Kikaangoni: Utapeli wa BSS ya Madam Rita, washindi wa nyuma nao wafuatiliwe

Kikaangoni: Utapeli wa BSS ya Madam Rita, washindi wa nyuma nao wafuatiliwe

Mi nadhani huu usumbufu madam Rita anajisababishia na hauna sababu yoyote. Hivi kwani angefanya kwamba lile ni jukwaa la kukufanya utambulike then mshindi alipiwe studio ngoma hata 3 tu na video then jumlisha promotion aliyoipata muda wote wa mashindano. Then baada ya napo mshindi apambane sasa na yeye, sidhani kama hizi gharama zingefika mil 50 ambazo zinamsumbua na kumdhalilisha saizi.
 
Mi nadhani huu usumbufu madam Rita anajisababishia na hauna sababu yoyote. Hivi kwani angefanya kwamba lile ni jukwaa la kukufanya utambulike then mshindi alipiwe studio ngoma hata 3 tu na video then jumlisha promotion aliyoipata muda wote wa mashindano. Then baada ya napo mshindi apambane sasa na yeye, sidhani kama hizi gharama zingefika mil 50 ambazo zinamsumbua na kumdhalilisha saizi.
ukumbuke yeye ela anachukua kwa wadhamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coca-Cola pop star haikuwahi kufanya mchezo kama huo ilitoa vichwa vya maana

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanachofanya wenzetu kwanza mashindano yao huwa yana vipaji vya ukweli, sio vya kuunga unga... so kinachotokea anatafutwa mtu waneona ana uwezo kisha wanaingia deal.... so, mshindi kupangwa haimaanishi hana uwezo....
 
TENDO moja la hisani hujenga thamani ya utu. Kinyume chake, tendo la dhuluma humpa dhulumati wasifu unaokinzana na ubinadamu. Katili ni lugha rahisi kutamkwa. Unyama linaweza kuwa neno gumu, lakini linandana na ukatili.

Yupo mama. Rita Paulsen ndio jina lake. Ni mwanamke jasiri na mtafutaji. Mrembo sana halafu. Vile ni chotara, ndio uzuri wake ukapata mkondo. Umri unakwenda, hapungui kuwa mzuri. Sasa, pata ladha; mwanamke mzuri, mrembo, jumlisha mtafutaji, mpiganaji. Ni bonge la package!

Mwanzoni mwa miaka ya 2000, Rita alianzisha kampuni ya kurekodi picha za video (motion pictures). Inaitwa Benchmark Production. Kumbukumbu bora ya ujio wa Benchmark ‘mjini’ ni video ya “Zali la Mentali”, kazi ya Prof Jay ft Sir Nature na Muni. Ni kazi ya mwaka 2003. Miss Ilala 2003, Nargis Mohamed ndiye mrembo aliyenogesha kichupa. Mgosi Mkoloni kauza sura pia.

Twende haraka tuwahi kumaliza; mwaka 2006, Benchmark walileta shindano la kusaka vipaji vya muziki. Linaitwa Bongo Star Search. Wenye haraka zao, waliamua kufupisha na kuliita BSS.

Ungemuona Madam Rita akiongoza panel ya majaji. Wanamwita Chief Judge. Ungewaona pia Salama Jabir na yule Mchaga “chizi muziki”, Master Jay. Walishakuwepo majaji wengine katika awamu tofauti. Legend John Kitime. Mdachi wa Mwenge Kijijini, P Funk. Kuna Mzungu Kichaa pia. Hao walipita.

Mwaka jana, kulikuwa na ingizo jipya la majaji; Mom in chief wa Bongo Fleva, Lady Jaydee na brotherman kuliko brothermen wote ndani ya Nyerereland, Dully Sykes, wakiwa na Master Jay, waliongozwa na Madam Rita kufanikisha shindano la BSS 2019.

Rejea mwaka 2007 safari ya BSS ilipoanza mpaka Aprili mwaka huu, unampata Madam Rita katika sifa hii; mwanamke shujaa, kioo, dira na daraja la kimaisha kwa vijana wadogo wenye vipaji. BSS ilichukuliwa kuwa jukwaa huria la mtoko wa kisanii kwa kila kijana mwenye kipaji cha kuimba muziki.

Kuanzia Aprili mwaka huu, sifa ya Rita imechafuka. Sasa anachukuliwa ni mwanamke mdhulumati. Alianzisha shindano bila misingi, na kwamba amekuwa akiwatumia vijana wenye vipaji kupiga hela, halafu hata zawadi ambazo huzitangaza kumbe huwa anawazima. Huyo ndiye Rita anayeonekana sasa.

Hakuna wakati mzuri wa kumpongeza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, kuliko huu. Angalau yeye, bila kutazama uso wa mtu, wala kutaka mazungumzo ya pembeni, aliamua ‘kukichafua’ kwa umma. Sasa wengi wamejua upande wa pili wa Rita.

Kila alichokizungumza Shonza kwa vyombo vya habari, kuhusu jinsi ambavyo Rita amekuwa akimzungusha mshindi wa BSS 2019, Meshack Fukuta, kupata zawadi zake za ushindi, yote unaweza kuyaweka kwenye tafsiri moja; Rita huendesha shindano kwa ubabaishaji. Rita huwadhulumu washindi. Na hili inabidi Rita afanye kazi kubwa kujitakasa.

