Kijeshi, Urusi imefeli vibaya sana huko Ukraine


Mgambo anafundishwa na nani na huyo Suma JKT anafundishwa na nani? Kwa muda gani na course content ikoje?

Suma JKT wako makundi mawili;
1. Wale waliopitia JKT kwa program ya kujitolea miezi sita ya kozi lakini mwisho wa siku wakakosa ajira kwenye vikosi vya Ulinzi na Usalama (serikalini),
2. Wale wanaookotwa kitaani kwenda crush program kupiga kozi fupi kisha kuvishwa uniform kuingia lindoni

Unatakiwa kujua kingine, kuna mgambo wameajiriwa Suma JKT pia kwa sababu Suma JKT ni shirika linaajiri kikubwa uwe na ujuzi wa mbinu za medani (Basic military training) hata wewe kama ulipita JKT zama hizo na cheti unacho hauna kazi nenda Suma JKT upate kibarua mwisho wa mwezi upokee laki 2 zako ukalale.

Kwanini Suma JKT wanakuwa watata na kupelekea watu wengi wawaogope? Hawa watu wengi wao wamekosa fursa za ajira ya moja kwa moja wengi wao wana hasira sana na wanafanya kazi kwa kujikakamua ili wasichukuliwe poa[emoji23][emoji23]

Ila kiuhalisia ni weupe tu zaidi ya mob psychology wanayoweza kuungana na kukufanyia vurugu, ukimbana mmoja mmoja hakuna jipya hata jioni ya leo kuna Suma JKT anawaza akitoka Lindoni pale atm ya crdb ataenda kula nini[emoji23][emoji23]
 
Unashangaa hili, Waziri wa Ulinzi wa Urusi yule Sergei Shoigu ni Civil Engineer na hakuwahi kuwa jeshini hapo kabla. Ni kama umbebe mtu Tanroads uko, sasa hajabu kwa mleta mada ni nini

Hakuna hajabu mkuu[emoji23][emoji23]
 
Kwa jicho la kijeshi!

Wengi humu kupitia michango yetu tunafahamu kuwa lengo mojawapo la Urusi kuivamia Ukraine lilikuwa ni demilitarization. Ila ni wachache sana tutafahamu kuwa, lengo hili mara nyingi hufanikiwa ipasavyo linapo ambatana na kuuondoa madarakani utawala wa adui.

Majeshi yote ya nchi huwa yako chini ya utawala wa nchi husika huku kiongozi wa nchi akiwa ndiye amiri jeshi mkuu. Hivyo, mara nyingi majeshi hutii amri na maagizo ya utawala uliopo madarakani. Hata katika masuala ya mobilization na recruitment ya majeshi pia viko chini ya supervision ya utawala uliopo.

Njia pekee zenye uhakika wa kuhakikisha kuwa zoezi la demilitarization dhidi ya adui linafanikiwa kwa ufanisi ni mbili:

1) Regime change. Kama nilivyosema, utawala uliopo madarakani ndiyo chachu kubwa ya kuyaongoza majeshi kuendelea kuilinda mipaka ya nchi. As long as utawala unaendelea kuwepo madarakani, basi majeshi yataendelea kufanya kazi zake.

Ushahidi wa hili ni katika vita kubwa zilizowahi kutokea duniani mfano, WW2. Iliyokuwa USSR ilipoteza wanajeshi wengi sana hasa dhidi ya Hitler wakati wa Vita ya Pili ya Dunia, lakini, uwepo wa serikali inayofanya kazi (functioning government) uliwezesha majukumu mengine kuendelea kama kawaida ikiwemo recruitment ya majeshi usiku na mchana kufidia upotevu.

2. Makubaliano. Hii ni njia ya pili ambapo pande zote mbili hufikia katika meza ya majadiliano na kisha kukubaliana kupunguza majeshi ya upande mmoja ama pande zote kwa maana ya demilitarization, kwa maslahi ya pande zote.

Uvamizi wa kijeshi wa Urusi nchini Ukraine kwa kiasi kikubwa ulikuwa na lengo la kuiondoa madarakani serikali iliyopo kama njia mojawapo ya demilitarization ambayo nimetoka kuisema. Lengo hili lilipo shindikana, ndipo tulipoanza kuona njia ya pili hapo ikijaribu kuchukua nafasi yake.

Kwa wale wanaosema kuwa Urusi haikuwa na lengo la kuingia Kyiv na kuuondoa madarakani utawala wa Zelenskyy nina swali moja kwenu ambalo ni rahisi tu.

Hivi, kwani hatukumsikia Putin mwenyewe mapema kabisa kwenye vyombo vya habari akiwaomba wanajeshi wa Ukraine wampindue ama wamuondoe madarakani Zelenskyy?

Je, majeshi ya Urusi yenyewe yalishindwa kutekeleza jukumu hilo, suala lililo pelekea mpaka kiongozi wa Urusi kutoka hadharani na kuliomba jeshi la adui yake kuwasaidia hilo jukumu?

