Nikiwa kama mzazi, nililea watoto kwa msaada wa dada huku nikiwa na majukumu mengine. Mtoto wangu wa kiume alipenda gadgets na kila siku yake ya kuzaliwa alichagua game au play station mpya. Kwakua alikuwa na bodi shuleni niliona hii ni kama asante yake ya kuitendea vyema ada tunayolipa na Baba yake.
Sasa yuko chuo anaingia mwaka wa pili. Chuo chao kilifungwa tangu March mwaka huu kwaajili ya corona lakini walipata online lectures na walituma kazi zao huko huko online.
Tangu aache kwenda chuo amekuwa ni mtu wa kujifungia chumbani kwake tu. Nilitumia nafasi hii kumlipia mafunzo ya udereva. Hii ilimhamasisha alikuwa na hamu ya kujua kuendesha gari. Tangu apate leseni amerudia tabia zake za zamani.
Mtoto anakesha kwenye michezo mpaka asubuhi. Huyu atakua raia wa aina gani? Ana miezi miwili ya kukaa nyumbani mpaka September atakapo rudi chuoni. Siku nifanye nini kukomesha hii tabia?
Wewe si unalea kizungu aya sawa endelea kwamba kila anachotaka unampa.
Kuna kipindi kwenye Maisha inabidi ubadilike na kuwa mkali kuna vitu inabidi umfunze kua ni hapana ata kama ni ndio sasa.
Games sio mbaya ila utumiaji wa kupindukia ndio mbaya nakumbuka kipindi niko primary nlikua nkitoka shule nakuta wameishakula wameniachia vyombo vya kuosha nyumba nzima nakula chakula changu naosha vyombo vyote ndipo naenda kucheza nlikua naumia naona nateswa but nimekuja jua Shangazi alikua ananipenda sana yani nlikua nkiomba kitu napewa ila kama hana uwezo anasema hiki sina na hiki sitaki mfano ntacheza nje ila saa moja jioni shart niwe ndani kinyume na apo ni fimbo displine hii ilinijenga mpk najitegemea nikitoka kazini kipindi nipo mkoa ni straight nyumbani sina kona sijui bar, sijui kwenye mpira nkitaka kunywa nanunua naenda kunywa nyumbani.
Mtoto anafundishwa kwa njia tofauti tofauti ata mbaya ili kitu kimwingie sasa kama kijana amekua mtu mzima ivyo jua kuna vitu apo
1. Kashajua yeye ni mkubwa so kuna kibri ( kashabarehe)
2. Mentality yake inamwambia ata wafanyeje hawawezi nipiga mimi si mtu mzima watasema wee Wataacha
3.Ninapendwa na Mama na Baba so mimi ni Tunda lao zuri sasa hapa ndio inawafanya wafanye chochote
Mwisho nakwambia umeongea wee umeona haifai sasa njia ni mbili tu kibongo bongo sisi tulikua tukizingua tu si atuskii tunapelekwa polisi ata masaa 3 tu unakaa pale kituoni unaona machungu yake ukitoka umenyooka
Option ya pili ni kusubiri ametoka chumbani au ameenda matbezi wewe ingia chumbani kwake toa takataka zote za games fungia stoo kaa na funguo akirudi akute azipo atajiongeza na badala ya kutoa games jitahid umtafutie ata books nzuri za stories atleast awe anasoma na wewe unakaa nae mna discuss aya ndio malezi.
una muuliza challenges zake anazopata mfano mimi mpk namaliza chuo Aunt yangu hakuwai niskia na ukaribu na mwanamke mpka akaniuliza tukakaa alikua na lengo la kunisaidia kwa kua alihisi ninatatizo but alipokuja jua kua mimi si mtu wa high profile akajua niko njema na ninamshukuru kwa ilo.
Maisha ni kupanga Dada angu sometimes ulezi wa kizungu ni mzuri ila unamadhara yake na wa kibongo au kiafrica unamadhara yake so jaribu kubalance.
Sisi ambao tulilelewa na Ndugu Mashangazi tukiwa na miaka 2 mpk leo hii watu na ndevu tunajua kabisa hapa tulipitishwa kwenye moto na tunawashukuru sana waliotulie.