Kijiji chote kimesombwa na Mafuriko, Kanisa limebaki

Kijiji chote kimesombwa na Mafuriko, Kanisa limebaki

IMG-20231207-WA0039.jpg


Nyumba iliyowekwa wakfu kwa Yesu Kristo imesimama katikati ya mkondo wa dhoruba uliobeba nyumba zote.
 
Huu wala sio muujiza bali ni ujenzi madhubuti.
Watanzania wengi hawajengi nyumba bali vibabanda vilivyopakwa rangi na kung'aa.

Wajenzi watanielewa.

Msiponielewa jifunzeni hata mfano wa Yesu kuhusu ujenzi imara.

1. Nyumba bora juu wa mwamba
2. Na nyumba ya kuvutia juu ya mchanga

Nyumba ni msingi imara na wenye viwango.

Lakini wengi kwa ubahili ama kutokujua...misingi sio imara na ni mifupi unaingia ukiendesha baisjeli.

Nyumba yenye msingi na matirio ya kiwango kiasi flani ina usalama.

Nyumba za Katesh 99% hata lenta hakuna na juu ya mlango na dirisha zinawekwa ubao...ulitegemea nini kwa janga kama hilo.

Hilo kanisa ni la RC na RC wako makini sana
 
Shughulisha akili Kanisa limejengwaa imara sehemu nzuri sio kama nyumba za wala hoi hizo
 
View attachment 2833512

"Kwenye madhara haya tumepata majeruhi pia wapatao 116, wanaume ni 56 na wanawake ni 60, ndugu Watanzania haya maafa ni makubwa sana, pia tumepata uharibifu mkubwa wa nyumba za kuishi, mashamba na mitambo mbalimbali ya magari, nimepata bahati ya kwenda Gendabi nyuma ya milima, kile kijiji nyumba zimeachwa upande wa kulia na kushoto eneo la katikati nyumba zote zimeondoka limebaki kanisa tu, hali sio nzuri,"

Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

===

Salamu,

Huko Hanan'g kijiji cha Ngendabi nyumba zote zimesombwa na maji ila kanisa limesimama vilevile.
Je hii ni sababu ya matereal za ujenzi au Koroho zaidi?
Ujenzi imara location sahibi. Hakuna nguvu za kiroho hapo kanisa lingekuwa na nguvu hiyo basi lingefichwa kama Nyuklia .Hakuna nguvu yoyote kwenye hizo imani
 
Back
Top Bottom