Tetesi: Kikao cha dharura cha wakuu wa vyuo vyote vikuu nchini kinaendela mjini Dodoma , kuna tatizo kubwa

Tetesi: Kikao cha dharura cha wakuu wa vyuo vyote vikuu nchini kinaendela mjini Dodoma , kuna tatizo kubwa

Tatizo lipo wazi kama meno ya ngiri waache kupoteza pesa kwa ajili ya vikao. NECTA wanapoamua kuafulisha wanafunzi wengi kwa kufanya standardization kwa mitihani ya form four na form six. Usimamizi mbovu wa mitihani ya darasa la saba ili watoto wote wafaulu na serikali ipate sifa.Hapo lazima vyuo vipate watu wabovu na hao wakisha fika vyuoni hawakamatiki tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
La mikopo ya wanafunzi haina maana

Anyway, elimu ya kwetu ya kukremishwa tu ndio mana hata tunashindwa ku compete na jirani zetu ambao kwao intelligence yao iko juu sana na wanajua kujieleza na wana confidence

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili la graduate makazini ni tatizo liangaliwe kwakweli wahitimu wa sasa wanasomea wapate vyeti na kuvaa joho wapige picha lakini field ni utumbo mtupu

Sent using Jamii Forums mobile app
Zile diploma za zamani huwezi kulinganisha na degree za mwendokasi za sasa. Kuna mzee tulikuwa naye ofisini, amestaafu kwa sasa. Akiwa ofisini hata kama haupo wala huna wasiwasi, wakati mwingine nikiwa hata na shaka kidogo na hii Masters yangu lazima nipate opinions kutoka kwake hasa kwenye ishu za field. Hawa wahitimu wa sasa kata-K sijui tutafika wapi...
 
Hiyo ya wahitimu ni kisingizio tu.

Hoja walioijia hapo ni rushwa ya ngono na maadili tu.

Wasidanganye watu.
Yule wa digrii ya "korosho" asiye na uwezo wa kutema ngeli alitoa rushwa ya ngono pia?
 
Kuna binti alikuwa ana shahada ya uhasibu kutoka chuo kikuu kimojawapo nchini. Aliomba kazi katika taasisi ndogo binafsi. Waajiri wakapiga simu kwa mkufunzi wake alieandikwa kama mdhamini(referree) kujiridhisha juu ya uwezo wa kitaaluma.

Huyo mhadhiri aliwathibitishia kwa msisitizo kuwa binti aajiriwe yupo vizuri.

Binti aliajiriwa. Lakini ilipita miezi 12 vitabu vilivyoandikwa ni vya kupokelea na kulipia fedha tu.

Alipoulizwa, ni kulia tu bila maelezo. Kwa hali hii kwanini kazi zetu zisichukuliwe ma wageni?

Ukweli wahusika wafanye hima kutekebisha hali. Maana ukipanda bangi utavuna bangi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatafuta mchawi wakati mchawi wanamjua.

..........Mitihani ya kidato cha nne inarudiwa kusahishwa ili wanafunzi wafaulu, Wastani wa ufaulu unashushwa, shule hazina walimu wa kutosha, maslahi ya walimu.
 
Tatizo la wahadhiri wengi wa vyuo vya Tanzania ni kuwa wengi waliajiriwa based mainly on their class performance bila kuweka msisitizo kwenye umuhimu wa practical experience.

Kwahiyo, imagine unafundishwa na mhadhiri mwenye first class but ufahamu wake kuhusu ulimwengu halisi ni mdogo sana. Hii ndiyo inayopelekea wanafunzi wengi wanapomaliza chuo na kuingia mtaani wanapata shida ku-cope na mazingira ya kazi.

Sababu nyingine ni kwamba, vitu vingi vinavyofundishwa kwenye vyuo vingi vya Tanzania vimepitwa na wakati, ingawa theoretically bado vipo viable. Mfano, katika ulimwengu wa sasa, huwezi kumfundisha mwanafunzi Bachelor degree ya Statistics bila kuweka kwenye mitaala masomo ya Data Science, data analytics. Kwahiyo, ili uwe comptent person kwenye statistics lazima uwe mzuri kwenye IT programming zinazo-deal na data, plus data analytics tools....hata za MS Excel zinatosha sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hili swala nilijua tu linaweza kuwa tatizo huko mbeleni, ikiwa mwanafunuzi anatahiniwa maswalli ya kuchagua mpaka kwenye hesabu saa ngapi ataweza kubrainstorm? mitihani ya siku hizi hasa shule ya msingi na secondary sidhani kama, inapima ufahamu zaidi ya uwezo wa kukariri. Maswali ya kuumiza kichwa kufikiria ni macheche hivyo tunapata wahitimu ambao hawawezi kijieleza.
 
