Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,384
- 3,926
Usitumie nguvu kubwa sana katika kumtongoza mwanamke, unaweza ukamkosa ukapoteza mda wako. Ila unaweza ukampata ukapoteza mda na pesa zako.
Usimtongoze mwanamke kwa mategemeo ya kumbadilisha ni kweli wapo wanawake ambao wanabadilishika ila kama mwanaume usifanye hiyo kazi utapoteza mda wako.
Kumbuka wewe ni tegemeo la baadae kwa watoto wako na ndugu zako. Muda unaotumia kujaribu kumbadilisha mtu ni vizuri ukautumia kujijengea future yako.
Kwa maana usitegemee kivuli kilicho nyooka kwenye mti uliopinda na usijione upo smart sana kichwani kwa kucheza na mwanamke kwa kujidanganya wanawake ni dhaifu. Wana akili na unachokifikiria na wao wanakifikilia hivyo ila wanachokifanyaga ni kutest akili yako kila mda.
Vitabu vya dini vinasisitiza kuishi kwa akili kwa sababu hawa viumbe wanamajaribu mengi sana. Hivyo basi katika majaribu yake kwako kama ukimshitukia atakuomba msamaha ila kama haujamshtukia hiyo itakuwa imekula kwako.
Vijana wa kiume kama unahisi utatumia nguvu kubwa sana kwa mwanamke kama haujamtongoza basi nashauri usimtongoze. Maana atakuja kukuendesha kiasi utapotea wewe na yeye pia atapotea.
Ila kama upo nae kwenye mahusiano we pambana naye, muombe Mungu tu huyo mwanamke asikutoe roho. Na kama unahitaji kuoa, basi hakikisha unaoa mwanamke ambae kwao chai mwanakunywa saa 6 kama wewe wa kiume kwenu chai mnakunywa saa 4.
Usije ukoa mwanamke ambae kwao chai mwanakunywa saa 2. Huyo siku ukikosa hakuelewi na pia haelewi maana ya kukosa. Lakini ukimuoa mwanamke huyo ndoa yenu kudumu kinachobaki zaidi ya hapo ukijikoroga tegemea tu neema za Mungu na upepo wa kisulisuli ufanye maajabu yake.
Maneno yangu kwa leo ndio hayo.