Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

Kijana, Wapi uliteleza hadi kuharibikiwa kimaisha?

UZEMBE.

Tukiachana na mahusiano na ulevi UZEMBE ni jambo linalotukwamisha sana vijana kufikia ndoto zetu.
Mimi ni mmoja kati ya wanafunzi waliobahatika kujiunga na elimu ya juu miaka kadhaa ilopita. Nliendekeza uzembe kipindi nikiwa chuo kiasi kwamba suala la kupga msuli sikulichukulia kama ndo kilichoniweka pale.

Mwaka wa kwanza nlipga GBA ya 2.1 na ata ckuwaza as long as bado nliexist kwenye system ya chuo na BOOM lilisoma kama kawa.

Mwaka wa pili pia sikubadili jambo. Aloo!!!! Hamuez amini nlikutana na neno DISCONTINUED likipambwa na maneno haya " reason: GPA below an average. "

Kuanzia apo akili yangu ilitibuka. Nikaona n kama nimetupwa na dunia.nilizunguka lila kona ya mtaa nisione cha kushika mazee 😁😁. Kila mtu nlihisi ananitenga na hatak stori na mimi. Familia yangu ndo kabisaaaaa, si baba, si MAMA, si ndugu, wote walinichukia an.

Kwa BAHATI nzuri nilikubaliana na hali ile mapema sana. Niliingia rasmi kitaa, nikafakamia kazi yyte inayopita mbele yangu. Kikubwa iwe halali na iwe na chochote. Nlijitafuta katika mazingira matata sana, nlilala nje siku 9 nikiwa sina pa kuutua mwili wangu baada ya Kazi ngumu za mchana zilizoniacha na buku 3 na uhakika wa kula tu😣😥. Nlipitia vingi lkn nikaona sawa tu, alaf fresh tu.

Nliparata mkonge sana, nikauza maji barabaran, nikafanya Kazi kiwanja cha SUNOLA Singida, nikatembeza nguo mwanza, mpaka pale nlipoamua kuwa MVUVI. Nimepiga kasia sana yani, apo kdg nikipata MWANGA na kuondoka tongotongo mpaka pale nlipoachana na kasia na kuanza biashara ya kuagiza na kusambaza nyavu. Hapa ndo nikaanza na kuongezeka uzito baada ya kuwa mkonde kwa muda mref.

Sikuufagilia uvivu na uzembe popote nlipopita an. Hii imenisaidia mpaka sasa nina miradi kadhaa ambayo inanipa kuishi. Angalau sasa nyumbani wananielewa, uhakika wa kufunga ela ndefu kwa mwezi upo.

VIJANA TUFANYE KAZI KWA BIDII. UVIVU, UZEMBE, MAHUSIANO MABOVU NA ULEVI tusiviabudu.
nimeokota kitu hapa aiseeh
 
Back
Top Bottom