Kijeshi, Urusi imefeli vibaya sana huko Ukraine

Kijeshi, Urusi imefeli vibaya sana huko Ukraine

Mwanzo donesk na luhansk waasi walikuwa wanamiliki nusu ya majimbo.sasa ivi waasi wanamiliki zaidi ya asilimia 70 ya majimbo.Jimbo la Kharkiv nusu linamilikiwa na warusi.jimbo la Zaporizhia asilimia 80 linamilikiwa na warusi.jimbo la kherson warusi wanamiliki asilimia 100.

Sasa hapo mpaka muda huu nani kapata hasara?
Ndani ya mwezi mmoja ujao Urus hatakuwepo Tena ndani ya Ukuraine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamanda wa majeshi ya Ukraine yaliyojichimbia kwenye mahandaki ya kiwanda cha chuma amemuomba papa Francis wa Vaticana asaidie kuokoa maisha yao.
Amesikika kwenye vidio akilalamika kuwa wamebakiwa na masaa machache tu huku akitilia maanani nyongeza ya muda wa kujisalimisha uliotolewa na Urusi huku na wao wakiwa wameishiwa na chakula na silaha na vile vile kuzingirwa kwenye njia zote za kutokea.
Huyo kamanda zaidi ya kuomba msaada kwa papa ili waokolewe amewaomba viongozi wote duniani kusaidia kuondoka salama eneo hilo hata ikiwa watapelekwa nchi nyengine ya mbali.
ttps://www.bbc.com/news/live/world-europe-61157670
 
hakuna rais aliyewahi kupigana na nchi zaidi ya 30,na akawa piga na kuwafanya waanze kuomba huruma kwa dunia yote wasaidiwe Vita,ukiacha Hitler ,ni Russia kwa Sasa,hata huyo marekani hajawahi kuingia Vita na nchi 30.

mpaka hapo,hakuna nchi yenye nguvu kijeshi duniani kushinda Russia ,Kama malengo ametimiza yote,kumzuia Ukraine akome kuwaza kuhusu NATO Hilo ametimiza, zelensky kwa ss NATO anaiona Kama sumu kwake na anajuta.pili kaigawa Ukraine izae vi nchi vingine Kama 3 au 4,Hilo amefanikiwa ,tatu Ukraine kwa Sasa haina bahari Tena Hilo amefanikiwa,lkn pia amefanikiwa kumvimbia marekani na kumuonyesha marekani sio super power Tena wa kuamua kila kitu Hilo amefanikiwa. Kiujumla NATO na marekani wamemfanya Russia again confidence zaidi kuwa yy ni taifa lenye nguvu duniani ,kuliko mwanzo.lakini pia hii Vita imeiweka Russia kwenye ramani nyingine kabisa duniani ,kuwa ni taifa pekee linaloweza kumdhibiti marekani na NATO yake ,na kubadili upepo wa world order!!!!

Sasa tunaelekea uelekeo wa new world order,na aliye i lonch ni Russia ,sio mmalekani tena.ila mtekelezaji ndo hatujui atakuwa Nani au wakina Nani!!
Putin atashindwa vita na huu ndo mwisho wake wa utawala amini hivo kama huamin basi subili muda utakupa majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana connection ndefu.
Hao wanauwezo wa kushawishi Nchi kubwa ili Ukraine apewe silaha na msaada mkubwa zaidi as long as it takes kumvunjavunja nguvu Urusi.
Na pia Wana uwezo wa kuwezesha vikwazo dhidi ya Urusi ving'ate kwelikweli
Wayahudi wamejaa pande zote Russia na Ukraine, na kote ni players wazuri sana kwenye uchumi wa nchi.

