Kijana wangu, ana miaka 20 kwa sasa, yuko chuo anamaliza mwaka wa kwanza, tangu alipomaliza kidato cha sita kawa mtu wa hasira sana, akikosea kitu ukimuonya hataki kabisa kusikiliza, badala yake ataanza kuongea kuonesha hakubaliani na baada ya hapo ananuna haongei na mtu hata siku 3.
Hali hii imekuwa kero sana kwa familia yetu kwani akiwa katika hali hiyo, kila anayemsemesha anamjibu kwa sauti ya kufoka, anapenda kukaa peke yake, anakuwa busy tu na simu yake na si watu wa familia yake, na ikifika wakati wa chakula hajumuiki na wengine anakula kwa wakati wake mwenyewe.
Kuna muda natamani hata likizo iishe arudi chuo nisimuone kabisa kwani kawa simba ndani ya nyumba yangu mwenyewe, kuna muda natamani kumkata makonde ila najizuia, sijui kapatwa na nini.
Je, nifanyeje kumsaidia aache tabia hii ambayo katika makuzi yake hakua nayo, kwa sasa ni mtu mzima siwezi hata kusema nitatumia fimbo.