Kuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutranisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.
Hatua ya kuitia kikao hicho imetokana na hali mbaya ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini ambapo mara wanapoajiriwa katika sehemu mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ambazo zingine ni rahisi kabisa.
Wahitimu wengine wanashindwa kuandika barua za maombi ya kazi, kushindwa kufanya majaribio mbalimbali na hata pia kushindwa kuandika taarifa kwa kwa lugha ya Kiswahili na pia kwa lugha ya kiingereza.
Waziri wa elimu profesa Naalichako ameamua kuitisha kikao hicho kujadili kuona wapi kuna tatizo.
Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili hali ya utoaji wa rishwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni ambapo huadiwa alama za juu ili kufaulu mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa masharti ya kushiriki vitenndo vya ngono na wahadhiri wao.
Ni muhimu taarifa kama hizi zikawekwa kwenye umma ili kuuelimisha kuhusiana na hali halisi ya kudorora kwa kwa kasi ya juu kwa utaji wa elimu ya juu nchini na kuachia wanafunzi khasa wa kike kutegema kutoa miili yao ili kupata alama nzyri.