Tetesi: Kikao cha dharura cha wakuu wa vyuo vyote vikuu nchini kinaendela mjini Dodoma , kuna tatizo kubwa

Tetesi: Kikao cha dharura cha wakuu wa vyuo vyote vikuu nchini kinaendela mjini Dodoma , kuna tatizo kubwa

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Kuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutanisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.

Hatua ya kuitia kikao hicho imetokana na hali mbaya ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini ambapo mara wanapoajiriwa katika sehemu mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ambazo zingine ni rahisi kabisa.

Wahitimu wengine wanashindwa kuandika barua za maombi ya kazi, kushindwa kufanya majaribio mbalimbali na hata pia kushindwa kuandika taarifa kwa kwa lugha ya Kiswahili na pia kwa lugha ya kiingereza.

Waziri wa elimu profesa Ndalichako ameamua kuitisha kikao hicho kujadili kuona wapi kuna tatizo.

Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili hali ya utoaji wa rishwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni ambapo huahidiwa alama za juu ili kufaulu mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa masharti ya kushiriki vitendo vya ngono na wahadhiri wao.

Ni muhimu taarifa kama hizi zikawekwa kwenye umma ili kuuelimisha kuhusiana na hali halisi ya kudorora kwa kasi ya juu kwa utaji wa elimu ya juu nchini na kuachia wanafunzi khasa wa kike kutegemea kutoa miili yao ili kupata alama nzuri.
 
Hitimisho la kikao ni nini sasa hapo
 
Tatizo liko huku kwenye mizizi. Lakini na maprofesa wa PhD wanataka kulitatua kule juu kileleni kwenye matawi.
Mimi ningeona wangeanza kujichungiza wenyewe kama hizo PhD zao ni za kweli.
You can't solve a problem by curing the symptoms.
Kuna shule wanafunzi wa FOM TUU (kidato cha 2) hawajui kusoma na kuandika. Tungeruhusiwa kufanya independent research sio ajabu tukakuta kuna form six hajui kusoma na kuhesabu.
 
Kuna riport moja hapa kazini niliifanyia Analysis... Wakataka irembwe zaidi. Wakawapelekea watu wa kwenye tawi waifanye, hawakuweza hata robo. Yeye mwenyewe aliyenilekekeza wapi pa kuanzia alipopewa data set afanye analysis amepotea hewani mpaka leo hakuweza ku analyse ile report.

Haya mambo haya ya kitaalam wanayaweza watu wachache sana. Watu wengi wana uwezo wa kati...
 
Kuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutranisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.

Hatua ya kuitia kikao hicho imetokana na hali mbaya ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini ambapo mara wanapoajiriwa katika sehemu mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ambazo zingine ni rahisi kabisa.

Wahitimu wengine wanashindwa kuandika barua za maombi ya kazi, kushindwa kufanya majaribio mbalimbali na hata pia kushindwa kuandika taarifa kwa kwa lugha ya Kiswahili na pia kwa lugha ya kiingereza.

Waziri wa elimu profesa Naalichako ameamua kuitisha kikao hicho kujadili kuona wapi kuna tatizo.

Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili hali ya utoaji wa rishwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni ambapo huadiwa alama za juu ili kufaulu mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa masharti ya kushiriki vitenndo vya ngono na wahadhiri wao.

Ni muhimu taarifa kama hizi zikawekwa kwenye umma ili kuuelimisha kuhusiana na hali halisi ya kudorora kwa kwa kasi ya juu kwa utaji wa elimu ya juu nchini na kuachia wanafunzi khasa wa kike kutegema kutoa miili yao ili kupata alama nzyri.
Uendeshaji wa elimu hapa Tanzania wapewe kanisa Katoliki waiendeshe angalau kwa miaka 10 ili waweke msingi thabiti halafu ndio serikali ikabidhiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo ya wahitimu ni kisingizio tu.

Hoja walioijia hapo ni rushwa ya ngono na maadili tu.

Wasidanganye watu.
 
Back
Top Bottom