Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

Objective football

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2023
Posts
1,195
Reaction score
2,771
Safari yetu ya utafutaji katika dunia hii imejaa misukosuko mingi sana either ya kifamilia, ndoa, kazi na kipato.

Wapo watu chungu nzima dunia hii inawasulubu na hawajui wafanye nini kila wanalofanya linakwama iwe ajira, mahusiano na kipato.

Wapo watu ambao mambo yao yamewanyokea kutokana na juhudi zao saizi wana usafiri, wanavaa safi na kusaidia familia zao kiasi kwamba wanaona wengine wazembe

Mfano mimi nimewahi pata msala katika utafutaji kama sio ndugu na washkaji zangu kunipa faraja, ushauri sidhani kama ningefika hatua moja mbele. Ilifika hatua nikamuomba MUNGU.

why Umeruhusu haya majaribu?

Shusha uzoefu wako ni msukosuko upi huwezi usahau ,na ulijikwamua vipi?

Na ambao mambo bado tafrani wafanyaje waweze kupata nafuu?
 
Safari yetu ya utafutaji katika dunia hii imejaa misukosuko mingi sana either ya kifamilia, ndoa,kazi na kipato.

Wapo watu chungu nzima dunia hii inawasulubu na hawajui wafanye nini kila wanalofanya linakwama iwe ajira,mahusiano na kipato...
Ulevi wa ngono.

Hiyo ni hatari mkuu.

But jesus rescue me I thank him"
 
MWANAMKE..

Nilikuwa na mwanamke kipindi fulani nikiwa vizuri kiuchumi. Nilimsomesha pia. Baada ya kumaliza alipata kazi. Ikumbukwe nilipata nae mtoto mmoja.

Baada ya yeye kupata kazi bahati mbaya maisha yangu yaliyumba sana kwa kuwa nilisimamishwa kazi kampuni niliyokuwepo wakati ule. Nilianza upya kutafuta kazi hadi kwa kuhonga ili niingie kwenye vitengo ila haikuwa hivyo, nilifeli.

Nilijikuta akiba yote imeisha nikiwa sijapata kazi, hapo ndipo mambo yalianzia. Mwanamke alianza kujazia sehemu zenye mapungufu japo kishingo upande, zikaanza influence za kwao kuwa aondoke kwangu sababu sina mchango wowote tena.

Aliondoka na vitu siku moja nikiwa safari kufukuzia kazi. Nilipigiwa simu tu na watu wa karibu kuulizia mbona ninahama. Asikwambie mtu, from there nikaanza kuishi kama kuku, kuzurura tu. Again I started from Zero. Hakuna alienielewa, si wazazi wake wala yeye. Home wakaniambia nipotezee tu.

Ni mengi sana yalipita nikipata time nitashusha kila kitu. I thank God, nilipata kazi tena kampuni jingine and from there my life is back on track. Sina vikuuubwa ila ninaishi maisha yangu.
 
Back
Top Bottom