Kijana wangu hataki kuonywa akikosea, ananuna haongei na mtu hata siku 3

Ni tabia za kurithi.
Kaka yangu kabisa wa Damu yuko hivyo. Akiwa na 8 yrs alisusa na hakutaka kuongea na mtu kwa siku 3. Hadi chakula cha usiku ile kujumuika pamoja alikataa.

Sasa ni mtu mzima. Aisee. tunajuta kuwa wadogo zake.
Ashaachana na wanawake 3. Mmoja wa ndoa kanisani. Wawili amezaa na kukaa nao kama mke..Na hapo bado Hajafika 40 yrs.

tena Huyo jamaa akipata hela na kuwa na familia yake atawasumbua sana.
Hana utu na atawatesa sana wanawake.

Ni mtu anayejiona kuwa yeye yuko sahihi. Na hatakiwi mtu mwingine kumkosea.

Kupatana nae ni kumfanya yeye ajione yuko sawa (hakosei kitu) na kumnyenyekea.

Kama amezaliwa katikati ya May 20 - June 23.
Basi ndio kabisa. Kisukari ni +++.

Kazi mnayo Kamanda.
😂😂😂😂
 
Wewe ni dingi yake kuna sehemu umeteleza toka awali, sasa hii balehe yake inampeleka puta, muite uongee nae kikubwa, ukishindwa mlete kwetu tumfunze adabu..

Kama dingi uko fiti. Akileta ujinga siku mveshe gloves, mpigane, ukishamkanda umueleze kwenye nyumba hiyo mwanaume ni mmoja tu ambae ni wewe, unafanya wale, yeye asome, sasa asilete mambo ya kisemge akotaka ubabe atafute kwake, kwako ni kauli ya mwanaume mmoja tu ndio inazungumza..... hapo kihuni,
Ila kisaikolojia pia inawezekana
Je km baba hana uwezo au nguvu za kushindana na Dogo?
 
Hiyo ni hali ambayo isipofanyiwa kazi inaota mizizi na kuwa tabia mbaya sana in the future, mkuu naomba ifanyie kazi utibu huo ugonjwa wa kijana wako maana atakuwa baba na mume sio mda mrefu sana.

Tuna workmate mwenye tabia hiyo, wallah sijawahi kuona, as I'm writing ana mwezi mzima hana engagement yoyote na staff yoyote, imagine hata salam, usipomsalimia hasalimii mtu, ukihitaji kitu hakupi maana ameweka barrier moja kubwa sana kati yake na wenzake. Watu wanajiuliza kosa gani amefanyiwa hakuna anayejua, amefatwa once kuulizwa ndio amezidi kununa, eeh Mungu mwanaume wa hivi sijawahi kumuona.

Rekebisha hiyo tabia kabla haijawa ugonjwa mkuu!!
 
Kijana wangu, ana miaka 20 kwa sasa, yuko chuo anamaliza mwaka wa kwanza, tangu alipomaliza kidato cha sita kawa mtu wa hasira sana, akikosea kitu ukimuonya hataki kabisa kusikiliza, badala yake ataanza kuongea kuonesha hakubaliani na baada ya hapo ananuna haongei na mtu hata siku 3.

Hali hii imekuwa kero sana kwa familia yetu kwani akiwa katika hali hiyo, kila anayemsemesha anamjibu kwa sauti ya kufoka, anapenda kukaa peke yake, anakuwa busy tu na simu yake na si watu wa familia yake, na ikifika wakati wa chakula hajumuiki na wengine anakula kwa wakati wake mwenyewe.

Kuna muda natamani hata likizo iishe arudi chuo nisimuone kabisa kwani kawa simba ndani ya nyumba yangu mwenyewe, kuna muda natamani kumkata makonde ila najizuia, sijui kapatwa na nini.

Je, nifanyeje kumsaidia aache tabia hii ambayo katika makuzi yake hakua nayo, kwa sasa ni mtu mzima siwezi hata kusema nitatumia fimbo.
Mikeka haiendi sawa.
Kazi ngumu sana kugeuza Rim paper kuwa Hela.

Shule tulikuwa tukikosea tunapigwa maana yake tulifunzwa kukataa makosa na tahia hii wengi wanayo ila wako kaamua kiwa 2pac kabisa akija mchanganyiko na Mamba 24.
 
wa kike au kiume? kama ni wa kiume, toka nae out, seheme fulani hivi amazing ongea nae kama baba, mzazi wake kwa upole but ukiwa serious, beba hatima yake kwenye utawala wako. Mwambie ukweli juu ya tabia yake, akileta mbwembwe mzabue intact double, go & return. Mpe na onyo..... karipio kali, achague kuwa na adabu au kupotelea huko shule.....mfuatilie na marafiki zake.... pole kwa changamoto
Uzi uishie hapa umenena vyema
 
Hiyo ni hali ambayo isipofanyiwa kazi inaota mizizi na kuwa tabia mbaya sana in the future, mkuu naomba ifanyie kazi utibu huo ugonjwa wa kijana wako maana atakuwa baba na mume sio mda mrefu sana.

Tuna workmate mwenye tabia hiyo, wallah sijawahi kuona, as I'm writing ana mwezi mzima hana engagement yoyote na staff yoyote, imagine hata salam, usipomsalimia hasalimii mtu, ukihitaji kitu hakupi maana ameweka barrier moja kubwa sana kati yake na wenzake. Watu wanajiuliza kosa gani amefanyiwa hakuna anayejua, amefatwa once kuulizwa ndio amezidi kununa, eeh Mungu mwanaume wa hivi sijawahi kumuona.

