Kijana wa miaka 29 sina kazi, sina mpenzi ila ninaishi

Pole sana Chief tusione aibu kuongea changamoto zetu jua tu you're not alone. Jitume tu ipo siku itaeleweka
 
Huo ushauri wako wa upande wa pili huo! Mhhh!!! Naona kama ndio utammaliza kabisa.
 
ila watu walio pata wanafikiri kila mtu atafanikiwa kwa njia aliyopita yy.
nakumbuka jamaa yangu mmoja anakwambia dogo kuku wanalipia ukianza na watano tu nikawa nawaza ss tuko kweny nyumba za kupanga uswahilini unafuga wapi ukiforce kwa eneo ulipo utakua umewapa watu kitoweo
unajitoa kweny vikazi vidogo hela unayopata nauli na kula mchana imeisha hapo bado haujaumwa unatakiwa uende hospital
unasema ukatafute ata pikipiki hamna boss anakuamini akupe chombo
kikubwa ni kua na jamii hasi sio wazazi hadi majirani ndio sababu watu wanajinyonga
vijana wanapitia mengi sn alafu unakuta mtu ana generalaz et vijana ni wavivu na wanaaibu
kubwa sio kukata tamaa na kingine utafutaji kwa sehemu uliyo zaliwa na kukuliwa kunachangamoto sn jamii inakua hasi sn bora kutoka kwenda sehemu nying ukaanze upya kwakwel.
 
Maisha Sio ABC maisha ni sentensi nzima haina formula kua utaanza na alfabeti gani
 
Nakumbuka miaka kama 7 iliyopita...nilikua machimbon huko nafadhili mashimo ya uchimbaj...nimekaa karib miez sita sijaona jiwe la manaa sanasana vijiwe vya elf 50 etc..hapo mtaj alionipa mzee umekata..kurud home naona aibu maana nilipewa hela ya mtaj. Umekwenda na maj..bas kuna muda tumechiimba wee ikafika jion kama sa kumi na moja hiv..tukawa ndo tunafunga tuondoke kwenda camp...dah..nikasogea pemben nkaanza mwaga michoz..vijana wangu wa kaz wanasema boss vip tena..unaumwA..ikabid nizuge najisikia vibaya sana ..kumbe nalia uchungu maisha yamekwama.no hope...bas tukaondoka..usiku nilisema mim si mtu wa kumwomba mungu leo ngoja niongee na mungu..bas nkaongea na mungu navojua mm kisela sela. Nkalala..usiku niliota ndoto ya ajab sana...siwez ihadithia muda mchache...ila huwez amin kesho yake tunaanza chimba tu..haikupita masaa mawil..tukapata jiwe ambalo tuliuza 16m...namii ndo shugul yangu ya uchimbaj iliishia hapo...sikurud tena had leo.na nmeendelea na maisha mengne....so amin nakwambia..unapofika muda kama huo...ongea na Mungu wako wa kwel aliekuumba wew..yaan sema..mungu ulieniumba mim...usikarir sjui mungu wa mtume nan.sjui mungu wa dheheb gan...sjui din gan..ukristo uisilam..we sema mungu aliekuumba wew hapo..atakuskia .
 
Hakika Mungu ni mwema kaka
 
Kama ipo ipo tu jamaa wa KFC katoboa maisha akiwa na miaka 62 wewe ni nani unalalamika ata nusu ya miaka hujafika.
Katoboa dakika za majeruhi [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Insparations mkuu
 
[emoji16][emoji16]bahat yako kazi za machimbo zile n kama kucheza kamari
Kuna jamaa aliwahi kupiga Kama 2B akaenda bungeni kuaga umaskini ila badae alifilisika kabisa baada ya kurudsha hela huko na mwaka jna kafarik ikakosekana hta hela ya kumrudisha kwao akazikwa kimya kimya
 
Mkuu halafu huyo dada ahudumiwe na nan,mtoto alelewe kwa msaada wa nan? Nafikiri mtoa mada yupo sahihi,chamsingi ni kuendelea kupambana kadiri ya uwezo wake,na swala la mahusiano lina nafasi kubwa ya kuamua uwe na furaha au huzuni,vijana tunashauriwa kujipanga kwanza yani tuhakikishe tupo imara kiuchumi na kiroho ili kuwa vichwa bora wa familia,na swala la uchumi sio mpaka awe tajiri ila uhakika wa mahtaj ya msingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…