Hizo barua za amombi ya Kazi wanazianfika kuomba kazi gani?

Magu anaajiri madereva na JKT tu.
Nenda website ya utumishi utakuta kazi zinazotangamwa ni madereva

Sehemu mbalimbali.

Waajiri wakati mwingine huamua kukubali baadhi ya maombi kwa lengo la kutaka kumuendeleza mwajiriwa.

Lakini inapokuja suala la kufanya kazi mbalimbali au tasks ambapo mambo kama kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzio, au team work, kazi za kutumia hesabu, kuandika taarifa au report na vingine inakuwa ni shida sana.

Kwenye lugha ya Kiswahili kuna matatizo ya kukosea maneno au herufi au hata kuandika kifungu cha maneno au paragraph na kutenganisha vifungu hivyo pamoja na sentensi.

Kwenye kuandika barua ya kiingereza au ya Kiswahili kuna tatizo la kutofahamu wapi ikae anuani ya mtumiwa barua na wapi kwa anuani ya mtuma barua.

Mtu wa namna hiyo utakuta ana alama ya za juu kwenye transcripts na shahada ya nguvu ya upper second au hata first class..

Wanapoamua kupitia upya vyeti vya mhusika na kulinganisha alama alizofaulu kwenye eneo husika na kuna kuwa na tofauti kubwa.

Masuali ndipo huanzia hapo juu ya uwezo halisi wa mwajjiriwa husika.
 
Hivi hili jambo huwa linasemwa, lina ukweli wowote?

Mwanamke anabaka! Anabakabakaje kwa mfano?

Ukibadili neno na kusema anashawishi ili kuhiyari tendo ama kwa vitisho, hilo lawezekana kubaka kisaikolojia, lakini siyo kubaka live kama 'baka' tunayoiongelea.

Na ndiyo maana kuanzia mashuleni wasichana kujazwa mimba,pamoja na hii sheria kandamizi ya miaka 30 jela, inayotumika sasahivi, wanawake haiwahusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maelezo yale ni mapana na ni technical, nikiwa na muda nitaeleza vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutanisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.

Hatua ya kuitia kikao hicho imetokana na hali mbaya ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini ambapo mara wanapoajiriwa katika sehemu mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ambazo zingine ni rahisi kabisa.

Wahitimu wengine wanashindwa kuandika barua za maombi ya kazi, kushindwa kufanya majaribio mbalimbali na hata pia kushindwa kuandika taarifa kwa kwa lugha ya Kiswahili na pia kwa lugha ya kiingereza.

Waziri wa elimu profesa Ndalichako ameamua kuitisha kikao hicho kujadili kuona wapi kuna tatizo.

Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili hali ya utoaji wa rishwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni ambapo huahidiwa alama za juu ili kufaulu mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa masharti ya kushiriki vitendo vya ngono na wahadhiri wao.

Ni muhimu taarifa kama hizi zikawekwa kwenye umma ili kuuelimisha kuhusiana na hali halisi ya kudorora kwa kasi ya juu kwa utaji wa elimu ya juu nchini na kuachia wanafunzi khasa wa kike kutegemea kutoa miili yao ili kupata alama nzuri.
I have nothing to comment
Wacha tuu nicheke [emoji23]

Maana hilo tatizo ni Pana Sana
Mabadiliko yanahitajika kwa Sehem kubwa
Sina uhakika na Solutions watakazo toka nazo hapo
 
Hapo ndio penyewe.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo nalo neno mkuu..

