Wanapoteza muda na pesa za walipa kodi. Tatizo ni kwamba wizara inataka kukusanya kutoka isipotawanya.. bhaasi. Wizara inasimamiwa na profesa lakini ana mtizamo kama wa mbuni, kufunika kichwa kwenye mchanga.
Tatizo ni kwamba serikali inakwepa jukumu muhimu kuwekeza kwenye vyuo vikuu, haijengi miundombinu, haiajiri wanataaluma, waliopo ni wazee na hawalipwi inavyostahili. Wanafunzi ni wengi kupindukia uwezo wa vyuo katika kila namna. Mwanataaluma anafundusha wanafunzi 500+, atoe assignments 2, seminars 2, labwork 3, theory test 2, final exam 1, asimamie yeye, asahihishe yeye, atoe matokeo yeye, na ahakikishe kila mwanafunzi aliye na tatizo analitatua kikamilifu.. Huo ni uongo na haiwezekani kamwe.
Tatizo wasomi wamekuwa wanafiki mno, hayo hawayasemi, wanaishia kuchakachua elimu. Ndo maana si ajabu kukutana na mhitimu asiyewezaandika barua ya kuomba kazi
Uhuni mtupu. Tatizo wanalijuwa, hakuna mchawi mwingine tofauti na serikali