Chukua maneno ya Shonza, kwamba alipopokea barua ya malalamiko kutoka kwa wazazi wa Meshack, aliwasiliana na Rita ambaye alidai sababu ya kuchelewa kumpa mshindi zawadi ni wadhamini, Star Media (StarTimes), kuchelewa kulipa fedha za udhamini.

Kwamba, uongozi wa Star Media umekwama China tangu Januari mwaka huu kwa sababu ya mlipuko wa Covid-19. Kwamba, kwa kukwama huko China, Benchmark ilishindwa kupata fedha za kumlipa mshindi.

Kumbe, Rita alisema uongo, viongozi wa Star Media wapo nchini na wamejaa tele. Kumbe, Star Media ilishalipa fedha zote za udhamini kwa Benchmark na muamala wa mwisho ulifanyika mapema Januari, mwaka huu. Kumbe sasa, ni Rita mwenyewe ndiye hajaamua kumlipa Meshack.

Wakati ya Meshack yakiwa hivyo, inavuja sasa, kwamba hata mshindi wa BSS 2015, Kayumba Juma, naye hakuziona zile Sh50 milioni za ushindi. Wapo watu sasa wanaamka na kuulizana; kumbe Madam Rita ndivyo alivyo?

Nakumbuka jinsi Kayumba alivyokuwa anapiga shoo. Alijituma kwelikweli. Kila mtu alimpenda. Hata ushindi wake haukuwa wa mbeleko. Alifanya kazi iliyomfanya astahili ushindi. Na alistahili kila stahiki iliyomstahiki mshindi.

Namkumbuka Madam Rita muda mfupi kabla ya kumtaja mshindi. Alisema “muda mchache ujao kuna maisha ya mtu yanakwenda kubadilika”. Naikumbuka sauti ya MC Penny. Alitangaza kuwa kati ya Kayumba na finalist mwenzake, Nasibu, mmoja wao alikaribia kutajirika.

Naikumbuka ile sura ya Kayumba wakati Rita akielekea kumtangaza mshindi. Alikuwa na hofu, alifumba macho kwa hisia. Bila shaka aliamini “ile siku” ilikuwa inawadia. Alipotangazwa, alimrukia Nasibu kwa furaha. Naam, yalikuwa yametimia.

Ni rahisi kupatia kuwa ile furaha haikuwa tu kushangilia ushindi, bali maisha kwa jumla. Sh50 milioni sio mzaha jamaa yangu. Kayumba aliona maisha ameyapatia. Inafika 2020, stori inakuja tofauti kuwa Sh50 milioni hakuziona. Alidanganywa nyumba na mpaka leo hata hati haioni. Alipewa gari skrepa. Akauza chuma chakavu. Kumbe Madam Rita ndivyo ulivyo?

Waza kama Mtanzania; muone yule kijana ambaye ana maisha hohehahe. Wazazi wanaishi kwa kujisukuma. Hawawezi hata kujiendesha. Yule kijana ana ndoto na kipaji. Anaamini kipaji chake kingebadili maisha yake na kuwafaa wazazi wake.

Yule kijana aliona tangazo la kushiriki shindano la BSS. Akapata matumaini kuwa huenda BSS ingebadili maisha yake. Akajitokeza kwenye mchujo, akavuka mpaka kupata tiketi ya ushiriki wa shindano. Akashindana kwa kujituma, akiamini ushindi wake ndio maisha yake. Vile Mungu hubariki juhudi za waja, basi akashinda.

Baada ya ushindi, yule kijana anafurahia mavuno ya jitihada zake. Familia, hasa wazazi, wanawaza yale mamilioni. Wanajiona wameukata. Majirani na marafiki wanamtazama kwa jicho la kumnyali. Wanamuona tajiri. Si mwenzao tena!

Siku zinapita, kila kitu kinaonekana ilikuwa ndoto ya mchana. Mshindi wa Sh50 milioni, anaishi kwa tabu kuliko mwenye kipato cha Sh300,000 kwa mwezi. Na ile hulka ya walimwengu, kuteta na kusengenya, basi mshindi wa Sh50 milioni anaanza kuchekwa na kusimangwa kuwa alichezea pesa, matokeo yake kafulia.

Muwaze Madam Rita, amekusanya pesa za udhamini na kutulia nazo. Mshindi anadai fedha za ushindi, anaambiwa mwezi ujao, kisha mwezi ujao, halafu mwezi ujao.

Rita yeye anaishi vizuri alhamdulillah. Anaongoza kampuni, analipa mishahara. Mtoto wake hapati tabu kuishi mjini. Alimpeleka shule nzuri. Mwanaye hapati tabu kusafiri kwenda Ulaya au Marekani.

Rita anashindwa kuelewa kuwa yule mshindi wa BSS ile zawadi ya ushindi ndio bingo ya maisha yake. Inatazamwa na familia yake yote. Kweli, mtoto huyo wa maskini ni wa kufanyiwa hivyo?

Tumemuona Meshack, kisha Kayumba, wengine je? Tunahitaji sanitizers tutakase mikono kuepuka virusi vya SARS Corona 2. Kwa Rita, hiyo sanitizer hata aoge, hatajitakasa hii kashfa ya kudhulumu zawadi za washindi BSS.

Ndimi Luqman MALOTO
 
Bila kujua hili anamtengenezea mwanae future mbaya sana... Karma daima humrudia mtesi na ikikukosa damu yako inahusika

Jr[emoji769]
 
inaumiza kwakweli geto lenyew analokaa huyo dogo la masela hatauhakika wa kula sin hakika
 
Back
Top Bottom