Kijana wangu anakesha kwenye games analala alfajiri

Kijana wangu anakesha kwenye games analala alfajiri

Hapa nilipo nimetoka kucheza game la mbio za magari.. muache wala usi msumbue.. ulitaka afanyaje sasa ? Yeye kaona game ni sehemu nzuri zaidi.. au unataka akachangamane na wakulungwa waanze mfundisha mambo machafu 😡😡
 
Mwaka wa pili mbona mkubwa huyo.Ila hawa watoto wa familia zenye uwezo huwa wanachelewa kukomaa kifikra.
Ila kagemu katamu nakumbuka mimi enzi hizo nilikuwa natoroka kanisani naenda kucheza gemu na marafiki zangu.Nakumbuka siku hiyo wazazi wetu waliamua kutufungia kazi nafikiri baada ya kututafuta kanisani na kutukosa.Sisi tumemaliza kilichotupeleka tukawa tunarudi kanisani japo mimi nilikuwa naenda kwa tahadhari sana maana Bi'mkubwa akichukia namfahamu.Hiyo njia ilikuwa ni mteremko halafu nilikuwa nina njaa kweli kwa hiyo nikawa nashuka kinyonge.Ile tumefika kona fulani hivi nikaona rangi ya nguo ya mama sura sikuiona ila sikuelewa nguvu niliipatia wapi maana nilipandisha ule mwinuko kama bajaji.Yaani kitendo cha hao wazazi wengine kuonana na watoto wao mimi tayari nishapotea mazingira yale.Mzazi wangu akarudi kapa ila wengine wakawapata wabaya wao. Nikategeshea muda wa kutoka kanisani ufike ndipo nikarudi.Katoka akanikuta nje,swali la kwanza ulikuwa wapi? Nikajibu ndani.Mbona nimekutafuta sijakuona? Nikamwambia hata yeye sikumuona.Walifundisha nini? Nikaanza kumhadithia vipindi vya toka asubuhi hadi pale nilipotoroka.Naye hakuchunguza sana akakubali.Nikaponea chupuchupu siku hiyo.
Ila kuna wakati haya madude utayacheza sababu ya mizuka tu ila kuna muda utafika utayachoka na kuanza kuwaza mambo mengine maana muda haukusubiri.Kama mimi sikumbuki ni lini nimeshika gemu kucheza japo ninalo.Naye atafikia hiyo hatua muda si mrefu halafu uzuri ni mtu mzima.Angekuwa mtoto hiyo ndo ingekuwa tabu.
 
Sasa kama mamaake unakesha jf kuendekeza siasa na kuwatetea kina Mbowe unategemea uwape watoto wako malezi bora kweli?

Na uhakika hapo ulipo wewe ni single maza, maana hakuna mwanaume atakubali kukaa na mwanamke anaekesha kuwatetea kina humu jf!

Tulia wewe MATAGA kila sehemu ni siasa. Buku 7 zinakutoa akili.
 
Unajua nmerudia kusoma tena! Hii tanzania aisee! Yani mtu mzima kabisa wa chuo mwaka wa pili bado anahitaji maelekezo ya wazazi? Wakati sisi wengine wakati kama huo tuko kitaa tunajitegemea!

Hebu pata picha wazazi wakifariki hilo toto litakuwa na maisha ya namna gani kama siyo kuwa shoga?
 
Kama Games hazimletei madhara katika Taaluma,tafadhali mfahamishe umuhimu wa kupumzisha Ubongo..
Ila usitumie nguvu nyingi kumkataza pia usiache kumkataza.
 
Mshukuru Mungu sana kwa mtoto ulie nae,Mshukuru mno.

Niishie hapo tu...
 
Maendeleo yake kielimu chuoni yakoje? Kama maendeleo ni mazuri basi huo ni wasiwasi wako.

Shida ipo hapa! Inakuaje mtu mwenye umri wa chuo unamnunulia play stations kama zawadi? Na yeye anapokea? Hayo mambo ya watoto wa miaka 10. Acheze ila anunue kwa pesa yake.
 
