Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

MWANAMKE..

Nilikuwa na mwanamke kipindi fulani nikiwa vizuri kiuchumi. Nilimsomesha pia. Baada ya kumaliza alipata kazi. Ikumbukwe nilipata nae mtoto mmoja.

Baada ya yeye kupata kazi bahati mbaya maisha yangu yaliyumba sana kwa kuwa nilisimamishwa kazi kampuni niliyokuwepo wakati ule. Nilianza upya kutafuta kazi hadi kwa kuhonga ili niingie kwenye vitengo ila haikuwa hivyo, nilifeli.

Nilijikuta akiba yote imeisha nikiwa sijapata kazi, hapo ndipo mambo yalianzia. Mwanamke alianza kujazia sehemu zenye mapungufu japo kishingo upande, zikaanza influence za kwao kuwa aondoke kwangu sababu sina mchango wowote tena.

Aliondoka na vitu siku moja nikiwa safari kufukuzia kazi. Nilipigiwa simu tu na watu wa karibu kuulizia mbona ninahama. Asikwambie mtu, from there nikaanza kuishi kama kuku, kuzurura tu. Again I started from Zero. Hakuna alienielewa, si wazazi wake wala yeye. Home wakaniambia nipotezee tu.

Ni mengi sana yalipita nikipata time nitashusha kila kitu. I thank God, nilipata kazi tena kampuni jingine and from there my life is back on track. Sina vikuuubwa ila ninaishi maisha yangu.
Ladies and gentlemen, I bring you... Women
 
Back
Top Bottom