Kijiji cha Manzeye Wilayani Mbinga hakina umeme, baadhi ya maeneo watakiwa kununua haki zao

Maguguma

Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
13
Reaction score
7
Kijiji cha Manzeye kilichopo Kata ya Wukiro Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma kipo kwenye orodha ya vijiji vilivyokosa umeme mkoani Ruvuma.

Kijiji hicho ambacho kinapakana na kata ya Litembo hadi sasa wananchi wake hawajui ni lini watapata umeme huo ingawa baadhi ya maeneo wasimamizi wa mradi wa REA walishasimika nguzo toka mwaka jana.

Wakati wa kusimika nguzo hizo baadhi ya maeneo yaliachwa bila kusimikwa huku watendaji wa REA wakifafanua kwamba maeneo hayo bado hayapo kwenye mpango wa kupata umeme kwa sasa.

lakini jambo la kusikitisha zaidi baadhi ya watendaji wa REA waliwataka wananchi wanaoishi eneo la Mheleketi (Malangali) watoe kiasi cha shilingi laki nne ili wapewe huduma hiyo wakati maeneo mengine walisimika nguzo hizo bila kuchukua pesa kwa wananchi.

Kiasi hicho cha fedha kilitafsiriwa kama ni rushwa na ilitakiwa kitolewe siku chache kabla ya sikukuu ya Noeli na Mwaka mpya.

Kimsingi eneo la kata ya Wukiro vijiji vyake vyote havina umeme hadi sasa lakini kata za jirani zina umeme hali ambayo imeendelea kuwakatisha tamaa wanakijiji wa Manzeye na kata yote kwa ujumla.

Kijiji hicho pia miundombinu yake ya barabara ni mibovu hasa kipindi hiki cha mvua. wanakijiji wanalazimika kutumia usafiri wa miguu na pikipiki kwenye shughuli zao za kila siku, wakati mwingine wanalazimika kutembea hadi Mbinga mjini zaidi ya kilometa 25 kwa miguu ili kufuata huduma mbalimbali.

Wakazi wa kijiji cha Manzeye ni maarufu kwa kulima kahawa, mahindi, ngano, ndizi n.k.

manzeye - 2023.jpg
IMG-20230327-WA0006.jpg
 
Ka center kao full burudani. Daah hiri rinchi rikubwa!

View attachment 2567846View attachment 2567848
 
Back
Top Bottom