Ndio maana Israel imenyamza kimya kwenye hii vita
 
Wewe hujui kwamba EU na Nato pamoja na US wako pamoja kumpiga Mrusi huo ni super power wenyewe, jeshi lako bado liko imara na uchumi wake bado unaendelea........Naomba unatajie vita yoyote US kaenda peke yake kupigana,
Kumbuka China na Russia wameiplan hii vita muda mrefu sana. Hizi ni super power mpya za dunia
 
I used to respect your contribution hapa jf, ila katika hili umefeli kufanya deep and objective analysis, malengo ya urusi sio kuteka kievi hapana ni matatu na ame achive almost 70% zerelesiky baada ya vita hawezi kua Raisi wa ukurain tena hapo ameshikiliwa na Nato pamoja na US propaganda ila wa Ukuraini wamesha kiona ni ze comedy kabisa malengo ya Urusi ni:

*Denazification of ukurain achieved 90%
*Kutenga ukurain na Nato achieved 99%
*Kuunda jamhuri mpya Donesk Republic achieved 50%
Hapo amefail wapi?.
Other achievements of Russia
  • Ameonyesha ulimwengu kwamba ni superpower
  • Amejaribisha silaha zake za siku nyingi
  • Amedhofisha marikani na kumtia aibu
*Amesababisha kuyubisha uchumi wa EU na US. NK.
Umesahau lingine; hi vita imeleta UFA wa umoja wa Marekani na mataifa ya Ulaya, zamani ilikua USA akisema wekea fulani vikwazo, wote wanakubali, this time German, France, Spain wameendelea kufanya biashara na Urusi pamoja na vikwazo vya USA to Russia.
 
Umesahau lingine; hi vita imeleta UFA wa umoja wa Marekani na mataifa ya Ulaya, zamani ilikua USA akisema wekea fulani vikwazo, wote wanakubali, this time German, France, Spain wameendelea kufanya biashara na Urusi pamoja na vikwazo vya USA to Russia.
China's Vice Foreign Minister Le Yucheng reiterated to Russia's Ambassador to China Andrey Denisov that Beijing intends to maintain its "high-level development" and "comprehensive strategic partnership" with Moscow.

"No matter how the international landscape may change, China will continue to strengthen strategic coordination with Russia for win-win cooperation, jointly safeguard the common interests of the two countries and promote the building of a new type of international relations and a community with a shared future for mankind," Le said, according to a readout of a meeting between the diplomats.

During the bilateral meeting, the two also discussed ways to "deepen cooperation in various fields" and talked about the war in Ukraine, according to a readout from China's Ministry of Foreign Affairs.

On Monday, the Biden administration said it had not yet seen China provide material or financial support to Russia for its invasion of Ukraine.

"If the PRC were to provide weapons, supplies or seek to help Russia evade sanctions, there would be strong consequences for that," State Department spokesman Ned Price said during a daily briefing.

— Amanda Macias
 
Pro NATO kwa kujifanya wajuaji hawajambo aloo. Yaani pamoja na kipigo wanachokula Kila siku hao mabwege mpaka wanajifukia kwenye mahandaki mtu Bado unapata ujasiri wa kusema eti Russia kashindwa😃😃😃😃😃😃😃😃.
Kubalini tu Putin kawavua nguo NATO mnatafuta Kila kilichojiri mbele yenu kufunika nyuchi zenu mpaka mnaokota visivyo okoteka🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Mafanikio vitani sio kuharibu makaazi ya raia,jua hilo
 
Ha ha ha ha ha ha
mpaka muda huu ukraine imegawanya kati kati miji ya ya lungnsk donenk mariupol kharkiv khersan oddess imeshakuwa chini ya Mrusi.

Mpaka muda huu ukraine haina tena bahari mijai tajawa hapo juu ni miji ya kichumi kwa ukraine. Kitenda cha urusi kuiteka miji hiyo kuna uwezekano uchumi wa ukraine usiufikie hata uchumi wa hapa morogoro

Alafu hii vita ni ya urusi na nato na nato wemepigika mno mpaka makamanda wao kukamatwa

Urusi sio marekani iliyoshindwa kuiteka kamji kadogo ka mogadishu pale Somalia.

ha ha ha ha ha ha ha
👍👍👍🤛🤛🤛
 
Mafanikio vitani sio kuharibu makaazi ya raia,jua hilo
Nakuelewa mkuu, umesahau kuongeza mafanikio kwenye vita siyo idadi ya Wanajeshi waliojisalimisha, idadi ya maeneo ya adui yanayoshikiliwa na idadi ya silaha zilizoharibiwa. Ndiyo maana pamoja na vita kuendelea Ukraine kila siku wanawagawia vifaa vya kivita Kenya
 
Ukiitazama hii vita katika jicho la kijeshi ni dhahiri urusi imefeli!
Imefeli kwa sababu imeshindwa kufikia malengo yake ya uanzishaji hii vita!

