Polee mkuu, nahisi maumivu yako.
Kuna mwanamke nilishawahi ku-date naye miaka ya nyuma, aisee nilimpenda sana na hali yake ya kunitegemea mm kwa kila kitu ndo ilinifanya nimpende zaidi na zaidi.
Aliniomba ahamie ghetto kwangu, kwa upumbavu wa kupenda uchi nikakubali, kumbe nafuga shetani, aisee nilikuwa namnunulia kila kitu mzee...chupi, pads, vocha yaan like 95% ya mahitaji yake yote ela ilitoka mfukoni kwangu.
Sasa kuna kipindi nilipatwa na matatizo, uwezo wangu wa kumhudumia ukapungua, aisee niliona kila rangi, sikuamini yale maneno yalitoka kinywani mwake. Kuna maneno alinambia bado nayakumbuka, ndo maana hadi leo naogopa wanawake wa Tanga.