Kijana wa Uingereza kaliza watu mamilioni ya Pauni kupitia Forex

Kijana wa Uingereza kaliza watu mamilioni ya Pauni kupitia Forex

The Mongolian Savage

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
8,082
Reaction score
17,838
Mzuqa wanajamvi!

Kijana mdogo 'Ontario wa Uingereza' mwenye miaka 20 Garvin Singh mwanachuo Uingereza anayesomea udaktari kaliza watu zaidi ya pauni za uingereza million 3 kwenye Forex aliyoianzisha kwenye Instagram na WhatsApp.
23044904-7856121-image-a-11_1578332140064.jpg

Dogo huyo aliyeanzisha Forex yake kwenye Instagram na WhatsApp na kukamata njemba (traders) zaidi ya1000 na kuwaingiza chaka aliingia na gia ya 'get rich quick'.
23044896-7856121-image-a-17_1578332202311 (1).jpg

Inaaminika Dogo Garvin Singh aliweza kuwashawishi njemba kama 1250 kujiunga kwenye Forex yake hivi kwa picha alizopiga akiwa kwenye Ferari na private jet na maisha yake ya anasa na kusafisha account zao usiku wa kuamkia krismasi 2019.
23044902-7856121-image-a-23_1578332256848.jpg

Dogo alipoanzisha aliwaaminisha kuwapanga na kuwaahidi Forex yake ni halali imesajiliwa na watakuwa wanatoa pauni 300 kwa siku iyo ni faida. Na kweli ikawa hivyo kwanivmambo yalienda vizuri sana kwa miezi wakawa wanapata faida na wengi wakawashawishi wengine kujiunga.

Ila ghafla baadaye mambo yakaanza kuharibika nakuona hela kwenye account zao zikipungua.

Lakini dogo akawapooza na kutoa visingizio kuwaambia mambo yatakuja kuwa freshi hadi march mwaka huu hii ni kwasababu ya Brexit.

Lakini ilipofika usiku wa kuamkia krismasi traders wakakuta account zao sifuri na dogo kukata mawasiliano kabisa.
21253024-7856121-MailOnline_has_been_in_contact_with_dozens_of_young_people_who_c-a-12_1578559...jpg

Dogo akakomba zaidi ya pauni million 3.5 za watu ambao wengi wao ni miaka 18-25 waliodai wamepteza maelfu ya pauni hela za familia, walizokopa na student loan.

Ikumbukwe pia sisi tulikuwa na Ontario wetu naye aliingia humuhumu Jamvini na kuuliza watu kwenye Forex na kuwaingiza chaka.

Siyo vizuri kuwachukulia watu hela zao kitapeli na kujifanya mjanja.

Pia ina huzunisha Mwanaume kumkabidhi mwanamme mwengine hela zako kiulainii na kwa hiari.

Tuweni makini sana kwenye hela zetu.

Soma zaidi hapa chini:

Hahahhah! Mimi watu wa namna hii nawapenda! Msemo wa waingereza unasema: "usipofanya wewe mwingine atafanya".
Watu wanataka utajiri wa haraka! Usipozichomoa hela kwao wewe mwingine atawachomoa! So, what is the difference? Kama kuibiwa sijui kutapeliwa whatever the case sikio la kufa halisikii dawa!
 
Safi sana,dogo amefanya jambo la maana sana piga hela za wajinga.

Mimi nikishaanza kuona mtu anapiga piga ma picha kwny mahotel ya bei ghali,ma gari ya mamilioni na mambo ya dizaini hio najua tu huyu ni tapeli(na hio ndio sifa kuu za matapeli).

dodge
 
Kijana mdogo mwenye miaka 20 Garvin Singh mwanachuo Uingereza anayesomea udaktari kaliza watu zaidi ya pauni za uingereza million 3 kwenye Forex aliyoianzisha kwenye Instagram na WhatsApp.
UJINGA NI MZIGO. Inakuaje unampa mtu ela zako?

Mimi nadhani wanastahili kupigwa hakuna namna! Hawa ni wavivu wasiopenda kujitegemea na kujifunza ili wa-trade independently!
 
Safi sana,dogo amefanya jambo la maana sana piga hela za wajinga.

Mimi nikishaanza kuona mtu anapiga piga ma picha kwny mahotel ya bei ghali,ma gari ya mamilioni na mambo ya dizaini hio najua tu huyu ni tapeli(na hio ndio sifa kuu za matapeli).

dodge
Kwa hiyo mama/mke/shangazi/baba ako akiwa mapumziko akipiga picha za kumbukumbu kwenye hoteli za bei ghali na yeye utamuita tapeli?
 
Safi sana,dogo amefanya jambo la maana sana piga hela za wajinga.

Mimi nikishaanza kuona mtu anapiga piga ma picha kwny mahotel ya bei ghali,ma gari ya mamilioni na mambo ya dizaini hio najua tu huyu ni tapeli(na hio ndio sifa kuu za matapeli).

dodge
Acheni wivu mtu kama tajiri wacha ale bata kama Irene Owoya anamiliki hotel 5 star (Kempinski na Mt. Meru) sasa akipiga picha kwenye mali zake anakuaje tapeli?
 
Hao walioliwa pesa zao si wakaroge mbona humu naona Kuna uzi ule wa kichawi watu wanatafunwa mpaka maskio! Hlf wanaibiwa ma pound huko wanaenda kusema kwenye media hawajitendei haki waende sehemu sahihi tuone watu wanavyokuwa vibogoyo na TOINYO😂
 
Atapukutishwa na polisi zotee na kuwa deported kwao akiwa hana hata cheti alichokifata kwa malkia ikiwa sio raia wa nchi hiyo kama ni raia basi atabaki hana hata mia
Wampukutishe tu,lkn nafurahi sana kuona maboya wanapigwa kweli kweli.

dodge
 
Acheni wivu mtu kama tajiri wacha ale bata kama Irene Owoya anamiliki hotel 5 star (Kempinski na Mt. Meru) sasa akipiga picha kwenye mali zake anakuaje tapeli?
Hahah usisahau hata Yule demu msanii(Tunda Mahoteli) ana 'miliki' mahoteli mengi tu hapa Town.

dodge
 
Back
Top Bottom