Je, tuendelee kuziamini hizi hoja kwamba Urusi haikuwa na malengo ya kuiondoa madarakani serikali ya Zelenskyy? Wakati hata kauli za viongozi wa juu wa utawala wa Urusi zinaonesha dhahiri malengo hayo!
 

Chukulia wamefeli ndio!!! Wewe unatakaje sasa
 
Umechambua vizuri sana mkuu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Sikuwa na nia ya kujibu Uzi huu na Uzi mwengine kwa sababu ya azma niliyojiwekea mwenyewe binafsi kwa kanuni na nidhamu ama misingi iliyoniwajibikia juu yangu. Isipokuwa ulichokiandika kimenifanya nami niandike.

Ningependa niende kwa vitendo kwa anuwani yako ya juu uliyoiwasilisha na vitendo vinazungumzo zaidi kwa sababu vinaepusha na kupunguza mlolongo wa maneno/maandishi zaidi.

Malengo ya Urusi kuanzisha hii vita ni haya:

Mtafute huyu You Tube, kuna speech yote ya Putin na malengo ya kuanzisha hii vita ambayo wao wanaiita military operation Putin ameyataja humo. A-Z yapo tofauti na uliyoyataja wewe.

Wengi wetu katika sisi ukiwemo na wewe na ndivyo ilivyozoeleka na ndivyo ambavyo inavyofanyika kwenye vita, jambo muhimu baina ya nchi mbili zinaposigana kijeshi basi nikuteka mji mkuu wa nchi ya mwenzako. Hiki ndicho wengi tunachokifikiria.

Ikiwa hii nukta uliyoileta ndilo lengo la Urusi inatubidi tuwaze mbali zaidi. Ikiwa Urusi kujihakikishia usalama wa nchi yake ni kumuondoa Zelensky nchini Ukraine na kuikalia hiyo nchi hii mbinu itadumu kwa muda gani?

Ukoloni ni jawabu tosha! Hata uwe na nguvu namna gani huwezi kumtawala mtu milele. Hususani suala kubwa kama nchi huwezi kuitawala milele. Ikiwa lengo lako ni kulinda usalama wa nchi yako utatumia mbinu gani? Mabepari walitumia mifumo yao ya kuhakikisha sisi kuendelea kuwa tegemezi kwao ili wao wapate mwanya ama fursa ya kulinda maslahi yao. Hivyo unabakiwa na uhuru wa bendera.

Fursa ya namna hii kwa Urusi ipo nayo ni majimbo yaliyo mashariki mwa Ukraine ambayo ina wakazi wenye asili ya Kirusi. Usalama wa Urusi upo kwenye haya majimbo. Piga ua hakuna namna, haya majimbo Mrusi atahakikisha yawe huru kwa kujitegemea yenyewe ili kabla ya kumgusa Mrusi kwanza uwaguse wale.

Hili suala ukiliangalia lina njia nyingi sana ambazo ni faida maradufu kwa Mrusi. Tusifikirie kwa kimazoea! Ukiangalia anachokifanya Mrusi anapita kwenye njia zilizojengeka kimazoea kimbinu za kivita na kwenye uwezo wa watu kufikiri kukamilisha malengo yake.Ukitaka kuamini hili tusubiri vitendo vilevile vitaongea (mwisho wa hii vita).
 

K**"ma mamaako...usilete ushabiki watu wakifariki kwa vita....Urusi amevamia Ukraine kibabe...ameua wananchi wengi
 
Urusi kafeli saaana..
 
KIUJUMLA Urusi wameshapata mafanikio makubwa sana katika hii vita. Ukraine na western allies wameshapotezwa, walihadaika na mipango ya urusi wakadhani urusi wana lengo la kuiteka Kiev, Siyo Kiev wala Kharikiv lilikuwa lengo la urusi. issue ilikuwa ni majimbo ya DONBASS NA LUHANSIK. na sasa harakati za kijeshi zinaendelea vizuri huko. western walitumia nguvu kubwa sana kuyazuia majeshi yenye malengo bandia yaliyokuwa yanatishia kuiteka kiev!
 
🀣🀣🀣
 
πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“ŒπŸ€£
 
Very objective comment
 
K**"ma mamaako...usilete ushabiki watu wakifariki kwa vita....Urusi amevamia Ukraine kibabe...ameua wananchi wengi
Kutukana hakukufanyi uonekane una uchungu sana na raia wa Ukraine kufa, neither haifanyi vita iishe wala Ukraine ashinde zaidi sana inaonyesha uwezo hafifu wa kufikiri kwako.

Urusi kavamia ukraine kaua watu then what? Nini utafanya wewe kama wewe ili kuzuia watu wasife Ukraine? Kwa kutukana?
 
Kwa maoni yangu ni mapema sna kutuaminisha kua urusi imeshindwa hii operation yake nchini Ukraine [emoji1255], siku katibu wa UN alipokua Kiev, urusi alishusha makombora kama yote
 
Kwa maoni yangu ni mapema sna kutuaminisha kua urusi imeshindwa hii operation yake nchini Ukraine [emoji1255], siku katibu wa UN alipokua Kiev, urusi alishusha makombora kama yote
Mbona wakienda viongozi wa Magharibi hashushi hayo makombora,anawaogopa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…