Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
Haa ha ha; we jamaa yaani kati ya mafunzo ya SUMA JKT na mgambo yepi makali? SUMA JKT wale ni wana jeshi kabisa wale kaka, sheria tu ndio haiwaruhusu kufanya zaidi ya kile wanacho kifanya, alipo SUMA JKT police anapaogopa. Sorry kua nje ya topic ila umenifurahisha kwa mchango wako
Mgambo anafundishwa na nani na huyo Suma JKT anafundishwa na nani? Kwa muda gani na course content ikoje?
Suma JKT wako makundi mawili;
1. Wale waliopitia JKT kwa program ya kujitolea miezi sita ya kozi lakini mwisho wa siku wakakosa ajira kwenye vikosi vya Ulinzi na Usalama (serikalini),
2. Wale wanaookotwa kitaani kwenda crush program kupiga kozi fupi kisha kuvishwa uniform kuingia lindoni
Unatakiwa kujua kingine, kuna mgambo wameajiriwa Suma JKT pia kwa sababu Suma JKT ni shirika linaajiri kikubwa uwe na ujuzi wa mbinu za medani (Basic military training) hata wewe kama ulipita JKT zama hizo na cheti unacho hauna kazi nenda Suma JKT upate kibarua mwisho wa mwezi upokee laki 2 zako ukalale.
Kwanini Suma JKT wanakuwa watata na kupelekea watu wengi wawaogope? Hawa watu wengi wao wamekosa fursa za ajira ya moja kwa moja wengi wao wana hasira sana na wanafanya kazi kwa kujikakamua ili wasichukuliwe poa[emoji23][emoji23]
Ila kiuhalisia ni weupe tu zaidi ya mob psychology wanayoweza kuungana na kukufanyia vurugu, ukimbana mmoja mmoja hakuna jipya hata jioni ya leo kuna Suma JKT anawaza akitoka Lindoni pale atm ya crdb ataenda kula nini[emoji23][emoji23]