Mwaka wa Mbele
JF-Expert Member
- Mar 5, 2026
- 1,013
- 3,017
Kijana wangu, ana miaka 20 kwa sasa, yuko chuo anamaliza mwaka wa kwanza, tangu alipomaliza kidato cha sita kawa mtu wa hasira sana, akikosea kitu ukimuonya hataki kabisa kusikiliza, badala yake ataanza kuongea kuonesha hakubaliani na baada ya hapo ananuna haongei na mtu hata siku 3.
Hali hii imekuwa kero sana kwa familia yetu kwani akiwa katika hali hiyo, kila anayemsemesha anamjibu kwa sauti ya kufoka, anapenda kukaa peke yake, anakuwa busy tu na simu yake na si watu wa familia yake, na ikifika wakati wa chakula hajumuiki na wengine anakula kwa wakati wake mwenyewe.
Kuna muda natamani hata likizo iishe arudi chuo nisimuone kabisa kwani kawa simba ndani ya nyumba yangu mwenyewe, kuna muda natamani kumkata makonde ila najizuia, sijui kapatwa na nini.
Je, nifanyeje kumsaidia aache tabia hii ambayo katika makuzi yake hakua nayo, kwa sasa ni mtu mzima siwezi hata kusema nitatumia fimbo.
Ni tabia za kurithi.
Kaka yangu kabisa wa Damu yuko hivyo. Akiwa na 8 yrs alisusa na hakutaka kuongea na mtu kwa siku 3. Hadi chakula cha usiku ile kujumuika pamoja alikataa.
Sasa ni mtu mzima. Aisee. tunajuta kuwa wadogo zake.
Ashaachana na wanawake 3. Mmoja wa ndoa kanisani. Wawili amezaa na kukaa nao kama mke..Na hapo bado Hajafika 40 yrs.
tena Huyo jamaa akipata hela na kuwa na familia yake atawasumbua sana.
Hana utu na atawatesa sana wanawake.
Ni mtu anayejiona kuwa yeye yuko sahihi. Na hatakiwi mtu mwingine kumkosea.
Kupatana nae ni kumfanya yeye ajione yuko sawa (hakosei kitu) na kumnyenyekea.
Kama amezaliwa katikati ya May 20 - June 23.
Basi ndio kabisa. Kisukari ni +++.
Kazi mnayo Kamanda.