzuri wake na kujitoa kwake hakumfanyi mwanaume akupende.
Upendo WA kweli hautengenezwi.
Kuupata upendo wa kweli ndio kipengele.
Na hapo ndipo mtoa mada hoja yake inapopata nguvu