Kuna kasumba moja vijana wa vyuo wanayo wanapokuja field! Namna wanavyo behave ni kama wengine wote hawajawahi kufika chuo ila wao tu! Ndiomaana ni wachache sana wanakuwa na utayari wa kuuliza au kuomba waelekezwe jambo fulani. Na hii ni kwa karibu fani zoteUkimchukua manafunzi wa IT au Engineer ambao wapo mwaka wa mwisho,waulize swali hili "Hivi wewe mpaka sasa unajua nini au umespecilize ktk eneo gani",huwezi amini hili swali 90% watashindwa kukujibu watakwambia "mimi najuajua",wamesahau ktk dunia hii ya sasa ambayo teknolojia inakuwa kwa kasi unatakiwa UJUE HASWA.
Kuna madogo walisoma Electronics and Commubication,Telecommunication Engineering walikuja field nikawaulizwa swali kama hili,wote walishindwa kunijibu na wengi wao wana amini kazi watajulia kazini,chuoni wameenda kutafuta GPA za kukariri.
Basi huwaga unawashauri vitu vya kusoma,unawapa softwares kwa ajili ya kufanya practical,unawapa tutorial za online,vitabu, unawa ambia ukishindwa ni ulize nikuelekeze,lkn hawakufuati wanakuja field hawabebi hata PC.Wapo wapo story zao series,madem na mabash unawatizama unawaonea huruma,sababu mtaani kugumu sana.
Ki ukweli system yetu ya elimu inahitaji maboresho makubwa sana! Huwa nawatania wenzangu wanitajie vitu walivyosoma chuo ambavyo hadi sasa bado wanavi-apply kwenye kazi zao ofisini
Chuoni unasoma ma vitu mengi lakini huyatumii yote! Na mwisho wa siku unaweza kuwa uko vizuri kwenye unit mojawapo GPA ikakukosesha kazi
Sent using Jamii Forums mobile app