Bora anacheza gemu, angejiunga Lumumba angekuwa anashinda humu anapambana na makamanda..
- GPA yake inasomaje?
-Umemtengenezea mfumo wa kuwa na majukumu ndani ya siku yake ?
-Ana aina gani za marafiki ?
Huyo mlimdekeza toka akiwa mdogo, samaki mkunje angali mbichi ila mtoto hakui kwa wazazi wake. Lazima muanze kumpa majukumu hata kukata majani ya ng'ombe au kusimamia shughuli za kilimo au biashara kama mnazo. Tatizo mnemzawadia mengi kuliko mazuri aliyoyafanya, mwisho wa siku mkiendelea kubembeleza hivi atakuwa ni mzigo tu kwenu.
 
Ana girlfriend? Akimpata basi itabidi uongee na girlfriend wake wawe wanatoka kutembea tembea, automatically dogo ataacha kucheza games.
 
Mkuu tabia hizo unazosemannadhan ziko applicable kwa wenzetu .. dunia ya 3huku mbona Kama unakuwa mtumwa tu..!unajikuta unalost

Mkuu ndiyo mtazamo wa vijana wa wakati huu huo. Hii haiepukiki kwasababu vision, dreams na matamanio yao ni tofauti sana na ya wazazi.

Hapa nazungumzia vijana wanaotoka familia “upper middle class” kwa Tz standards.

Hapa Arusha most youths are like this. They spend most of time on the Internet. They dream big, very BIG. Unaweza dhani wamechanganyikiwa. But who are you to stop them from dreaming big and go after what they love most in life?

Kuwafanya wafanikiwe ni kuwa-support zaidi kama uwezo upo kwasababu vinginevyo utaanzisha migogoro.....atapata depression na hato kusikiliza tena hata ufanye nini.

Huyo Sky azidi tu kwenda naye fair kwasababu inaonyesha ndiyo life style yao hapo home.
 
Tulia wewe MATAGA kila sehemu ni siasa. Buku 7 zinakutoa akili.
Ameniudhi sana! Huwa namuona humu akichambua mambo nafikiri ana akili kukbe zero, ameshindwa hata malezi,

Kijana wa mwaka wa pili chuoni anahitaji maelekezo ya wazazi juu ya maisha yake kweli?

Hivi siku hao wazazi wakatoweka ghafla duniani hilo likijana unategemea litakuwa na maisha ya namna gani?

Yani hilo utakuta hata nguo linafuliwa
 
Sehemu zote mbili anaweza kupata maisha (Future) au kupoteza baina ya moja au zote, endapo ni yupo multi basi Games ni future nzuri sana kwake.

Kama akiwa na kazi yenye kuingiza millioni 10 kwa mwezi au kusaidia jamii kuondoka na umaskini na hali duni ya fikra kwa asilimia 0.7 kwa mwezi ni sawa anaweza kuingiza millioni 30 kwa mwezi kutokana na games.

Kama yupo vizuri sana kwa games, fanya investment kubwa na ataweza kutengeneza maisha (ya pesa) vizuri.
 
Bora anacheza gemu, angejiunga Lumumba angekuwa anashinda humu anapambana na makamanda..
- GPA yake inasomaje?
-Umemtengenezea mfumo wa kuwa na majukumu ndani ya siku yake ?
-Ana aina gani za marafiki ?
Huyo mlimdekeza toka akiwa mdogo, samaki mkunje angali mbichi ila mtoto hakui kwa wazazi wake. Lazima muanze kumpa majukumu hata kukata majani ya ng'ombe au kusimamia shughuli za kilimo au biashara kama mnazo. Tatizo mnemzawadia mengi kuliko mazuri aliyoyafanya, mwisho wa siku mkiendelea kubembeleza hivi atakuwa ni mzigo tu kwenu.
Sasa si unaona mamaake anashinda humu kupambana na lumumba kumbe nyumbani kwake malezi yanaenda kombo
 
Back
Top Bottom