Rekebisha hiyo tabia kabla haijawa ugonjwa mkuu!!
Kwani kusalimia lazima? Au kuwa na engagement na staff wenzio? Anaepusha mengi, kwanza yuko sahihi mazoea ya kiwaki kazini ya nini?
Muhimu anafanya kazi yake vizuri na kwa weledi basi, hayo mengine hayawahusu, punguzeni kufatilia ya watu. Woiiiih
 
Kumwambia unakula bure sio sahihi kwasababu umemzaa wewe ila hakupaswa kukujibu hivyo!
 
Huyo inabidi apuuzwe muda wa msosi ukifika mkimuita mara moja imetosha na msibakizie chakula asipopiga simu hakuna mkupigia lakini kama atakuwa ananuna kidogo tu halafu mnamnyenyekea atawapanda kichwani
Mjomba mnoko kwenye ubora wako..!! 😹
 
Wewe ni dingi yake kuna sehemu umeteleza toka awali, sasa hii balehe yake inampeleka puta, muite uongee nae kikubwa, ukishindwa mlete kwetu tumfunze adabu..

Kama dingi uko fiti. Akileta ujinga siku mveshe gloves, mpigane, ukishamkanda umueleze kwenye nyumba hiyo mwanaume ni mmoja tu ambae ni wewe, unafanya wale, yeye asome, sasa asilete mambo ya kisemge akotaka ubabe atafute kwake, kwako ni kauli ya mwanaume mmoja tu ndio inazungumza..... hapo kihuni,
Ila kisaikolojia pia inawezekana
Nilitaka nikuite mshkaji wangu, bora umefika na umemalizaa..!! Ushauri murua
 
Kijana wangu, ana miaka 20 kwa sasa, yuko chuo anamaliza mwaka wa kwanza, tangu alipomaliza kidato cha sita kawa mtu wa hasira sana, akikosea kitu ukimuonya hataki kabisa kusikiliza, badala yake ataanza kuongea kuonesha hakubaliani na baada ya hapo ananuna haongei na mtu hata siku 3.

Hali hii imekuwa kero sana kwa familia yetu kwani akiwa katika hali hiyo, kila anayemsemesha anamjibu kwa sauti ya kufoka, anapenda kukaa peke yake, anakuwa busy tu na simu yake na si watu wa familia yake, na ikifika wakati wa chakula hajumuiki na wengine anakula kwa wakati wake mwenyewe.

Kuna muda natamani hata likizo iishe arudi chuo nisimuone kabisa kwani kawa simba ndani ya nyumba yangu mwenyewe, kuna muda natamani kumkata makonde ila najizuia, sijui kapatwa na nini.

Je, nifanyeje kumsaidia aache tabia hii ambayo katika makuzi yake hakua nayo, kwa sasa ni mtu mzima siwezi hata kusema nitatumia fimbo.
Mimi nina kijana wa kiume yupo chuo kama kijana wako,
Akizinguwa najifungia nae ndani tunazichapa haswa,,
Sasa kanyooka .

Piga makofi hyo wacha kuleta huruma kwenye malezi.
 
Huyo inabidi apuuzwe muda wa msosi ukifika mkimuita mara moja imetosha na msibakizie chakula asipopiga simu hakuna mkupigia lakini kama atakuwa ananuna kidogo tu halafu mnamnyenyekea atawapanda kichwani
Inatakiwa wampige huyo. Atawanyea mkimuendekeza.
 
Mkuu kuna pahala umekosea baina yenu nyie wazazi\walezi
Kama hawezi badilika kwa ushauri,amesha fika umri wa kujitegemea wwe unachofanya kwake no bonus tuu
Usiwe mzazi was doticom kuogopa motto kununa be a man dude ain't a boy
 
Mimi nina kijana wa kiume yupo chuo kama kijana wako,
Akizinguwa najifungia nae ndani tunazichapa haswa,,
Sasa kanyooka .

Piga makofi hyo wacha kuleta huruma kwenye malezi.
Hii ndio solution. Ujinga wake akafanyie kwake huko sio kwako. Hao ni wale watoto wakileta ujinga wanachekewa.
 
Mara ya mwisho umekaa na kuzungumza naye lini?

Wakati mwingine gap baina ya Wazazi na mtoto huweza kuchangia hayo kutokea

Kwahiyo ni vyema wakati mwingine kama wazazi kujenga utaratibu wa kuzungumza na watoto wetu, wakuzoee na uwazoee pia...

Zungumza naye akiwa kwenye Hali kawaida na umweleze usivyopendezwa na tabia yake.

Atambue wewe ni Baba yake, kwahiyo ni lazima aishi na kubehave vile unavyotaka.

Mambo ya kununa na kususa atafanya kwenye mji wake

Hapo ni kwako na mkeo

Sisi zamani, tuliweza kupigwa na Wazee wetu hata tulipokuwa na miaka 23, sembuse hiyo 20 ya "dogolasi"

Na Kuna makabila, hata uwe na miaka 40, ukizingua unaitwa na kutandikwa bakora
 
Hii ndio solution. Ujinga wake akafanyie kwake huko sio kwako. Hao ni wale watoto wakileta ujinga wanachekewa.
Kabisa mkuu,,napiga makofi sawa sawa,,
Akiniona tu,,ananyoosha maelekezo.
Iweje kijana wako mwenyewe ushindwe kuthibiti?
 
Back
Top Bottom