Lengo la Kijeshi la Urusi ilikuwa ni kuingia Kiev haraka, kukamata mji mkuu na kuuangusha utawala wa Zelensky. Lakini hadi leo hii takriban siku ya 60 ya kivita, Urusi imeshindwa kukamata Kiev, na majeshi yake baada ya kukutana na upinzani mkali yakakimbia(retreat) kutoka miji ya ndani na kurudi huko Mashariki ambako walikuwa wanapakalia toka mwaka 2014.

Urusi imepata hasara kubwa sana ya vifaa na askari. Vifaru vyake vilikuwa vikikaangwa kwelikweli na Javelin missiles, pamoja na drones za Bayraktaar.

Logistics za kupeleka chakula na silaha ndanindani kwa askari wake ilikuwa shida

Wakati huo vikwazo vikiendelea kuichakaza urusi kwelikweli.

Hadi hivi sasa Zelensky amefanikiwa kuilinda serikali yake, na kinachofuata sasa ni kuandaa operesheni kabambe ya kumtoa nyoka pangoni huko Mashariki, Hii itakuwa operesheni kali sana na ngumu sana lakini itawezekana.

Urusi ni Taifa kubwa lakini uchumi wake ni mdogo kuliko jimbo moja tu la Texas Marekani, haina fedha za kupigana hii vita kwa muda mrefu, itakachokifanya ni kutafuta kideal cha kizushi na Ukraine ili kuficha aibu ya uso wake!

Kikubwa nilichojifunza katika hizi vita, Moyo wa askari una nguvu kuliko silaha kali ktk mikono ya askari asiye na moyo wa mapambano!

Mafanikio ya kijeshi ya Urusi huko mashariki mwa Ukraine katika vita hii ya Sasa wala si jambo la ajabu maana warusi walishakuwepo huko toka mwaka 2014, hakuna kitu kipya!. Ni sawasawa na kupiga bomu mochwari na kisha kushangilia kuwa umeua!
Ni kweli kabisa Mimi Kama mwanajeshi na mtaalamu WA makombora ya masafa ya kati.russia ameShindwa Vibaya sana
 
Nakuelewa mkuu, umesahau kuongeza mafanikio kwenye vita siyo idadi ya Wanajeshi waliojisalimisha, idadi ya maeneo ya adui yanayoshikiliwa na idadi ya silaha zilizoharibiwa. Ndiyo maana pamoja na vita kuendelea Ukraine kila siku wanawagawia vifaa vya kivita Kenya
Kwa haraka ni nchi gani imepoteza silaha nyingi na za thamani kubwa? Pima na idadi ya mpinzani je mpiingia mkiwa na uwezo sawa wa silaha? Ukraine kilichomsaidi ni ari na Javelin pamoja na drone za Mturuki. Putin kaingia akiwa na kila kitu lakin mpaka leo hajafikia malengo yake. Nini tafsiri hapo? Kashindwa au kashinda?
 
Kwa haraka ni nchi gani imepoteza silaha nyingi na za thamani kubwa? Pima na idadi ya mpinzani je mpiingia mkiwa na uwezo sawa wa silaha? Ukraine kilichomsaidi ni ari na Javelin pamoja na drone za Mturuki. Putin kaingia akiwa na kila kitu lakin mpaka leo hajafikia malengo yake. Nini tafsiri hapo? Kashindwa au kashinda?
Mkuu mbona mimi nimekuunga mkono sasa hapo juu😀😀😀😀😀😀😀kwamba iliyoyasema uko sahihi kajisa isipokuwa tu nimekuongezea na machache niloyodhani umesahau!
 
Mkuu mbona mimi nimekuunga mkono sasa hapo juu😀😀😀😀😀😀😀kwamba iliyoyasema uko sahihi kajisa isipokuwa tu nimekuongezea na machache niloyodhani umesahau!
Sawa mkuu ila nilijaribu kurejelea comment yako juu kabisa
 
Back
Top Bottom