Ili hayo yaweze kufanyika lazima vitu kadhaa vitokee
1. Kufumua mitaala inayotumika kwa sasa maana ni ya karne ya 20. Kilichofanyika kwa kushirikiana na TCU ilikuwa ni kupiga viraka nguo kukuu. Mwisho wa siku mitaala inabakia na mtazamo ule ule, wa kizamani.
Wahitimu waliotokana na mitaala ya zamani hawawezi kushindana na wale walifundishwa kwa kutumia mitaala ya kisasa. Kuthibitisha hilo, vijana wa kichina, kihindi na kizungu wako hapa nchini wakifanya kazi nyingi katika miradi mbali mbali, kazi ambazo zinawahusu vijana wa kitanzania. Tatizo tu ni kwamba largely, hawana sifa stahiki, maana yake walichojifunza siyo

2. Kubadilika kutoka elimu ya nadharia kwenda kwenye elimu ya vitendo. Hili naliunga mkono tena sana. Hili litafanyika endapo mitaala itaboreshwa pia. Zaidi katika hili ni kiwango cha uwekezaji kinachotakiwa. Elimu ya vitendo haifanyiki kwenye hostel au katika kumbi tupu za mihadhara. Elimu kwa vitendo inafanyika kwenye maabara na karakana zilizoboreshwa, zenye usimamizi wa kitaalam.

Katika haya mawili, serikali huwa inafunika kombe ili mwana haram apite badala ya kuja na mkakati wa kuwekeza pesa. Tukisema pesa zilizowekezwa kwenye ndege zilikuwa totally misallocated, kuna vi/aza fulani hutokwa povu. Kuwekeza kwenye elimu ndio kuwekeza kimkakati, hayo mengine ni kupoteza fursa za nchi kujikwamua

Asante kwa mchango
 
Kuna tetesi kuwa kikao cha dharura kimeitishwa mjini Dodoma kinachowakutanisha wakuu wote wa vyuo vikuu nchini.

Hatua ya kuitia kikao hicho imetokana na hali mbaya ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini ambapo mara wanapoajiriwa katika sehemu mbalimbali wanashindwa kufanya kazi ambazo zingine ni rahisi kabisa.

Wahitimu wengine wanashindwa kuandika barua za maombi ya kazi, kushindwa kufanya majaribio mbalimbali na hata pia kushindwa kuandika taarifa kwa kwa lugha ya Kiswahili na pia kwa lugha ya kiingereza.

Waziri wa elimu profesa Ndalichako ameamua kuitisha kikao hicho kujadili kuona wapi kuna tatizo.

Pia kikao hicho kinatarajiwa kujadili hali ya utoaji wa rishwa ya ngono kwa wanafunzi wa kike vyuoni ambapo huahidiwa alama za juu ili kufaulu mitihani yao ya mwaka wa mwisho kwa masharti ya kushiriki vitendo vya ngono na wahadhiri wao.

Ni muhimu taarifa kama hizi zikawekwa kwenye umma ili kuuelimisha kuhusiana na hali halisi ya kudorora kwa kasi ya juu kwa utaji wa elimu ya juu nchini na kuachia wanafunzi khasa wa kike kutegemea kutoa miili yao ili kupata alama nzuri.

CCM hoyeee! Ndio chama pekee kinachoweza kutuingiza karne ya ishirini na moja kifua mbele,namba tumeisoma wote!
 
Ukimchukua manafunzi wa IT au Engineer ambao wapo mwaka wa mwisho,waulize swali hili "Hivi wewe mpaka sasa unajua nini au umespecilize ktk eneo gani",huwezi amini hili swali 90% watashindwa kukujibu watakwambia "mimi najuajua",wamesahau ktk dunia hii ya sasa ambayo teknolojia inakuwa kwa kasi unatakiwa UJUE HASWA.

Kuna madogo walisoma Electronics and Communication,Telecommunication Engineering walikuja field nikawaulizwa swali kama hili,wote walishindwa kunijibu na wengi wao wana amini kazi watajulia kazini,chuoni wameenda kutafuta GPA za kukariri.

Basi huwaga unawashauri vitu vya kusoma,unawapa softwares kwa ajili ya kufanya practical,unawapa tutorial za online,vitabu, unawa ambia ukishindwa ni ulize nikuelekeze,lkn hawakufuati wanakuja field hawabebi hata PC.Wapo wapo story zao series,madem na mabash unawatizama unawaonea huruma,sababu mtaani kugumu sana.
 
Back
Top Bottom