Vito...
Dots katika kanuni za uandishi unaandika tatu tu...
Nimefurahi kuwa katika yote niliyoeleza katika historia hii ulichokiona kikubwa kwako ni kuuliza kwa nini Abdul hakujitoa katika uchaguzi ule.
Hili swali lishaulizwa hapa mara kadhaa na nimelijibu.
Ulikuwa unaijua historia hii?
Historia ya African Association (AA) 1929 hadi kufikia TANU 1954 ina uhusiano mkubwa sana na ukoo wa Sykes kama waasisi na wafadhili wake.
Abdul angejitoa uchaguzi ule dhidi ya Nyerere wanachama wangehisi kachukia na kasusa na hii ingevuruga murua wa TAA na pengine kukiridusha chama nyuma sana.
Abdul alikuwa anaungwa mkono na wanachama wengi kutoka 1950 alipoingia katika uongozi na Dr. Vedasto Kyaruzi.
Kujitoa katika uongozi katika kipindi kile cha uchaguzi isingekuwa kitu cha busara.
Nyerere pale anaingia katika uchaguzi hakuwa anajulikana Dar es Salaam.
Judith Listowel kakielez kisa hiki vizuri sana katika kitabu chake, ''The Making of Tanganyika, '' (1965).
Sikiliza maneno ya Hamza Mwapachu kwa Abdul Sykes kuhusu uchaguzi uliokuwa mbele yao na umuhimu kwa kuunda TANU katika uchaguzi ujao wa 1954.
Kwa nini umeshughulishwa na kujitoa kwa Abdul na siyo imekuwaje historia ya TANU imeandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni Abdul Sykes na Hamza Mwapachu hawakutajwa katika kitabu hicho?
Au huamini kuwa haya niliyoeleza ndiyo historia ya kweli ya TANU?
Hivyo vitabu hapo chini kuhusu historia ya TANU vinatoka kwenye chanzo kimoja.
Kitabu cha Abubakar Ulotu kimenakiliwa kutoka mswada uliokuwa katika maktaba ya TANU ulioandikwa na Dr. Wilbard Klerruu 1962/63.
Kitabu Chuo Cha Kivukoni hakiko tofauti sana na kitabu cha Ulotu.
Vitabu vyote hivi viwili vinatokana na mradi wa TANU wa kuandika historia yake ambao mwandishi mkuu alikuwa Abdul Sykes akisaidiwa na Dr. Kleruu lakini kwa bahati mbaya Abdul akajitoa katika kazi hii.
Dr. Klerruu akakamilisha mswada lakini haukukuchapwa.
Kitabu cha Abubakar Ulotu inaaminika unatokana na mswada huu.
View attachment 2218707